Ramani, makadirio, Elimu na ushauri kuhusu Ujenzi

Wakati mwingine unaweza ukashindwa kuendelea mbele na ujenzi kwa sababu kuna watu uliwafanyisha kazi, lakini haki zao ukawadhulumu

Lakini pia Mungu anaweza akakuacha ukafanya ujenzi wako hivyo hivyo kwa dhulma dhulma, na baada ya nyumba kukamilika, hiyo nyumba isidumu hata miaka mitano ukaipoteza (kuungua, kukuingiza hasara katika matengenezo kila kukicha na mabalaa mengine) yote ni kwa sababu kuna watu wanalilia haki zao kwako na hutaki kuwalipa.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
daaah! Hapa sasa hapa ...
 
Kabisa, na nadhani bati ndio bidhaa ambayo inatengenezwa na kampuni nyingi kwa hapa kwetu kwa hivyo ushindani wake kwa hizi kampuni ambazo bado zinajitafuta ni mkubwa sana. Maafisa masoko wanaenda kutafutia wateja huko huko site
hivi hizi kampuni zinazojitafuta wanakuwaga na bati OG kwel?
 
Kwa kweli sina uhakika, maana ukipita mitaani unakutana na nyumba nyingi tu, ni mpya lakini bati zake tayari zimeshaanza kupauka na kuchakaa

Kinachofanya bati lidumu zaidi ni kiasi cha aluminium kilichotumika kutengenezea hilo bati (aluminium huwa haipati kutu). Sasa ni ngumu kuwa na bati zilizotengenezwa na madini ya aluminium tupu (ni gharama sana), kwa hivyo huwa wanachanganya na madini mengine mfano chuma ili kupunguza gharama za uzalishaji
 
mkuu, naomba msaada,kwa uzoefu wako, ukitoa kiwanda cha alafu, ni kiwanda gani Kinaweza kukaribiana kwa ubora na alafu?
 
sunbank vip
Kwakweli sifahamu ndg yangu, yote kwa yote kama unachukua hizi bati zingine basi nashauri uchukue gauge 28 in case kama bei ya gauge 28 ya hizo bati bado iko mbali na bei ya gauge 30 ya Alaf
 
Hechy Essy Naomba muongozo wa wataalam.
Kati ya tofali za udongo za kuchoma na hizi za block (cement+mchanga) ni zipi imara zaidi? Na endapo unajengea tofali za udongo za kuchoma ni vyema kutumia cement ama tope la udongo?
 
Kwakweli sifahamu ndg yangu, yote kwa yote kama unachukua hizi bati zingine basi nashauri uchukue gauge 28 in case kama bei ya gauge 28 ya hizo bati bado iko mbali na bei ya gauge 30 ya Alaf
so ni nora gauge 30 ya Alaf kuliko 28 za hawa wengine?
 
Nikisema ndio nitaeleweka vibaya, kiufupi gauge ni kipimo cha mark ya bati (unene wa bati) kwa hivyo gauge 28 ya bati la kampuni yoyote haiwezi ikawa sawa na bati la gauge 30 ya kampuni nyingine yoyote (kama standards za uzalishaji zitazingatiwa).

Hapo nimezungumzia gauge tu, sio masuala ya ubora na pia kama imeshindikana kabisa kupata bati za ALAF kutokana na bajeti, hakuna njia nyingine zaidi ya kuangalia bati za kampuni nyingine ambayo itaendana na bajeti iliyopo so katika kuangalia huo upande mwingine, tips kama hizi ni za kuzizingatia pia.
 
Ndugu Hechy Essy je kama nyumba ina muendelezo / itaendelea kuna ulazima wa kuacha matoleo au katika kuendeleza unaweza kuunganisha kuta kwa zege / nguzo za zege?
 
Sijawai ona bati Ya chenga chenga Migongo mipana kutoka ALAF sijui kwa nini
 
Ndugu Hechy Essy je kama nyumba ina muendelezo / itaendelea kuna ulazima wa kuacha matoleo au katika kuendeleza unaweza kuunganisha kuta kwa zege / nguzo za zege?
Njia zote zinatumika, aidha kuacha matoleo au kuunga kwa nguzo japo hii ya kuacha matoleo kidogo ujenzi wake huwa unasumbua maana tofali zake huwa zinachomekwa kwenye mapengo yaliyoachwa hivyo inakuwa ngumu hata kujaza udongo wa mortar katika joint za tofali na tofali.

Unaweza ukaacha matoleo ya step (ngazi) badala ya matoleo ya zigzaga lakini nayo itabidi ukuta utoke nje sana (mana hata ukienda kwa step ndogo ya sentimita 15, ukuta itabidi utoke nje mita 1.5 kama utajenga kozi 10 kutoka mkanda wa chini mpaka mkanda wa juu)
 
Kwahiyo njia ya zege ndo bora zaidi mkuu.
 
Ndio, nguzo ya zege haina compication nyingi lakini wakati wa kupiga plaster, hakikisha unaweka wire mesh kwenye hayo maungio kabla hujachapia udongo wa plaster vinginevyo baada ya muda utaona ufa unaanza kujitokeza kwenye maungio (zege na tofali ni vitu viwili tofauti, kwa hivyo ikitokea mabadiliko ya joto, kila kimoja kinatanuka/kusinyaa kwa namna yake)
 
Katika uwekaji wa balcony (iwe ni nyumba ya ghorofa au hata nyumba ya chini), pendelea kuweka balcony ambazo reli zake ni za kusimama kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Kila unachoweka katika nyumba, fikiria na usalama wa watoto pia
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
FB_IMG_1745133715776.jpg
 
Back
Top Bottom