mohamedidrisa789
JF-Expert Member
- Jun 20, 2015
- 5,613
- 23,745
Ndio, roof coating zina madaraja yake na huwa inawakilisha uwezo wa bati kustahmili moto (fire resistance). Kuna class A, Class B na Class C ambapo class A ndio ina uwezo mkubwa wa kustahmili moto kuliko class zingine na class C ndio ina uwezo mdogo wa kustahmili moto kulinganisha na hizo class zingine. Hiyo Class D binafsi sijawahi kukutana nayo, labda kama ni daraja jipya wamelianzisha hivi karibuni au labda lipo lakini ni adimu kuonekanandugu Hechy Essy kuna mahali nimeona mabati ya mgongo mpana limeandikwa hivi coating class D
kumbe hizi rangi zina class yake?
ahaa nikajua ni ubora wa rangi ya batiNdio, roof coating zina madaraja yake na huwa inawakilisha uwezo wa bati kustahmili moto (fire resistance). Kuna class A, Class B na Class C ambapo class A ndio ina uwezo mkubwa wa kustahmili moto kuliko class zingine na class C ndio ina uwezo mdogo wa kustahmili moto kulinganisha na hizo class zingine. Hiyo Class D binafsi sijawahi kukutana nayo, labda kama ni daraja jipya wamelianzisha hivi karibuni au labda lipo lakini ni adimu kuonekana
Zile mbao tatu huwa zinaugwa vipi, zile ngazi zinatokea pande mbili?.Ukiweka 6 4 4 bado itaonekana kama ngazi mbili, labda uweke 6 5 4 kwa maana ya 1x6, 1×5 na 1x4
Ngazi zinatokea upande mmoja tu, upande wa juu mbao zote zinakuwa zinaflash, kwa hivyo upande wa chini ngazi zinatokea automatically kwa kuwa mbao zinapishana upanaZile mbao tatu huwa zinaugwa vipi, zile ngazi zinatokea pande mbili?.
Safi mkuu kwa maelezo mazuri..Plaster nzuri ni ile ambayo ukimwagia ukuta maji, ukuta unakauka bila kuchora alama za matofali. Kiujumla michoro ya tofali katika ukuta uliopigwa plaster hutokea pale ratio ya udongo uliotumika kujengea tofali ni kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kupigia plaster
Kitaalam udongo wa kujengea tofali tunatumia ratio ya 1:6 na udongo wa kupigia plaster tunatumia ratio ya 1:4 na 1:5 (ratio ya 1:4 inatumika kwenye kuta upande wa nje, na 1:5 upande wa ndani)
Ratio ya plaster inatakiwa iwe kali kuzidi ratio ya udongo uliotumika kujengea
Kwa mahitaji ya ramani, makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
KazuriPLN 0001 2BR
Ramani ya Vyumba Viwili
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana
- Living room (Sebule)
- 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
- 1 Single bedroom
- Kitchen (Jiko)
- Public toilet (Choo cha jumuiya)
Bei: Tsh. 100,000/=
Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Hapo inategemea na size ya tofali (urefu, upana na unene) pamoja na idadi ya tofali unazotaka kutengeneza kwa kila mfuko mmoja wa cementSa
Safi mkuu kwa maelezo mazuri..
Naomba nikuulize, hivi ratio ya udongo wa kutengenezea/kufyatulia tofali inapaswa kuwa ngapi..?
Je ni sahihi kutumia mbao za size moja kwa paa kama hili. (mfano 2*3 zote au 2*4 zote)..?Hapo inategemea na size ya tofali (urefu, upana na unene) pamoja na idadi ya tofali unazotaka kutengeneza kwa kila mfuko mmoja wa cement
Sio sahihi,Je ni sahihi kutumia mbao za size moja kwa paa kama hili. (mfano 2*3 zote au 2*4 zote)..?View attachment 3463866
kuna ulazima wa kuweka public toilet ikiwa room zote ni selfNyumba ya vyumba viwili yenye sebule, jiko, dining, public toilet na store inaweza isiwe na utofauti au zikazidiana kidogo katika gharama na Nyumba ya vyumba vitatu yenye sebule, jiko na public toilet.
Kama unataka kujenga nyumba ndogo kwa lengo la kupunguza gharama, basi angalia vitu vya ulazima kuwepo. Jiko lazima liwepo, choo lazima kiwepo, sebule lazima iwepo, dining room ni optional kwa maana watu wanaweza wakalia chakula sebleni, store pia ni optional kwa maana unaweza ukajenga jiko kubwa kidogo ili kusiwe na ulazima wa kuwepo store.
Hii ni kwa kujenga nyumba ndogo kwa lengo la kupunguza gharama vinginevyo unaweza ukavijumuisha tu na hivyo vyumba ambavyo ni optional kuweka.
Kama choo cha nje hakipo, basi kuna ulazima wa kuwepo public toilet ndani ya nyumba vinginevyo itamlazimu mgeni aingie chumbani ili aende chooni kitu ambacho sio kizuri kiusalama.kuna ulazima wa kuweka public toilet ikiwa room zote ni self
Mkuu, unataka kusema hata miti ya matunda itakuwa inafatwa na hao viumbe kwa sababu ya sukari?Kuna hii miti ya kisasa ya kivuli ambayo inakuaga na vitunda vidogo vya rangi nyekundu, Nyoka huwa wanaipenda sana. Nadhani huwa wanafuata hivi vitunda (sina uhakika, lakini nilijaribu kuvionja nikagundua kuwa vina sukari, hata Ndege pia wanavipenda sana)
Hapa ninapoishi kuna hii miti ya kivuli miwili, na ndani ya wiki moja tu nimeua Nyoka watatu, mmoja katika hao ni mrefu anazidi futi 4 kwa hivyo ni vyema sana kuwa makini na hii miti.
Usiruhusu mti ukawa mkubwa mpaka kufikia hatua matawi yakawa yanakaribia ama kugusa kuta za nyumba kwani itakuwa rahisi Nyoka kuingia ndani ya nyumba kupitia dirishani au sehemu yoyote iliyo wazi na mara nyingi hawa Nyoka huwa utawaona kipindi cha baridi au mvua inaponyesha (wanatafuta hifadhi katika majumba baada ya mashimo/miti kuloana na maji)
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane