Ukweli kuhusu dini

mwidaddy

Senior Member
Feb 19, 2022
131
170
Utata wa udini unatokea sana kwa sababu ya baadhi ya binadamu wanaoujua ukweli kujaribu kuwapotosha wengine kwaajili ya kulinda maslahi yao binafsi bila kuzingatia athari kwa watu wengine.

Tangu enzi na enzi Mungu amekuwa na utaratibu wa kuwatumia mitume wake ili kuwapatia mafunzo watu wake wasipotoke, kuanzia nabii Adam hadi kufikia kina Iburahim, Mussa, Nuhu hadi Yesu Kristo ilikuwa ni mpango wa Mungu kwa watu wake katika usahihi wa maisha ya mwanadamu, kizazi hadi kizazi taifa kwa taifa limepewa mwongozo kupitia mitume na manabii hao na mwishowe Yesu kristo amekuja kuleta agano jipya lililobeba mafunzo mapya katika maisha mapya.

Kutokana na watu kuwa na Imani haba zaidi na kutoamini mafunzo ya Yesu kristo kwa wakati huo basi Yesu akanena Yohana 6:5-20 kuhusu habari za msaidizi wake ambaye atakuja duniani kuleta habari zinazohusu ukweli, na haki na ukombozi huku akimtukuza Mungu na Yesu pia kwa kuyatumia maneno ya Yesu katika kutoa mafunzo yake pia hatokifahamu anachokisema ispokuwa Mungu atanena kupitia yeye, kwa uthibitisho huu na maneno haya ya Yesu kristo mwenyewe inamaanisha alitabiri juu ya ujio wa mtume wa mwisho na wa kweli ambae kiukweli ni Muhammad s.a.w.

Muhammad hakujua anachokisema ila alizungumza maneno yake ambayo yameiunda Quran hii inamaanisha Mungu alimtumia yeye kuishusha Quran.

Quran ndiyo kitabu kilichokusanya vitabu vyote ikiwemo Tourati, Injili, na vitabu vingine Vilivyomo katika biblia na Quran yenyewe. Pia Quran inamtambua Yesu messiah kama mtume wa mwenyezi Mungu na matendo yake na mafunzo yake yanatukuzwa pia ndani yake.

Kilichopo ni baadhi ya watu wa mwanzoni kuzijua hizi dini wameamua kupotosha wengine ili kulinda maslahi yao ikiwemo Warumi na Wayahudi walioanzisha makanisa yao mapema kupitia dini ya kikristo ambapo walilenga kuitumia dini ili kutawala sehemu kubwa ya dunia ndy sababu hadi sasa wanaweza kukusanya pesa duniani kote kupitia makanisa yao na kuzipeleka Vatican Italy kwaajili ya kuendesha shughuli na hawaingiliwi na serikali yeyote ikiwemo hata ya nchini kwao.

Viongozi wakubwa walioisoma biblia vyema wanaujua ukweli na ndy maana wanajua namna ya kupindisha agizo la Mungu kwaajili ya manufaa yao.

Ningewaomba waumini wote wa kikristo tusome biblia vyema hasa yale maeneo ambayo hayazungumziwi Sana kama vile kitabu cha Yohana ukweli upo wazi na kuhusu dini, hamna zaidi ya dini moja tu iliyoanzishwa na manabii wa mwanzo hadi kufikia kwa Yesu na Muhammad akamalizia kuitimiza dini hiyo, kwa fact hakuna ukiristo wala dini nyingine dini ni ile Muhammad aliyoitimiza kutoka mikononi mwa messiah.

Tuamue wenyewe kuchanganywa na wapotishaji au tusome tupate maarifa zaidi yatakayotusaidia kuufahamu ukweli wenyewe.

Tusiangamie kwa kukosa maarifa.
 
Mungu, Dini 👈 hivi vyote ni nadharia, Hadithi za kutungwa Tu na watu, ili kuwa control mindset
 
Back
Top Bottom