Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Umemuuliza swali zuri sana.

Tusubiri ifikapo 2020 tuone kama kura yake moja na ya mama Jesca ndizo zitakazomrudisha Ikulu!

Atapata,maana hata JK alisema haihitaji KURA zetu na akashinda.Hahhahahahahha
 
Sijasema kuwa yote anayoyafanya JPM kuwa ni mabaya, la hasha.

Yapo mambo anayoyafanya ambayo ni mazuri kama vile kuwadhibiti watumishi wa Umma ambao walikuwa wakifanya kazi kwa mazoea.....

Hata hivyo yeye kama Rais wa nchi ni lazima aongoze nchi kwa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama, kwa kuwa aliapa kuitii na kuilinda Katiba yetu kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa hili.

Kwa mfumo anaotumia wa kuyageuza matamko yake ya kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa sheria, hilo ni jambo la hatari ambalo linaweza kuja kulitumbukiza katika hatari Taifa letu.
Ukifikirià Chakula cha Leo,yaani lunch and dinner Magufuli is doing very good,but ukifikiria kesho na kesho kutwa,he is going nothing zaidi ya kufikiria tu 2020 tena akitumia siasa ñyepesi sana
 
Watu mnamsifia sana Kenyatta lakini mkumbuke na haya, mwenyekiti as tume ya uchaguzi Kenya aliuawa na serikali baada ya yeye kusema hakuna anayeweza kuingia kwenye system isipokuwa yeye Tu kwa kutumia finger print zake,
Uhuru tayari kashawapiga mkwara majaji kuhusu kesi yoyote itakayoletwa na upinzani dhidi yake.
Uhuru kajilimbikizia Mali na mashamba kama sumaye.
Na kama yeye anademokrasia ya UKWELI si aruhusu wapinzani waangalie matokeo kwenye hiyo system ya IEBC ili wajiridhishe.


Shida wewe unakariri sasa matokeo yameangaliwa je kama finger zimeoza? Amejilimbikia mashamba kama SUMAYE? unachukia bila sababu........... mashamba ya MKAPA hamuyaoni mpk vitalu hapana mnona mashamba ya mahindi huli kilosa?
 
Ukifikirià Chakula cha Leo,yaani lunch and dinner Magufuli is doing very good,but ukifikiria kesho na kesho kutwa,he is going nothing zaidi ya kufikiria tu 2020 tena akitumia siasa ñyepesi sana


Na mbaya zaidi hatakaa aamini ndio atajua ballot zitaongea mshenzi kabisa i real hate this man
 
Shida wewe unakariri sasa matokeo yameangaliwa je kama finger zimeoza? Amejilimbikia mashamba kama SUMAYE? unachukia bila sababu........... mashamba ya MKAPA hamuyaoni mpk vitalu hapana mnona mashamba ya mahindi huli kilosa?

Password yake imetumikaje?
 
Kama tunataka demokrasia ya kweli basi hatuna budi kujifunza kutoka America, tuachaneni na hizi taka taka za Kenya ,watu wengi wanaifahamu Kenya itakuwa ni vigumu sana kuwabadili mawazo, Obama for me is the champions of democracy in the world at the moment, ni vizuri tukamwambia Magufuli ajaribu kupitia hotuba zake kuna kitu atajifunza, Obama kitu alichokuwa akiongea na kutenda vinawiana, hata juzi ambapo kulikuwa na maandamano mtu mmoja akapoteza maisha na wengine kujeruhiwa at Charlottesville, Obama kashusha bonge la message ,ule ujumbe ni wakibinadamu, hata ukiisoma unajua kweli Obama ni kiongozi, leo hii mimi ukiniambia eti Magufuli should learn from Uhuru,atajifunza nini? ajifunze matakataka atuletee nchini maana yake ni kuizika demokarasia na kuanza kuchapana sisi kwa sisi. Hebu tubadilikeni.
kwa sababu yà ukweli kuwa kenya na wakenyà wanatuzidi katika mambo mengi basi tuna inferiority nào.Post yako is a result of that
 
Uoga wako ndio umaskini wako.Kwani unafikiri Kenya imefikia hapo kwa uoga au unadhani walizaliwa wakiwa na katiba nzuri?au Maendeleo ya Dunia yamefikishwa hapa na watu waoga.Ukiwa mwoga hutaweza kujifunza hata kuendesha Baiskeli sembuse kurusha ndege.Majasiri ndio wamefanya mpaka watu wakafika Mwezini.
Mimi nakuhakikishia kwamba watu wameridhika na jinsi wanavyotawaliwa.


Naungana na wewe kabisa dereva wa Kenya huwewzi mlinganisha na wa Tanzania anajiamini mno na anasimamia haki yake huku mtu anakuambia acha tuu nani kasema?
 
Ndugu yangu kosa pia ni la CCM !! Huwezi mchukua mtu ambayo huko nyuma hakuwahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ktk chama na kumpandisha ghafla, na kumpa vyeo vyote bila kuwa na udhibiti. Huyu bwana angebaki kuwa Rais huku chama kikimuweka sawa kwa muda. Baadaye ndiyo angepewa uenyekiti. Lakini ccm kwa kutaka waendelee kubaki salama wanakimbilia kumpa uenyekiti ili kiendelee kuwa chama dola.

Uhuru ameanza mbali alijaribu na kuanzia upinzani na alianguka mwanzoni. Kesi za the Hague imemfanya kufanya alliance ya nguvu na Ruto (kalenjin) kuukwaa u Rais. Hivyo anajua thamani ya kuwaheshimu wananchi!! Huyu yule mmachinga alidictate mkutano mzima na kumweka hapo hawezi kujua thamani ya kura moja ya mwananchi

Cairo's


Cairo thanks a lot aisee kama kuongea umesema kitu kabisa..................... huyu wetu ni shida hana ethincs hata za kuiongoza familia yake........... ndio aje kwa wananchi? mtu hana lugha tamshi la maana kinywani? Eti kama mshahara hautoshi nenda mkalime mtalima wote? kweli huyu mtu kwangu bado kabisa
 
Mtu jasiri haogopi mtu wa watu husikiliza hisia za watu yumkini akapata jambo moja jema katikati ya mambo mengi ya hovyo. Mtu mwoga huwa daima hajiamini na wala hawezi ruhusu mwinyine kusema lolote labda awe anamsifia

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kweli mkuu,ukisikiliza utàsikia Yale uñayoyajua na usiyoyajua hivyo utapata nafasi ya kujifunza,but mkuu wetu ama hajui ukweli huu au anàkosa listening skills
 
Nakubaliana nawe Mkuu ya kwamba ni vigumu kwa nchi za kiafrika kufikia kiwango cha demokrasia iliyofikiwa na mataifa makubwa ya magharibi for example USA.

Hata hivyo kama ilivyo kwenye FIFA rankings, Tanzania tunatrail behind Kenya kwa namna walivyoipanua demokrasia yao.

Kumbuka hapa nchini Mkuu wa nchi akitamka hadharani kuwa amepiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020, huku akijua kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inaeleza wazi kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vinatakiwa kufanya shughuli zao vikiwa huru.....

Ndiyo maana tukifanya comparison ya Uhuru Kenyatta kusema anawaruhusu wapinzani wanaotaka kuandamana kupinga matokeo yaliyompa Urais yeye na akawaelekeza Polisi kuwa wajibu wao siyo kuzuia maandamano hayo Bali kuyalinda ili yafanyike kwa amani......

Sasa compare na hapa kwetu walipokuwa wanapanga kuandamana katika yale maandamano waliyoyapa jina la UKUTA.....

Unakumbuka nini kilitokea?

Ni Mkulu kupiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi na kwa Mara ta kwanza nchini kwetu tokea baada ya vita ya Kagera miaka ile ya 70, tuliwashudia maaskari wetu wakifanya mazoeslzi yao ya kivita huku uraiani huku kila mtu akishuhidia .....

