Raisi Magufuli likatae pendekezo la kuwashughulikia mitume na lile la kujenga makanisa mpaka kwenye vituo vya usafiri wa Mwendokasi.

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Wataalamu wa mawazo na wanazuoni:

Inaelekea watu wengine sifa za msingi na Kuu za Mungu hawazijui. Inaelekea kana kwamba baadhi ya dini hazijachukua wala kutenga muda wa kutosha kusoma Falsafa kabla ya kuamua kusoma Teolojia. Ingalikuwa wahusika waliwekeza muda wa kutosha kusoma Falsafa ili kubainisha asili ya vitu vyote ikoje(uncreated Creator), basi watu wengine tusingaliweza kusikia mapendekezo ya ajabuajabu kadri ya mada hii.

Ni hivi, Mungu kwa asili yuko mahali pote(Omnipresent). Ninaposema kwamba yupo mahali pote, ina maana yupo ndani na nje ya Space. Mungu anapokuwa ndani na nje ya space maana yake anaona na anakuwa aware na kila jambo au hali inayotukia ndani ya space au nje ya space(Omniscience).Maana yake ni kwamba Mungu, haitaji kuambiwa na kiumbe chochote ili ndio aelewe kwamba jambo fulani linaendelea au lilitukia au litatukia.

Sifa nyingine ni kwamba Mungu anafahamu yote na kukumbuka yote yaliyotukia, toka alipofanya uumbaji wa vyote tunavyovifahamu na tusivyovifahamu. Anafahamu yote yanayotokea sasa ndani na nje ya space. Anafahamu kila jambo na kila hali itakayotokea kwa kila kiumbe kilicho hai na hata visivyo hai. Kwa ufupi, kwa Yeye Mungu kuwa Omnipresent na Omniscience ni kwamba yuko na Control ya kila jambo. Kwa lugha ya kisasa yuko TIMAMU.

Sifa nyingine kuu ya Mungu inayoendana na hizo mbili hapo juu,ni kwamba Mungu anao uwezo wa kwa kila jambo.Yeye yuko juu ya kila uweza. Mungu anaweza kila lisilowezekana au lililoshindikana kwa viumbe wengine. Kwa mantiki hiyo yeye ni UWEZA USIOWEZWA.

SASA katika hali ya kushangaza sana,kinyume na ukweli ambao nimeubainisha hapo juu, jana wamesikika watu wawili wakiweka mbele ya Raisi Magufuli, mambo ya ajabu sana. Mmoja ni wa dini ya Kiislamu, ambaye kwa nafasi yake ni mmoja wa Wakurugenzi wa BAKWATA, Makao Makuu. Na wa pili ni kutoka dini ya Kikristu,naye ni yule anayejiita “Askofu” Gwajima wa kikundi cha kidini cha “Ufufuo na Uzima”.

Watu hao wamesikika wakiwasilisha kwa Raisi Magufuli jana,katika kikao chake na Viongozi wa dini, mambo ambayo sio ya Kisera wala Kikatiba. Na wengine wamesikika wakiwasilisha mbele ya Raisi Magufuli ombi la yeye kushughulikia masuala ambayo ni ya Omnipresence, Omniscience na kadhalika. Kwa lugha nyingine walisahau kwamba Raisi Magufuli sio Mungu kwa sababu maombi waliyompatia mwenye uweza nayo ni Mungu pekee.

Ni hivi,Kiongozi mmoja wa Kiisalmu, kwa jina la Muhammed, kutokea BAKWATA,Makao Makuu, alitaka Raisi Magufuli aingilie kati na kumnyamazisha mhubiri mmoja wa Kiislamu anayejiita Nabii(Mtume) HAMZA. Kwa wale msiomfahamu huyu Nabii HAMZA, ni muislamu ambaye amekuwa akipingana na Fundisho la Kiislamu kudai Yesu Kristu hakufa msalabani bali Mungu alimuweka mtu mwingine pale msalabani na ndiye huyo aliyekufa na wala sio Yesu Kristu.

Kwa hiyo, pamoja na jamaa huyo kuhubiri mambo mengine positive juu ya Yesu, kinachowakera Waislamu hadi wafikie hatua ya kumchongea kwa Raisi Magufuli ni yeye kujiita “Mtume” au “Nabii”. Kwa uelewa wa kiislamu,wanaamini kwamba mtume wa mwisho ni Muhammad na wala siyo Yohana Mbatizaji kama Wakristu wanavyoamini,mtu ambaye hata Yesu alimwagia sifa za kutosha sana miongoni mwa Manabii.

Kiongozi mwingine ambaye alitoa wazo kwa Raisi lisilo la Kisera ni “Askofu Gwajima.” Yeye baada ya kusikia waislamu wanatoa ombi jingine lisilo la Kisera la kujenga Msikiti mwingine Uwanja wa Ndege wa Dar es salaam, naye akatoa ombi la kujenga Kanisa hapo hapo sawa na waislamu wanavyoomba.

