Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Mkuu hivi mkikadiria bati kwenye makadirio hua inakua exactly?
Huwa tunaongeza asilimia flani kama allowance

Kila fundi huwa ana namna yake ya kutumia material ndio maana fundi mmoja anaweza akakutajia bati 110 na mwingine akakutajia bati 115 na wote hao ukakuta bati zote zikaisha (wakatofautiana kwenye mabaki (wastage), mwingine akawa na wastage chache na mwingine akawa na wastage nyingi)

Hii sio kwenye bati tu, ni katika hatua zote za ujenzi (ni muhimu kuwe na allowance).
 
Katika ujenzi kuna makosa madogo madogo huwa yanafanyika ambayo huwezi ukayanotice kwa haraka, sasa ili hayo makosa yasiendelee kuzaa makosa mengine katika hatua zingine zinazofuata ni vyema katika kila hatua ya ujenzi ukawa unafuata procedure zote bila kutumia/kutegemea hatua iliyotangulia kama reference

Mfano katika ujenzi wa kuta, ule usawa wa juu kabisa wa boma unaweza usiwe level moja kwa nyumba nzima (kuna sehemu zinaweza zikawa zinapishana kidogo), sasa mfano ukisema utumie usawa wa juu wa boma kama reference katika kupima height ya dari, dari pia halitakuwa level (litainama) ndio maana zoezi la kupigilia mbao za dari, lazima pipe level itumike ili kuhakikisha dari linakuwa na usawa mmoja katika nyumba nzima hata kama kulikuwa na makosa katika ujenzi wa kuta. Mifano ni mingi lakini kwa leo, huo mfano mmoja unatosha

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Mkuu kwani haiwezekani kumsimamia fundi atumie pipe level kwenye top level pale ili kuweka height sawa kwa nyumba nzima. Kuliko tena kwenda kuitafutia kwenye upigaji wa dari.
 
Wakitumia pipe level katika kozi ya mwisho, napo kuna changamoto inaweza kutokea...wanaweza wakakuta kuta zinatofautiana kwa kiasi kikubwa hivyo italazimisha sehemu zingine wajaze udongo mwingi ili kuinua kuta ziende juu zaidi, na sehemu zingine waweke udongo kidogo sana ili kushusha kuta ziwe chini

Kama wakitumia pipe level kozi mbili kabla ya kufika mwisho, inasaidia kugawanya huo utofauti uliotokea na kuubalance udongo katika kozi zote mbili hivyo udongo unakuwa haurundikwi sehemu moja pekee (katika kozi moja)

Kuna level flani ya kuta ikishafika (mfano kozi ya 6 au ya 7), pipe level inatumika kutafuta level nyumba nzima na kutokea hapo kwenda huko juu, kozi zote zinakuwa zinatumia hiyo level iliyotafutwa kama reference japo pia katika zoezi la kufunga mkanda ni vizuri pia kuhakikisha level kama iko sawa
 
naona wengi wanatafuta level kwenye mkanda ili madirisha yawe sawa wakipigilia zile mbao za button za madirisha
 
Wakitumia pipe level katika kozi ya mwisho, napo kuna changamoto inaweza kutokea...wanaweza wakakuta kuta zinatofautiana kwa kiasi kikubwa hivyo italazimisha sehemu zingine wajaze udongo mwingi ili kuinua kuta ziende juu zaidi, na sehemu zingine waweke udongo kidogo sana ili kushusha kuta ziwe chini

Kama wakitumia pipe level kozi mbili kabla ya kufika mwisho, inasaidia kugawanya huo utofauti uliotokea na kuubalance udongo katika kozi zote mbili hivyo udongo unakuwa haurundikwi sehemu moja pekee (katika kozi moja)

Kuna level flani ya kuta ikishafika (mfano kozi ya 6 au ya 7), pipe level inatumika kutafuta level nyumba nzima na kutokea hapo kwenda huko juu, kozi zote zinakuwa zinatumia hiyo level iliyotafutwa kama reference japo pia katika zoezi la kufunga mkanda ni vizuri pia kuhakikisha level kama iko sawa
Mtaalam. Hivi mbao ya msedelea unaweza tumia kjtengeneza milango ya ndani na isiliwe na mchwa au kupinda?
 
Aise ndg yangu huu mti kwangu ni mgeni, ndio leo nausikia kwako kwa hivyo sina experience nao.

Labda wenye uzoefu na mambo ya mbao waje kutupatia elimu zaidi
 
Katika ujenzi wa ghorofa, nondo huwa zina mpangilio wake maalum kwa hivyo kama fundi asipozingatia huo mpangilio, bado jengo lako litakuwa katika risk maana unaweza ukaweka nondo mahali ambapo hapahitajiki kuwekwa nondo (hii sio shida, utakuwa umepata hasara tu), au ukaacha kuweka nondo mahali ambapo nondo inabidi ziwekwe (hapa ndio changamoto ilipo sasa)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kuna nyumba moja ni mpya kabisa (nyumba za kuficha paa), wenyewe wamehamia mwaka huu huu lakini jana nimepita nimekuta watu wapo juu ya paa na mtungi wao wa gesi (bati zimeanza kuvuja kwenye maungio ya bati na kuta).

Wakati huo huo kuna nyumba nyingine mwaka jana ilibadilishwa mfumo wa paa (katoa paa la kuonekana, akaweka paa la kuficha). Nae pia anajuta kufanya huo uamuzi, anasema ni bora angeacha paa lake lile lile mana mvua ikianza, wanaanza kuhamisha vitu ndani visiloe
 
Ila nadhan wapauaji ndio tatizo. Kuna wengine yako safi tu. Kwenye maungio wanapiga FLASH COVER saafi kabisa
 
Kuna nyumba moja ni mpya kabisa (nyumba za kuficha paa), wenyewe wamehamia mwaka huu huu lakini jana nimepita nimekuta watu wapo juu ya paa na mtungi wao wa gesi (bati zimeanza kuvuja kwenye maungio ya bati na kuta).