Kitendo cha vikosi vya Ulinzi na Usalama kufanya mazoezi yao ya kivita uraiani yalikuwa yana lengo la kuwatisha wananchi wasifanye maandamano yake ambayo ni haki yao ya kikatiba kuyafanya.....

Sikubaliani na Jinsi Magufuli anavyo handle democracy nchini, lakini pia sio vyema tukasema tuige mfano wa nchi ambayo imeshindwa kidemocracy, mfano Kenya watu wameandamana wanapigwa na polisi ,amri jeshi mkuu katoa order ya shoot and kill, Haikuruhusiwa kipindi cha uchaguzi Kenya kutuma taarifa au photos ambazo sio sahihi kabla hazijathibitshwa ( mis-iformations) hii ni yale yale ya cyber crimes ambazo serikali ya Tz ilipitisha wakati ule, mwandishi wa habari NTV kawekwa ndani katika zongo hizi hizi za uchaguzi, IEBC kufanya kazi za chama kimoja wabunge wa upinzani majimboni wakiuliza kura za raisi vipi ,wanaambiwa hili halikuhusu ,je vitendo hivi ni demokrasia? au demokrasia ni kwenda kwenye tv kuongea vitu tofauti na amri unayotoa kwa upande mwingine? ndio maana nikasema tuachane ni hizi taka taka za Kenya maana dunia inajua pale hakuna demokrasia ,kwanini tujifunze vitu ambayo tayari tunavifanya Tanzania?.
 
Siasa za Kenya ni tofauti na Tanzania.............!

Tofauti iliyopo kati ya siasa za Kenya na Tanzo ni kwasababu ya Viongozi wapumbavu wa CCM walioamua kwa Maksudi kusigina Katiba na kupindisha sheria ili waendelee kuitawala Tanzania kama vile ni mali yao. Nitafafanua. Baada ya machafuko huko Kenya mwaka 2007 Wakenya waliamua kuunda Katiba mpya ambayo ndiyo inaongoza nchi kwa sasa. Chini ya Katiba hiyo mpya wamefanikiwa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka(IEBC)ambayo ndiyo imesimamia Uchaguzi wa Kenya kwa Uhuru na Haki.
  1. Tanzania kwa ujinga wa Viongozi wa CCM wamekataa Katiba mpya kwa vile Tanzania wanaichukulia kama ni mali yao. Hawataki kuunda Katiba mpya wala Tume Huru ya Uchaguzi kwa vile wanaona vitu hivo ni tishio(threat) kwao na hatari ya kupoteza madaraka.
  2. Lakini pia CCM hawahawa hata Katiba iliyopo wanaipindisha ili kuendelea kujikita Ikulu. Rais JPM amezuia Mikutano na Maandamano kwa vlle anaona Upinzani wakiruhusiwa kuandamana watakosoa na ataonekana Rais dhaifu!!
  3. Lakini pia Rais JPM amekataa kurejesha mchalato wa kupata Katiba mpya kwasababu hizo hizo za hofu ya kung'olewa madarakani na Wapinzani pindi akionekana ana boronga. Kwa hofu hiyo sasa kaamua kuchukua upande wa Kidikteta kwa kuzuia kila kitu cha Upinzani kisionekane, kusikika wala kuzungumzwa.
  4. Tumeshuhudia Kuzuiliwa kwa Bunge Mubashara, kuzuia Maandamano na Mikutano ya Upinzani, Kuwakamata na Kuwafunga jela au mahabusu Wabunge wa Upinzani(kwa masaa 24/48) na Kuwanyamazisha au Kuwafukuza Wabunge wa upinzani toka Bungen kwa mwaka mzima au zaidi.
  5. Zote hizi ni mbinu chafu za Serikali ya Magufuli kinya Wapinzani ili abakia kusikika yeye tu kila . Huu ndiyo upuuzi ambao umma mkubwa wa Watz hautakubaliano nao.
Baba wa Taifa Mwl . Nyerere (Mungu amrehemu) alifika mahali akasema kama watu wataamua kumbeba Kiongozi yoyote wa kisiasa/upinzani na kumzungusha nchi nzima kwa Maandamano acha wafanye hivo. Kuzuia ni kutaka kuwapa WA[INZANI UMAARUFU usio wa lazima!!!Lakini maskini JPM hataki kusikia Ushauri huu yeye ameamua kupambana na wapinzani hadi mwisho wa Utawala wake na hajui kuwa anazidi kuharibu!!!
 
Ulishawahi kusikia Kemya wamefanya siasa baada ya uchaguzi? Kama jibu ni ndio, basi una haki ya kueleza zaidi ili kumtofautisha JPM na UK


Kama hujui kitu kaa kimya kabisa................... Odinga hajawahi kaa kimya ndio wakaja na NASA kaa mbali kabisa lazima siasa ziendeleee
 
Nilipenda Uhuru zaidi alisema niliwahi kugombea urais nilishindwa lakini nilienda nikasubiri but now nimeshinda...............

Tena mnafanya kosa sana kumfananisha UHURU na Magufuli ( Magu-Fool) maana ni shida hana ethics wala hajui uongozi ni nini yeye ni mnyapara kabisa hatakaa awe kiongozi
Wale wapambe wake wakikusikia wanaweza wakakuita mchochezi na wakashinikiza ukapimwe mkojo!
 
Tofauti ni iliyopo ni kwasababu ya Viongozi wapumbavu wa CCM kwa kuamua kwa Maksudi kusigina Katiba na kupindisha sheria ili waendelee kuitawala Tanzania kama vile ni mali yao. Nitafafanua. Baada ya machafuko huko Kenya mwaka 2007 Wakenya waliamua kuunda Katiba mpya ambayo ndiyo inaendesha nchi kwa sasa.
Chini ya Katiba hiyo walifanikiwa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka(IEBC)ambayo ndiyo imesimamia Uchaguzi wa Kenya kwa Uhuru na Haki.
  1. Tanzania CCM wamekataa Katiba kwa vile wanaiangalia Tanzania kama mali yao. Hawataki kutengeneza Katiba mpya wala Tume Huru ya Uchaguzi kwa vile wanaona vitu hivo ni tishio(threat) kwa ya kupoteza madaraka.
  2. Lakini pia CCM hawahawa hata Katiba iliyopo wanaipindisha ili kuendelea kujikita Ikulu. Rais JPM amezuia Mikutano na Maandamano kwa vlle anaona Upinzani wakiruhusiwa kuandamana watakosoa na ataonekana Rais dhaifu!!
  3. Lakini pia Rais JPM amekataa kurejesha mchalato wa kupata Katiba mpya kwasababu hizo hizo za hofu ya kung'olewa madarakani na Wapinzani pindi akionekana ana boronga. Kwa hofu hiyo sasa kaamua kuchukua upande wa Kidikteta kwa kuzuia kila kitu cha Upinzani kisionekane, kusikika wala kuzungumzwa. Tumeshuhudia Kuzuiliwa kwa Bunge Mubashara, kuzuia Maandamano na Mikutano ya Upinzani, Kuwakamata na Kuwafunga jela au mahabusu Wabunge wa Upinzani na Kuwanyamazisha na au Kuwafukuza Wabunge wa upinzani toka Bungen(saa 24/48).
  4. Zote hizi ni mbinu za Serikali ya Magufuli kuwaminya Wapinzani ili abakia kusikika yeye tu kila . Huu ndiyo upuuzi ambao umma mkubwa wa Watz hautakubaliano nao.
Baba wa Taifa Mwl . Nyerere (Mungu amrehemu) alifika mahali akasema kama watu wataamua kumbeba Kiongozi yoyote wa kisiasa/upinzani na kumzungusha nchi nzima kwa Maandamano acha wafanye hivo. Kuzuia ni kutaka kuwapa WA[INZANI UMAARUFU usio wa lazima!!!Lakini maskini JPM hataki kusikia Ushauri huu yeye ameamua kupambana na wapinzani hadi mwisho wa Utawala wake na hajui kuwa anazidi kuharibu!!!
absolutely true what you have commented....

