yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,919
- 4,174
Hapa sijaelewa mkuu. Huu ufa unakata na grenda? Je unakata mpaka unatokea upande wa pili? Ukikata kila sehemu yenye dirisha hupunguzi uimara wa nyumba?Katika nyumba, kuna zile sehemu ambazo uwezekano wa kutokea nyufa katika kuta ni zaidi ya asilimia 80. Hii ni kutokana na utofauti wa kiwango cha stress kati ya eneo moja na eneo jingine katika jengo, sehemu zingine zina stress ndogo na sehemu zingine zina stress kubwa.
Mfano mzuri wa hizi sehemu ambazo zina uwezekano mkubwa wa kutokea kwa nyufa ni chini ya uwazi wa madirisha, ni moja kati ya sehemu dhaifu mno katika jengo ambapo ikitokea movement yoyote, nyufa zinaanza kutokea hapo.
Mara nyingi nyufa huwa zinatokea katika pattern ya zig zag, sasa huwa tunaweka hivi chini ya uwazi wa madirisha (kati kati) ili hizi nyufa za zig zag zisitokee, kiufupi ni kama tunatengeneza ufa wetu wenyewe ambao unakuwa umenyooka kabla huo ufa halisia (zig zag) haujaja.
Hii tunaita Control Joint
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasilianeView attachment 3476210
Je huu ufa unafanyaje kazi ya kuzuia hizo nyufa za zigzag?