Sasa kwa nini mjadala juu ya hoja hizi mbili: ya ujenzi wa makanisa na misikiti kila mahali na kuzuiwa watu wengine kujiita mitume?

Watu wengi sana wanaendelea kujadili mambo haya kilaini laini tu kama mambo ya kawaida sana. Na wengine wanaona kana kwamba Waisalamu wanaonewa kwa kuzuiliwa kujenga misikiti au Makanisa.Na akina Gwajima wanataka kututumbukiza katika fikra za kwamba kila waombalo waislamu nasi Wakristu au Vikundi vingine vya kiimani navyo vinapaswa kuomba sawia na waislamu. Sasa kwa nafasi ya leo, naomba tujadili hoja hizi mbili, nje ya Duara ya Mashaka.

1. Hoja ya misikiti na makanisa kwenye maeneo ya umma.

Ni hivi kwa uwezo wa Mungu ambao nimeubainisha hapo awali, Mungu ili atambue na kutuona kwamba tuko tunamuomba sio lazima tu tuwe kwenye chumba,compound au eneo fulani tu liitwalo Msikiti au Kanisa.

Mungu yuko popote pale.Yuko ndani na nje ya space.Yuko mioyoni mwetu. Kabla hatujamuomba yeye alishafahamu tulikusudia kumuomba nini kila mmoja wetu,na tena, kabla hata ya kuumbwa kwetu. Kwa hiyo,haitaji Mungu atuone ndani ya Misikiti au Kanisa ndio aweze kubaini sala na dua zetu kwake. Mungu wetu ni Mungu mwenye wingi wa MANTIKI, UFAHAMU NA AKILI.

Mungu wetu ni mwingi wa ufahamu;anafahamu ni wakati gani na mahali gani afanye mambo kwa ajili ya ustawi wetu. Kinyume chake hatuwezi kuwa na Mungu ambaye hawezi kututaka tujenge Misikiti na Makanisa kila mahali:kwenye vituo vya Mwendokasi,Sokoni, Baharini kwa wavuvi, Barabarani na katika njia za waenda kwa Miguu.Fikra za namna hii zimenipeleka kujiuliza yafuatayo:

  • Ni kwa nini watu kama viongozi wa dini, wanaochukuliwa kuwa na maono ya Kimungu washindwe kuelewa kwamba Raisi anahusika na mambo ya Kisera na Kikatiba, sio masuala kama haya ya kulilia kuzuiwa kujenga MIsikiti au Makanisa?
  • Hivi kama kuna mtu anaona amenyimwa haki ya Kikatiba kwa nini asitimkie Mahakamani kuomba haki hiyo?
  • Je,Viongozi wa dini kushindwa kuwa na uelewa wa kutosha juu kuwa wapi pasemwe lipi na wapi kusemwa lipi, sio kigezo cha kuthibitisha kwamba Mungu hajawapa maono yoyote bali wamejipachika tu hayo maono yao?

2. Hoja ya kuzuiwa watu wengine kujiita mitume

Kikatiba ni kwamba kwa nchi yetu suala la kuabudu ni suala la uchaguzi. Kila mtu yuko huru kuchagua amuabudu nani na aamini nini? Mwenye jukumu la kwenda kuamua nani alikuwa sahihi ni Mungu mwenyewe. Hapa duniani sio Polisi,Jeshi na wala IKULU yenye jukumu la kuchagulia watu wajiiteje kiimani na wala wafundishe nini.

Wakati baadhi ya waislamu wanalalamika juu ya “Nabii HAMZA” wanasahau kwamba hata Muhammad naye utume wake aliutwaa katika mazingira kama hayo ya Nabii HAMZA. Historia iko wazi kwamba hakuna Nabii ambaye hakuwahi kuwa endorsed na Mungu. Kila Nabii katika Historia ya Ulimwengu, alipotumwa na Mungu ilikuwa lazima Mungu amthibitishe kupitia kwa Mitume wengine wanaokuwa wamemtangulia au Mungu vile vile alifanya hivyo kwa miujiza kabisa.Maana yake kwamba Mungu alimjalia mtu huyo uwezo wa kufanya miujiza.

