Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

kwa maan hapo hapakua na pipe level either kwenye lenta level
Ukiangalia vizuri, utagundua kwamba shida ilianzia mbali kabla hata ya kufikia level ya mkanda na kuna uwezekano huu ukuta wote umejengwa na fundi mmoja tu. Tofali zote ujengaji wake unafanana, hapo unakuta fundi kobilo anayo lakini kaiacha chini kwenye begi lake ili akimbizane na muda kazi iishe
 
Tako la litre elf ngapi ndjo linaweza wekwa juu ya canopy?
Kwa usalama zaidi, tank lisizidi lita 2000...kama unataka uweke tank kubwa zaidi ni heri ukajengea mnara pembeni ya nyumba mana slab ya kibaraza huwa inabebwa na tofali zilizosimamishwa, sio kulazwa
Mzee umeona balaa hili?

Device yako imekuwa addicted na hilo neno kiasi autocorrect inakataa hukuandika tank uliandika tako ingekuwa ndiyo ulikuwa umamjibu mama mkwe ingekuwaje?
 
Mzee umeona balaa hili?

Device yako imekuwa addicted na hilo neno kiasi autocorrect inakataa hukuandika tank uliandika ingekuwa ndiyo ulikuwa umamjibu mama mkwe ingekuwaje?
Nakwambia nikiwa nachata na mama mkwe uzuri anajua english so nachat nae english kukwepa mambo kama hayo
 
Hata mimi naona kabisa naelekea kuvunja paa la kuficha nipaue upya kawaida. Hata sielewi nilifikaje huko
Na bora sasa uwe bado una uwezo huo,fikiria kwa mtu ambaye hana uwezo wa kufanya kitu ajikute kwenye situation kama hii ni mtihani mzito.

Nilisoma mahali humu nyumba flat roof ilikuwa style hasa ya kujengwa kwenye majangwa sasa sijui kweli?
 
Umepigaje hapo kwenye round colum 4 imerokea wapi tena jamani hesabu hizi wenhine tulikimbia
Wakitumia pipe level katika kozi ya mwisho, napo kuna changamoto inaweza kutokea...wanaweza wakakuta kuta zinatofautiana kwa kiasi kikubwa hivyo italazimisha sehemu zingine wajaze udongo mwingi ili kuinua kuta ziende juu zaidi, na sehemu zingine waweke udongo kidogo sana ili kushusha kuta ziwe chini

Kama wakitumia pipe level kozi mbili kabla ya kufika mwisho, inasaidia kugawanya huo utofauti uliotokea na kuubalance udongo katika kozi zote mbili hivyo udongo unakuwa haurundikwi sehemu moja pekee (katika kozi moja)

Kuna level flani ya kuta ikishafika (mfano kozi ya 6 au ya 7), pipe level inatumika kutafuta level nyumba nzima na kutokea hapo kwenda huko juu, kozi zote zinakuwa zinatumia hiyo level iliyotafutwa kama reference japo pia katika zoezi la kufunga mkanda ni vizuri pia kuhakikisha level kama iko sawa
Pipe level ni nini mkuu?
 
Mtaalam...katika uwekaji watiles pale kibarazani, kipande kinatakiwa kiwe karibu na mlango wa kuingilia au kipande kiwe huku mwanzoni wa kibalaza? Fundi wangua naona simuelewi.
 
Pipe level ni nini mkuu?
Hii ndio Pipe level
Huu mpira unajazwa maji halafu levels za maji (mwanzo na mwisho wa mpira) katika huo mpira ndizo zinazotumika kutafutia level
20250409_063716.jpg
 
Mtaalam...katika uwekaji watiles pale kibarazani, kipande kinatakiwa kiwe karibu na mlango wa kuingilia au kipande kiwe huku mwanzoni wa kibalaza? Fundi wangua naona simuelewi.
Kama umetumia mfumo wa Square pattern, hapo vipande vitakuwa upande mmoja na vinatakiwa vifie ukutani
Na kama umetumia mfumo wa diagonal, vipande vitakuwa pande zote lakini allignment yake inatakiwa iwe katika namna ambayo zile nyuzi 90 za tiles hazitakuwa zinagusa mkanda (strip), zile angle 90 za tiles zikiwa zinagusa huo mkanda ni rahisi sana kukatika watu wakiwa wanakanyaga ndio maana wengine huwa wanaanza na square pattern kwenye edge zote za kibaraza then katikati ndio wanaweka diagonal pattern

Bila shaka hapo mlangoni kuna step (floor level ya sebule ipo juu kulinganisha na floor level ya kibaraza)
 
Umeeleweka mkuuu. Asante. Ngoja nipambane na huyu fundi michael
 
Dah kumbe. Hii nahisi mafundi wengi hawaiapply au pia hawaijui
Sidhani kama kuna fundi ambaye haijui pipe level, maana ndio kifaa cha bei nafuu zaidi katika matumizi ya aina hii.

Nadhani ni uvivu tu, na pia hiki kifaa matumizi yake ni lazima muwe watu wawili, sasa muda mwingine unakuta kazi ni ndogo na fundi yupo peke yake kwahivyo inakuwa ngumu kwake kukitumia
 
Siku hizi makampuni mengi yanayotengeneza bidhaa za ujenzi huwa wanawaahidi mafundi mgao (pesa) kwa kila mteja watakayempeleka dukani/kiwandani kununua material, sasa wewe kama boss inabidi uwe makini na ushauri wa fundi anaokupa maana fundi atakupeleka mahali ambapo ameahidiwa commision kubwa na sio masuala ya ubora wa material/bidhaa

Ramani, Makadirio, au Ushauri tuwasiliane
 
Mafundi wa mabati ndio kazi yao hiyo
 
Mafundi wa mabati ndio kazi yao hiyo
Kabisa, na nadhani bati ndio bidhaa ambayo inatengenezwa na kampuni nyingi kwa hapa kwetu kwa hivyo ushindani wake kwa hizi kampuni ambazo bado zinajitafuta ni mkubwa sana. Maafisa masoko wanaenda kutafutia wateja huko huko site
 
Tofali za msingi siku zote huwa zinalazwa, option ya kusimamisha au kulaza tofali ipo kwenye boma tu
mkuu naomba msaada wa viwanda vizuri vinavyotoa bati imara za vigae/ngazi,nami ntachagua kitakachoufaa mfuko wangu. Asante.@Hechy Essy
 
Je wajua, bati lina upande dume na upande jike?

Sasa katika upigiliaji, upande jike unatakiwa uwe juu ya upande dume. Ukifanya vice versa, mtu akipita nje atakuwa anaona bati zote zilipoanzia na zinapoishia (inapoteza mvuto, inakua kama umetandika mikeka) na kingine hata upepo ukipita juu ya bati, upepo utakuwa unakwama kwama kwenye maungio ya bati moja na lingine ambapo itakuwa rahisi kuezua bati

Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane
utofauti gani uliopo kati ya upande jike na dume?
 
Back
Top Bottom