Wakati huo huo kuna nyumba nyingine mwaka jana ilibadilishwa mfumo wa paa (katoa paa la kuonekana, akaweka paa la kuficha). Nae pia anajuta kufanya huo uamuzi, anasema ni bora angeacha paa lake lile lile mana mvua ikianza, wanaanza kuhamisha vitu ndani visiloe
what a solution
 
Hivi kuna tofauti gani katika boma fundi anapojenga tofari 10 akafatia lenta akamalizia na 3 za mwisho

Na anayejenga tofari 11 akafatia lenta akamalizia 3 za mwisho

Na pia inawezekana fundi akajenga 10 akaweka lenta juu akamalizia 4 na sio tatu na ipo vixuri au kiufundi sio sahihi
 
Wakati mwingine sio lazima sana kuchukua vifaa vyote vya ujenzi vikiwa ktk hali yake ya uzima mfano unapoenda kununua tiles, unanunua box za tiles ambazo ni nzima na ukifika site tiles zingine unazikata ili upate vipande vya kujazia na wakati huo huo pale hardware uliponunulia hizo tiles kuna box za tiles ambazo baadhi ya vipande vimekatika na muuzaji anauza kwa bei ya hasara hivyo kama ungechanganya box nzima na zile zilizokatika ungeokoa kiasi flani cha pesa

Hii pia unaweza ukaapply kwenye gympsum board ktk uwekaji wa dari, tofali n.k kwa lengo la lengo kupunguza gharama

Kabla ya kufanya uamuzi inabidi ufanye mahesabu ili upate makisio kwamba nyumba yako itahitaji vitu vizima vingapi, ili uweze kujua sehemu iliyobaki itahitaji kiasi gani cha material ambazo sio nzima (hapa simaanishi ubovu, namaanisha utimilifu)
Bonge Moja la Uzi .....

Mtoa Uzi ....u have my respect [emoji91][emoji91]
 
Hivi kuna tofauti gani katika boma fundi anapojenga tofari 10 akafatia lenta akamalizia na 3 za mwisho

Na anayejenga tofari 11 akafatia lenta akamalizia 3 za mwisho

Na pia inawezekana fundi akajenga 10 akaweka lenta juu akamalizia 4 na sio tatu na ipo vixuri au kiufundi sio sahihi
1. Idadi ya kozi kutoka mkanda wa chini mpaka mkanda wa juu inategemea na mtu anataka aweke madirisha ya urefu gani.

Kama utaweka kozi 10, ukuta wako utakuwa na urefu wa around futi 9. Wengi wanaojenga kozi 10 kati ya mkanda na mkanda, madirisha yao huwa ni ya urefu wa futi 5 (kozi 4 kwa kozi 6) au futi 6 (kozi 3 kwa kozi 7).

Sasa wengine huwa wanaweka dirisha za urefu wa futi 7 au zaidi, kwa hivyo hawa wanalazimika kuongeza idadi ya kozi

2. Kozi 3 juu zinatosha kama slope ya bati ni ya kawaida ila sasa kama mtu bati lake lina slope kali na anataka bati liwe na overhang kubwa, hapo itabidi aongeze kozi zaidi kwa maana kadri overhang/slope inavyoongezeka, nafasi ya kuta inazidi kufichwa na paa
 
Kuna nyumba moja ni mpya kabisa (nyumba za kuficha paa), wenyewe wamehamia mwaka huu huu lakini jana nimepita nimekuta watu wapo juu ya paa na mtungi wao wa gesi (bati zimeanza kuvuja kwenye maungio ya bati na kuta).

Wakati huo huo kuna nyumba nyingine mwaka jana ilibadilishwa mfumo wa paa (katoa paa la kuonekana, akaweka paa la kuficha). Nae pia anajuta kufanya huo uamuzi, anasema ni bora angeacha paa lake lile lile mana mvua ikianza, wanaanza kuhamisha vitu ndani visiloe
Hata mimi naona kabisa naelekea kuvunja paa la kuficha nipaue upya kawaida. Hata sielewi nilifikaje huko
 
Hawa ndio mafundi wa chap chap, huwa wanawaza kumaliza kazi tu ili wapate hela yao waondoke.

Picha yenyewe nimepiga kwa kuvizia, ukuta umeinama kiasi kwamba hata ukikaa mbali unauona kabisa kama umeinama

Fundi kupaua asipojiongeza, paa nalo litainama pia.
20250403_112943.jpg
 
Hawa ndio mafundi wa chap chap, huwa wanawaza kumaliza kazi tu ili wapate hela yao waondoke.

Picha yenyewe nimepiga kwa kuvizia, ukuta umeinama kiasi kwamba hata ukikaa mbali unauona kabisa kama umeinama

Fundi kupaua asipojiongeza, paa nalo litainama pia. View attachment 3292171
mkuu kongole sana kwa huu uzi I salute you, mm ni mtaalamu wa ujenzi ila sijui kila kitu with due respect nadiriki kusema uzi wako umekuwa shule tosha kwangu. ( huwa nakuja hapa kuongeza nyama nyama kwenye Ile knowledge ndogo ya ujenzi niliyonayo ). keep it up bro nikipata mteja wa ramani ntamrecommend kwako kuonyesha appreciation yangu kwako
 
Nashukuru sana kwa appreciation, tuko pamoja ndugu
 
Back
Top Bottom