Mazingira kama haya hayapo na hayajawahi kudhihirika kwa Muhammad. Sasa kwa hali hiyo,wale wanaoomba “NABII HAMZA” anyamazishwe kutumia neno “Nabii” nao:
  • Wanaelewa kuwa hata Muhammad kuna dini iliyomtangulia inamuona kama hana vigezo vya kujiita Mtume au Nabii,achilia kuwa nabii wa mwisho?
  • Masuala ya utume na Ukuhani ni masuala ya Kimungu. Mungu ndiye ana Authority ya kumtangaza fulani ni HALALI na mwingine ni BATILI. Je,ni kwa nini mambo kama hayo anapelekewa Raisi Magufuli?
  • Wanao-appeal kwa Raisi Magufuli masuala ambayo hana uwezo nao wameambiwa na Mungu kwamba Magufuli kwa sasa anakaimu nafasi ya Mungu?
  • Je,wanao-appeal kwa Raisi Magufuli kwamba “Nabii HAMZA” azuiliwe kujiita Mtume, ikitokea Wayahudi na Wakristu walioutangulia Uislamu, nao wakaenda kwa Raisi Magufuli kulalamika ili waislamu wazuiwe kumuita Muhammad ni mtume na tena mtume wa Mwisho,watakubali au nao watasikilizwa?
  • Je,wale wanaotaka “NABII HAMZA” azuiliwe utume wake,ikitokea akazuiliwa kuitwa hivyo hapa Tanzania lakini akaendelea kuitwa hivyo sehemu sehemu zingine duniani,itakuwaje? Je,Wataenda kushitaki Umoja wa Mataifa?
BASI,kwa maswali na hoja zingine kutoka kwenu karibuni kwa mjadala.
 
This is too deep. Nimesikia wengine wakitaka nao wamepewe nafasi ya kuomba wakati wa kumuapisha Rais na pia wapewe fursa sawa kurusha vipindi vya dini kwenye idhaa za taifa. Tunakoenda itabidi tujitathimini namna ya ku handle mambo ya dini. Pengine Kagame kwa udogo wa nchi yake aliona mbali akachukua hatua kudhibiti mifumko holela ya dini na madhehebu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikia wengine wakitaka nao wamepewe nafasi ya kuomba wakati wa kumuapisha Rais na pia wapewe fursa sawa kurusha vipindi vya dini kwenye idhaa za taifa. Tunakoenda itabidi tujitathimini namna ya ku handle mambo ya dini.


Ni kwani sababu tumegeuza Falsafa ya dini kuwa mashindano au Mbio za Marathoni. Wengine wanafikiria Makanisa mengine yamekuwa kutokana na kubebwa.
 

"Katika sheria ya uislamu hakuna Nabii wala mtume,baada ya Mtume Muhammad,tatizo sio yeye kujiita nabii,tatizo ni huo unabii wake kuuegemeza katika uislamu,wakati uislamu,umeshaweka sheria zake,za kuwa hakuna nabii ,baada ya Mtume Muhammad S A W."

Kama hakuna sheria hiyo na mtu amejiita hivyo ni mtume automatikali anakuwa sio Muislamu Wa aina yenu. Kama ndivyo ni kwa nini mnataka azuiwe kujiitikadi kama mtume? Ninyi inawauma nini au inawapunguzia nini? Mbona mumejawa wivu hivyo kama ule Wa "kike"?

Je,dini zilizomtangulia zingemuwekea roho mbaya,unafikiria Muhammad angalifika wapi? Inakuwaje Muhammad yeye alipewa nafasi ya kuwatukana Mayahudi na Wakristu lakini sasa anageuka na kuwapeni maelekezo muwazuieni wenzenu?
 

"Katika sheria ya uislamu hakuna Nabii wala mtume,baada ya Mtume Muhammad,tatizo sio yeye kujiita nabii,tatizo ni huo unabii wake kuuegemeza katika uislamu,wakati uislamu,umeshaweka sheria zake,za kuwa hakuna nabii ,baada ya Mtume Muhammad S A W."

Kikwajuni One Kama hakuna sharia hiyo na mtu amejiita hivyo ni mtume automatikali anakuwa sio Muislamu Wa aina yenu. Kama ndivyo ni kwa nini mnataka azuiwe kujiitikadi kama mtume? Ninyi inawauma nini au inawapunguzia nini? Mbona mumejawa wivu hivyo kama ule Wa "kike"? Je,dini zilizomtangulia zingemuwekea roho mbaya,unafikiria Muhammad angalifika wapi? Inakuwaje Muhammad yeye alipewa nafasi ya kuwatukana Mayahudi na Wakristu lakini sasa anageuka na kuwapeni maelekezo muwazuieni wenzenu?
 
Hoja Yako Kuhusu Msikiti Na Makanisa Umetembea Vyema, Shida Iko Kwenye Kudhibiti Vikundi Vya Dini, Lazima Serikali Iingilie Kati , Lakini Sio Kwa Mkitadha Wa Jana, Vinginevyo Tutakuwa Na Taifa La Hovyo Sana, Eti Kwa Sababu Baa Zinaongezeka ,
 
Vyema, Shida Iko Kwenye Kudhibiti Vikundi Vya Dini,

Hakuna cha mtu kudhibitiwa. Acheni watu wahubiri kadri wanavyopata maono. Mungu ndiye atachambua kati ya aliowapa maono na waliojipa maono. Kama Watu wangeweka vizingiti ina maana Leo Muhammad isingekuwa sio habari kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom