Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Huyu wetu anakosa ueledi wa kuwaona WaTz kama nao ni muhimu ktk uongozi wake, Bali huamini kichwa chake na hulka yake!! Alishasema Katiba si kipaumbele chake. Akiamini yeye kama yeye anaweza kunyoosha nchi!!

Washauri wake wafanye kazi ya ziada kumfanya kuwa democrat

Cairo's
Haiwezekani Rais wetu aamini kuwa kila anayemkosoa amchukulie kuwa mtu huyo ana lengo la kumjaribu........

Na kulielekeza Jeshi la Polisi kumkamata mtu yeyote anayetoa maneno ya kumkosoa.......

Hebu aige mfano wa mwenzake Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye ameruhusu wafuasi wa Raila Odinga wanaopinga matokeo yaliyomtangaza yeye kuwa Rais waweze kuandamana na kuliagiza Jeshi lake la Polisi kuyalinda maandamano hayo ili yawe ya amani.
 
Kama kweli wakenya wangekuwa wanamkubali JPM kama unavyotaka kutuaminisha basi wangemchagua "mshirika" wake Raila.......

Sasa ni kwanini wakenya wamempiga chini Raila na kumchagua Uhuru Kenyatta?

Jibu liko wazi kuwa wakenya hawakutaka style ya utawala wa TZ ihamie kwao Kenya, style hiyo si nyingine bali ya ONE MAN SHOW........
Mbona unakuwa mgumu kuelewa vitu vyepesi, nimekuambia kwa wakenya ukabila ndio kigezo namba moja ktk uchaguzi - hivyo unapokuja uchaguzi ni lazima watamtosa Raila ingawa hilo haliondoi ukweli kwamba wakenya wengi wanampenda ngosha!
Na hii nakupa sio kwamba ni simulizi, nimeishuhudia mwenyewe, Raila yeye anahukumiwa kwa kigezo cha ukabila ila wakenya wengi wanampenda sana ngosha.
Kumbuka Kenya kuna ufisadi sana, sasa kinachowavutia wengi kwa ngosha ni utumbuaji majipu....wanatamani na kiongozi wao afanye kama ngosha!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuelewa.Kwani Magufuli amevunja Katiba?Hawa wenzetu wa Kenya kumbuka walifanya mabadiliko kwenye Katiba.Halafu wakati mwingine tusisahau hawa marais ni binadamu.Bahati nzuri nina DSTV imejaa channels za Kenya na mm nimfuatiliaji wa Channels hizi.Ukimuangalia Kenyata anaufanya Urais so simple.Ukiingia ukumbini ukakuta anahutubia kama haumfahamu unaweza usitambue kama ni Rais wa Nchi anautubia.The guy is simply so simple.Mungu ibariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unayesema Rais hajavunja Katiba, hebu kaisome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) ambayo inaeleza wazi kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vinapaswa vifanye shughuli zake vikiwa huru na kutoingiliwa na chombo kingine chochote.....

Sasa hebu nieleze Rais wetu amepata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020, wakati akiruhusu chama chake cha CCM kufanya mikutano ya kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na vyombo vya usalama?
 
Kama unampenda sana kenyata hamia kenya, by the way ukiondoa ukabila - wakenya wanamkubali ngosha vibaya kabisa asikuambie mtu!
Ngosha anafungamana na Raila nikweli kabisa, ila wakenya wengi kamwe hawawezi kumuunga mkono raila kwa sabb ya ukabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani kakuambia wanamkubali ngosha? Kwa kipimo kipi unacholinganishia? Kwa taarifa yako wanamkubali zaidi Ali Kiba kuliko Ngosha maana wananunua album zake kuliko kumsikiliza ngosha.
 
Mbona unakuwa mgumu kuelewa vitu vyepesi, nimekuambia kwa wakenya ukabila ndio kigezo namba moja ktk uchaguzi - hivyo unapokuja uchaguzi ni lazima watamtosa Raila ingawa hilo haliondoi ukweli kwamba wakenya wengi wanampenda ngosha!
Na hii nakupa sio kwamba ni simulizi, nimeishuhudia mwenyewe, Raila yeye anahukumiwa kwa kigezo cha ukabila ila wakenya wengi wanampenda sana ngosha.
Kumbuka Kenya kuna ufisadi sana, sasa kinachowavutia wengi kwa ngosha ni utumbuaji majipu....wanatamani na kiongozi wao afanye kama ngosha!!



Sent using Jamii Forums mobile app
Sijasema kuwa yote anayoyafanya JPM kuwa ni mabaya, la hasha.

Yapo mambo anayoyafanya ambayo ni mazuri kama vile kuwadhibiti watumishi wa Umma ambao walikuwa wakifanya kazi kwa mazoea.....

Hata hivyo yeye kama Rais wa nchi ni lazima aongoze nchi kwa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama, kwa kuwa aliapa kuitii na kuilinda Katiba yetu kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa hili.

Kwa mfumo anaotumia wa kuyageuza matamko yake ya kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa sheria, hilo ni jambo la hatari ambalo linaweza kuja kulitumbukiza katika hatari Taifa letu.
 
Wewe unayesema Rais hajavunja Katiba, hebu kaisome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) ambayo inaeleza wazi kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vinapaswa vifanye shughuli zake vikiwa huru na kutoingiliwa na chombo kingine chochote.....

Sasa hebu nieleze Rais wetu amepata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020, wakati akiruhusu chama chake cha CCM kufanya mikutano ya kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na vyombo vya usalama?
Nimekuelewa ila naomba nisiingie kwenye mjadala huu kwani mm si mtaalam eneo hili.Naomba unilinde.Mungu ibariki Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona unakuwa mgumu kuelewa vitu vyepesi, nimekuambia kwa wakenya ukabila ndio kigezo namba moja ktk uchaguzi - hivyo unapokuja uchaguzi ni lazima watamtosa Raila ingawa hilo haliondoi ukweli kwamba wakenya wengi wanampenda ngosha!
Na hii nakupa sio kwamba ni simulizi, nimeishuhudia mwenyewe, Raila yeye anahukumiwa kwa kigezo cha ukabila ila wakenya wengi wanampenda sana ngosha.
Kumbuka Kenya kuna ufisadi sana, sasa kinachowavutia wengi kwa ngosha ni utumbuaji majipu....wanatamani na kiongozi wao afanye kama ngosha!!



Sent using Jamii Forums mobile app

Ninachoamini ni kwamba Watu wanatawaliwa kama walivyo.Ukiwatawala tofauti na walivyo hakukaliki.Kwa hiyo kama kuna mazuri au mabaya yanayotendwa na viongozi na uone wananchi wametulia elewa ndivyo wanavyopenda kutawaliwa.
 
Nani kakuambia wanamkubali ngosha? Kwa kipimo kipi unacholinganishia? Kwa taarifa yako wanamkubali zaidi Ali Kiba kuliko Ngosha maana wananunua album zake kuliko kumsikiliza ngosha.
Bora Mkuu umempa vipande vyake huyo kada ......

Hiyo ni propaganda ambayo maccm wanapenda kiitumia hao CCM ili kutuaminisha wananchi kuwa mapenzi ya kupendwa Magu yamevuka hata nje ya mipaka yetu.......
 
Kenya wanaweza kuandamana maana hawana kauli mbiu kama ya rais wetu HAPA KAZI TU
Na bado wakiandamana atawapiga risasi, mbona hawasemi wangapi wameuawa, mbona hawasemi mtaalamu wa ICT Aliyeuawa? Halafu mnasifia ujinga.
 
Ninachoamini ni kwamba Watu wanatawaliwa kama walivyo.Ukiwatawala tofauti na walivyo hakukaliki.Kwa hiyo kama kuna mazuri au mabaya yanayotendwa na viongozi na uone wananchi wametulia elewa ndivyo wanavyopenda kutawaliwa.
Ngoja nipingane nawe Mkuu.

Siamini kuwa watu wapo kimya kwa kuwa wameridhika na hatua ya watawala wetu ya kutuziba midomo.....

Ila ninachoamini ni kuwa watu wanaamua kukaa kimya kwa kuwa wanayaogopa magari ya washawasha na virungu vya Polisi na kuogopa kufunguliwa mashitaka ya uchochezi na kulazimishwa kwenda kupimwa mkojo!
 
Watu mnamsifia sana Kenyatta lakini mkumbuke na haya, mwenyekiti as tume ya uchaguzi Kenya aliuawa na serikali baada ya yeye kusema hakuna anayeweza kuingia kwenye system isipokuwa yeye Tu kwa kutumia finger print zake,
Uhuru tayari kashawapiga mkwara majaji kuhusu kesi yoyote itakayoletwa na upinzani dhidi yake.
Uhuru kajilimbikizia Mali na mashamba kama sumaye.
Na kama yeye anademokrasia ya UKWELI si aruhusu wapinzani waangalie matokeo kwenye hiyo system ya IEBC ili wajiridhishe.
 
Ngoja nipingane nawe Mkuu.

Siamini kuwa watu wapo kimya kwa kuwa wameridhika na hatua ya watawala wetu ya kutuziba midomo.....

Ila ninachoamini ni kuwa watu wanaamua kukaa kimya kwa kuwa wanayaogopa magari ya washawasha na virungu vya Polisi na kuogopa kufunguliwa mashitaka ya uchochezi na kulazimishwa kwenda kupimwa mkojo!

Uoga wako ndio umaskini wako.Kwani unafikiri Kenya imefikia hapo kwa uoga au unadhani walizaliwa wakiwa na katiba nzuri?au Maendeleo ya Dunia yamefikishwa hapa na watu waoga.Ukiwa mwoga hutaweza kujifunza hata kuendesha Baiskeli sembuse kurusha ndege.Majasiri ndio wamefanya mpaka watu wakafika Mwezini.
Mimi nakuhakikishia kwamba watu wameridhika na jinsi wanavyotawaliwa.
 
Tunatamani kuwa huru kama Wakenya.
Tunatamani watanzania tuheshimiane kama wakenya.
Tunatamani wabunge wetu na madiwani waheshimiwe.
Tunatamani tuwe na uhuru wa kupata habari na kutoa maoni.
Tunatamani nchi iendeshwe kwa kufata haki na utawala wa sheria.
Tunatanani chaguzi zetu ziwe huru na za haki.
 
Back
Top Bottom