Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 860
- 3,238
- Thread starter
- #1,261
Nahisi alimaanisha kuanzia hatua ya msingi mpaka hatua ya upauajiMkuu 25M nyingi sana ata ukitumia ALAF ile ya 22k kwa meter bado unabakiw na chench ya 10M
Nahisi alimaanisha kuanzia hatua ya msingi mpaka hatua ya upauajiMkuu 25M nyingi sana ata ukitumia ALAF ile ya 22k kwa meter bado unabakiw na chench ya 10M
Acha uta i so kumbe nimekalia nyumba hapa mfukoniMkuu 25M nyingi sana ata ukitumia ALAF ile ya 22k kwa meter bado unabakiw na chench ya 10M
Ndio hivyo mkuu kuanzia msingi mpaka kupauaNahisi alimaanisha kuanzia hatua ya msingi mpaka hatua ya upauaji
iyo RCD inafungwa wapi?Katika mfumo wa umeme, kuna kifaa kimoja kunaitwa Residual Current Device (RCD). RCD ni mojawapo ya aina za vifaa vya kulinda mfumo wa umeme (circuit breakers) ambacho huwa kinakata umeme pindi shida flani inapojitokeza.
Kifaa hiki watu wengi huwa wanakipuuzia kukiweka katika mifumo yao ya umeme lakini kiuhalisia kina faida kubwa sana kiusalama.
RCD huwa inafanya kazi ya kulinganisha umeme unaotoka (kupitia waya wa live) na umeme unaorudi (kupitia waya wa neutral). Kitaalam current inayotoka inatakiwa iwe sawa na current inayorudi kwa hivyo ikitokea kuna utofauti wa kiasi cha hizo currents mbili katika circuit husika, RCD inatafsiri kwamba kuna mahali umeme unavuja na hivyo inakata umeme (kutrip) usiendelee kutembea.
Utofauti wa hizo currents unaweza ukasababishwa na mambo mengi lakini moja wapo katika hayo ni mtu kushika waya wenye moto ambapo inafanya umeme upate njia nyingine ya kupita (kupitia mwili wa binadamu) hivyo kufanya kiasi cha umeme kilichotoka kisifanane na kiasi cha umeme unaorudi. RCD inatumia muda mdogo sana (chini ya robo sekunde) kutrip kwa hivyo kama ilikuwa ni mtu ndio ameshika waya bahati mbaya, RCD itakata umeme na mtu ataweza kusalimika na short ambayo pengine ingeweza kumsababishia madhara makubwa au hata kifo kutokana na kutowepo kwa hicho kifaa (RCD)
Watu wengi hudhani kwamba MCB inaweza ikamlinda mtu asipigwe short kitu ambacho sio kweli, MCB inatrip pale inapotokea kuna Overloads katika vifaa vya umeme au inapotokea short circuit.
Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
Hiki kifaa unaweza pia nunua online Kikuu, mimi nilinunua KIKUU kwa 10,000 kinapiga kazi fresh mwaka wa nne huuNi kweli kabisa bei yake kawaida huwa shingap
Inafungwa ndani ya Distribution board (main switch), kimuundo haina tofauti sana na circuit breaker ya kawaida (MCB) isipokuwa kazi zao ndio zinatofautiana.iyo RCD inafungwa wapi?
Unaweza kufunga vyote viwili (RCD na Circuit Breaker) kwa pamoja?Inafungwa ndani ya Distribution board (main switch), kimuundo haina tofauti sana na circuit breaker ya kawaida (MCB) isipokuwa kazi zao ndio zinatofautiana.
Ndio, kiusalama inabidi viwepo vyote viwili kwa kuwa kila kimoja kina kazi yake. Kuna kifaa kimoja ambacho kinaweza kufanya kazi za hao wote wawili (MCB na RCD) kinaitwa RCBO (Residual Current Breaker with Overcurrent protection).Unaweza kufunga vyote viwili (RCD na Circuit Breaker) kwa pamoja?
Hiki kifaa unaweza pia nunua online Kikuu, mimi nilinunua KIKUU kwa 10,000 kinapiga kazi fresh mwaka wa nne huu
Yah ni kweli, photocell nyingi zina hii changamoto au hata umeme ukikatika usiku then ukarudi, photocell zingine zinashindwa kuwasha taa ndio maana inatakiwa katika ufungaji wa photocell kuwepo na switch ambayo utaamua taa zako zijiwashe automatically au manually ili in case kama photocell imejiwasha mchana kutokana na giza la mawingu uweze kuzima taa manually kwa kutumia hiyo switchHii Photocell uwa sio salama sana na hali ya ewa pia changamoto yake kubwa ni mabadiliko ya hali ya hewa.kama hata mchana wingu likiwa kubwa basi taa zinaweza kuwaka nchana
Mimi uwa siwanunulishi wateja iyo photocell, mimi uwa nawambia wanunue digital timer tena iwe ya Tronic au ABB ili ukifunga basi umefunga mkatabaUkiachana na kifaa cha Photocell ambacho kinawasha na kuzima taa kutokana na kiasi cha mwanga kilichopo eneo husika pia kuna kifaa kingine kinaitwa Timer Switch ambacho hiki unaset muda wa taa kuwaka na kuzima kama unavyoset alarm katika saa/simu (Unaweza ukatumia hii Timer switch kama mbadala wa Photocell kutokana na changamoto zake kadhaa ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi).
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Hizi ni baadhi ya Digital timer za single phase za tronic-uwa sijawai kusumbuliwa toka nizifunge ni mkataba kama zitasumbua basi baada ya miaka 5 mbele huko
Ratio ya plaster kwa kuta za nje tumia 1:4 (sawa na ndoo kubwa 8 kwa mfuko mmoja wa cement), na kwa kuta za ndani tumia 1:5 (sawa na ndoo kubwa 10 kwa mfuko mmoja wa cement). Lakini pia inategemea na mchanga wako jinsi ulivyo, wakati mwingine inakulazimu kupunguza idadi ya ndoo za mchanga ili kupata plaster inayoshika vizuriMkuu plasta inatakiwa iwe nch ngap? na resho ya plasta ni ngapi nyumba ya kawaida ya makazi
Kuhusu uwekaji wa kitchen vent, je ni bomba la material ipi linatumika kuwekwa ukutani kuanzia ilipo vent yenyewe hadi nje na huwa lina kipimo cha mm ngapi. Ni lazima lipite ukutani tu au linaweza kutokea juu ya ukuta na kutambaa kwenye dari hadi kuja kutokea kwenye overhang?.Kwa vifaa vya umeme ambavyo vinatumia umeme mkubwa kama vile A.C, pump ya maji, heater ya maji n.k unashauriwa utumie Double Pole switch (DP switch) badala ya hizi switch za kawaida (single pole switch).
DP switch mara nyingi button yake ya kuzima/kuwashia huwa ina rangi nyekundu (zipo nyeupe pia), na pia inakuwa na kitaa chekundu kwa juu ambacho huwa kinawaka switch inapokuwa ipo ON (imewashwa)
DP switch inapokuwa imezimwa, inazuia umeme katika nyaya zote mbili (live na neutral) hivyo inakuwa salama zaidi hata unapotaka kufanya marekebisho tofauti na switch za single pole ambayo inazuia umeme katika waya wa live pekee. Switch za single pole zinatumika katika vifaa vya umeme mdogo kama vile taa na feni
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Bei gani hii?Mimi uwa siwanunulishi wateja iyo photocell, mimi uwa nawambia wanunue digital timer tena iwe ya Tronic au ABB ili ukifunga basi umefunga mkataba