Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Unaweza ukachagua kibaraza kimoja wapo (kati ya kibaraza cha mbele sebleni, au kibaraza cha nyuma jikoni) kuweka zege juu ili usiingie gharama ya kujenga mnara wa tank la maji pembeni ya nyumba, lakini kingine utakuwa ume-save eneo kwa ajili ya matumizi mengine.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Tako la litre elf ngapi ndjo linaweza wekwa juu ya canopy?
 
Na hili unalosema mie naonaga sana kwenye ramani which i feel inanyima nyuma mzunguko mzuri wa hewa maana inatokea upande mmoja tuu.

Sasa kwa mantiki hiyo, dirisha na mlango vinatakiwa kutazama north alafu madirisha mawili mingine yatizame east au west? Which is better? East au west?
Mkuu, hewa ya nje unaitaka ya kazi gani ndani ya nyumba ukizingatia nyumba yote ni vioo vitupu madirishani. Zaidi ya kukaribisha vumbi ndani, madirisha ni kwa ajili ya mwanga tu.
 
Tako la litre elf ngapi ndjo linaweza wekwa juu ya canopy?
Kwa usalama zaidi, tank lisizidi lita 2000...kama unataka uweke tank kubwa zaidi ni heri ukajengea mnara pembeni ya nyumba mana slab ya kibaraza huwa inabebwa na tofali zilizosimamishwa, sio kulazwa
 
Inategemea na ukubwa wa vyumba pamoja na kina cha msingi, kama ni vyumba vya ukubwa wa futi 10 kwa 10, kila kozi moja itachukua tofali 130. Hapo sasa utaangalia msingi wako utakuwa na kozi ngapi, ambapo utazidisha na hiyo 130 kupata jumla ya tofali za msingi

Mfano kama utajenga kozi 6, utatumia tofali 780 sawa na 130pcs/course x 6 courses
Hapa mbona sijaelewa mwanawane u apataje tofali 130 kwa kozi moya ya chumba cha 3m x 3m?

Maana tofali length yake ni 45cm
Perimenter ya chumba ni 12m. Sasa ukigawa hapo sii inakuja kama 26 hivi
 
Matundu katika kuta za msingi yanatakiwa yawekwe katika namna ambayo mtu akichora mstari wa kuunganisha hayo matundu, maumbo ya pembe tatu yatengenezeke kupitia hiyo mistari kwa maana ya kwamba matundu mengine yawe chini, na matundu mengine yawe juu kwa kupishana (yasifuatane kwa wima) ambapo mstari wa chini ndio utakuwa na matundu mengi kuliko mstari wa juu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Hapa tuwekee picha mzeya tuelewe vizuri
 
Ukienda kununua kiwanja, tafuta kiwanja ambacho marefu na mapana yake yanawiana kiasi flani mfano 20m x 25m, 30m x 30m n.k (kiwanja kisiwe chembamba mfano 10m x 20m n.k)

Maeneo mawili yanaweza kufanana square meters lakini yakatofautiana mzunguko (circumference). Sasa eneo zuri katika hayo mawili ni lile ambalo linakuwa na mzingo mdogo

Mfano
Kiwanja "A" (20m x 30m)
Eneo= 20m x 30m = 600m²
Mzingo = (20m + 30m)×2 = 100m

Kiwanja "B" (40m x 15m)
Eneo = 40m x 15m = 600m²
Mzingo = (40m + 15m)×2 = 110m

Kiwanja "A" kina mzingo wa mita 100, wakati kiwanja "B" kina mzingo wa mita 110 kwa hivyo kama ungekuta hivi viwanja ndio vimebaki huko site, basi kiwanja kizuri ni kiwanja "A", pia hata ukijenga uzio (fence), kiwanja "A" kitatumia tofali chache kulinganisha na kiwanja "B" lisha ya vyote kuwa na SQM zinazofanana

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Duh sasa sie wwnyw viwanja virefu vya 40m na upa a wa 20. Inakuwaje ujenzi hapo?
 
Katika vyumba vya kulala, imezoeleka kwamba switch za kuwashia taa huwa zinakuwa ndani ya chumba

Sasa wengine huwa wanafanya hivi hivi hata kwenye vyoo kitu ambacho sio sahihi. Switch za kuwashia taa za vyooni zinabidi ziwe kwa nje pembeni kidogo ya mlango ili mtu awe anawasha taa kabla hajaingia, na kama ni kuzima basi azime taa baada ya kutoka chooni

Switch za kuwashia taa za vyooni zikikaa ndani ya choo, kuna uwezekano pia maji yakaingia kwenye hizo switch na ikasababisha madhara

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Kha! Maji yaingie kwenye switch tena huo uogaji gani jamni🤣🤣🤣
 
Naombeni ushauri kesho naenda kukutana na fundi ili anipigie gharama za kuanza msingi kwanza

Je kuna ulazima wa kuwa na vyoo viwili vya ndani kimoja master na kimoja cha public, nyumba ya vyumba viwili tu

Au nikiweka choo kimoja tu hicho cha public itakuwa good

Kibaraza cha jikoni hicho kina umuhimu wa kukaa hapo au nikiondoe

Na naomba mnisaidie kwenye upande wa ukubwa sebule inakuwa na ukubwa gani standard urefu na upanda(futi na meter)

Chumba cha master kinakuwa na ukubwa gani pia,chumba cha kawaida kinakuwa na ukubwa gani, choo kinakuwa na ukubwa gani na jiko la kawaida linakuwa na ukubwa gani.

Sitaki nyumba kubwa inisumbue kwenye kuimalizia, nataka iliyotulia standard isinitese kwenye vifaa vinavyoanzia na english huko
Haka mzeya msingi na boma umetumia milioni ngapi?
 
Tofali za msingi huwa tunazilaza, kwa hivyo uso wa juu wa msingi unakuwa na upana wa 230mm, nyuso za tofali za boma zinakuwa na upana wa 125mm (nchi 5) au 150mm (nchi 6)

Ukisimamisha tofali kati kati, juu ya ukuta wa msingi maana yake nyuso za kuta za msingi bado zitakuwa zinaonekana kushoto na kulia mwa kuta za boma ( itakuwa ni (230mm-150mm)÷2=40mm kama utatumia tofali za nchi 6 katika boma au 52.5mm kama utatumia tofali za nchi 5)

Hizo 40mm au 52.5mm ya kuta za msingi zinazoonekana ndio zinatumika kama level (timanzi) ya floor wakati unamwaga zege la floor katika vyumba
Je, ikiwa utalaza tofali za boma, zile za msingi zinatakiwa ziwekwe vipi?.
 
Back
Top Bottom