Viongozi wa CCM siku zote wanatanguliza mbele maslahi yao binafsi na ya Chama Chao....

Watu wa CCM siku zote maslahi ya nchi kwao siyo priority......

Hebu ona kule Bungeni namna Spika Ndugai anavyowatimua wabunge wa upinzani eti kisa wanaikosoa serikali ya CCM!
 
kwa sababu yà ukweli kuwa kenya na wakenyà wanatuzidi katika mambo mengi basi tuna inferiority nào.Post yako is a result of that

Sisi tuko kimataifa zaidi ,naangalia na kujifunza matukio ya dunia nzima sio Kenya tu, mimi Kenya sina cha kujifunza, na ukitaka kuwa mshindani hapa duniani unatakiwa uangalie na mtu anaefanya vizuri katika Nyanja ile ili ujifunze, ndio maana case study zote za Japanese/Asian kuhusu economy hawadili na Europe zote ni USA , maana ndo yuko juu, njoo na facts na compare demokrasi ya Kenya before na after elections,je majority wanasema nini? sio kuona kwenye tv tu ukakimbia kuja hapa nakusema Magufuli fuata uhuru inavyofanya, usiangalie tu upande wa rulling party, angalia pia opposition wanasemaje? lasivyo utakuwa huwatendei haki wapinzani ambacho tunapinga Tanzania pia tunapinga Kenya . Angalia pia opposition leaders nchi zingine kama Uganda --besigye anasema nini juu ya demokrasia au uchaguzi huu wa kenya? , lakini ukichukua case study moja tu ya Jubilee na Chadema ukahalalisha demokrasia ya nchi mbili basi ni makosa.
 
...nawashangaa sana sana watanzania haswa viongozi wa asasi mbali mbali kumwacha rais wa tz kuminya haki hii ya msingi ya kikatiba.....inashangaza na kusikitisha sana...kumwona mtu mmoja tu Tundu Lissu akilikemea hili...
 
absolutely true what you have commented....

Viongozi wa CCM siku zote wanatanguliza mbele maslahi yao binafsi na ya Chama Chao....

Watu wa CCM siku zote maslahi ya nchi kwao siyo priority......

Hebu ona kule Bungeni namna Spika Ndugai anavyowatimua wabunge wa upinzani eti kisaa wanaikosoa serikali ya CCM!

I remember one book titled ' A LONG WALK TO UHURU'' yaani kutembea mwendo mrefu kufikia Uhuru. Ndivyo ilivyo Tanzania kwa sasa kabla ya kufikia Uhuru wa kweli. Tulicho nacho ni Uhuru Bandia chini ya CCM ambayo ilishasema Wapinzani hawatakaa waingie Ikulu Bara au Visiwani. Tumeyaona yaliyotokea Uchagauzi Mkuu huko Zanzibar, kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) kwa makusudi iliamua kufuta matokeo baada ya kuona ushindi unaenda kwa CUF!!
CCM wako radhi kufuta hata matokeo ya Nchi nzima kwa maana ya Tanzania Bara kama wataona ushindi unaelekea kuchukuliwa na Upinzani kwa vile hizi Tume za Uchaguzi za NEC na ZEC ni zao na kuna watu wao mle ambao hawawezi kukubali CCM ishindwe na kuna sheria walisha jitengezea za kuhakikisha CCM inashinda kwa gharama zozote!!!

Kwa kweli Tanzania bado tuna safari ndefu............!!
 
wapinzani wa kenya wanajielewa na wanajua wanachokisimamia, huwezi kulinganisha na ukawa ambao hata ukiwauliza wanataka nini huwezi kupata majibu ya kueleweka.
 
Back
Top Bottom