Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Mjanja amegundua this time akiwazuia kwa mtutu

anarudi the Heague.

Hata hivyo katembeza kipigo kwa raia hadi basi, kachapa kule Kisumu, homabay,kibera, mathare hadi mtoto kafariki, watu wakaanza kulaani,juzi kati odinga kaliamsha dude ndo katoka alikojificha kwa aibu ya wizi wa kura anasema maandamano yalindwe, yalindwe wakati watu tayari wameshakufa? hapa kwetu tunasema hiyo ndo demokrasi tuige, poor Africans.
 
wapinzani wa kenya wanajielewa na wanajua wanachokisimamia, huwezi kulinganisha na ukawa ambao hata ukiwauliza wanataka nini huwezi kupata majibu ya kueleweka.

Aise acha upumbavu haro!
Kusema Wapinzani wa Kenya wanajielewa ni ujinga na ushenzi ambao hauwezi kukubalika.Upinzani ni upinzani tu swala hapa ni VIPI SHERIA NA KATIBA YA NCHI zinatoa haki kwa upinzani. Is not an issue of self awareness or what!
Kama KATIBA ya Tanzania imeruhusu mfumo wa vyama vingi kwa kupiga kura,kuchagua,na kuongoza lakini MTU MMOJA kama Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Serikali ya CCM anapozuia vyama vingine wasifanye siasa unategemea nini? Je,utasema kosa ni la wapinzani kujielewa au ni tatizo la Watawala wa chama fulani wasotaka kuona vyama vingine vikikamata dola??
 
Tumemsikia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipolihutubia Taifa lake baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya, kuwa anawaruhusu wafuasi wa mshindani wake mkuu kisiasa Raila Odinga kuwa wanaruhusiwa kuandamana na kuelezea hisia zao kwa kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba na akaliagiza Jeshi la Polisi la nchi hiyo liyalinde maandamano hayo na wala wasiwazuie wananchi hao kuandamana.

Nimejaribu kulinganisha kauli ya Rais wa Kenya na kauli ya Rais wetu nimeona zinatofautiana sana kama umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!

Tumeshuhudia hapa nchini kwetu Rais wetu akipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akijiruhusu yeye mwenyewe na chama chake kuendelea na shughuli za kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Tumewahi kumsikia Rais wetu wakati ule ambapo vyama vya upinzani waliopokuwa wakipanga maandamano waliyoyapa jina la UKUTA, Rais wetu alipiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi!

Tumeshuhudia nchini kwetu viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani wakikamatwa na Jeshi la Polisi hata pale wanapofanya vikao vya ndani kwa kile ambacho kimekuwa kikiitwa tuhuma za uchochezi kwa kile ambacho Jeshi hilo limekuwa likidai ni maelekezo toka juu.........

Kama nchi yetu inaongozwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inaelezea kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vina Uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa, sasa ni kwa nini Rais wetu anaamua kuivunja Katiba ya nchi yetu na kuamua kuendesha nchi yetu iwe kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja?
Pkease don't put words in Mr. Kenyatta's mouth. Kasema abaruhusu maandamano ya amani. Haya ni maandamano ya Pasaka; Maulidi ya Mtume; Wazee wa World War 2; na graduation ya dogodogo Centre. Hebu nikuulize: unategemea maandano ya amani Halima Mdie mbele Mchungaji Msigwa katikati na Sharif Hamad nyuma? Kimwete aliwaita Mbowe na Tundulissu wanywe chai Ikulu mwrnzao Mnyika akasena Rais ni dhaifu. Lakini nani hajui Kenya ibaendeshwa na Ukabila?
 
Kama unampenda sana kenyata hamia kenya, by the way ukiondoa ukabila - wakenya wanamkubali ngosha vibaya kabisa asikuambie mtu!
Ngosha anafungamana na Raila nikweli kabisa, ila wakenya wengi kamwe hawawezi kumuunga mkono raila kwa sabb ya ukabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
Punguza hisia hata kama wewe ni mwanamke!Hisia huondoa uwezo wa kufikiri kwa kina.Samahani lakini
 
WAKENYA WALISHUTUKA, HUWEZI KUWA NA URAFIKI NA MTU MSIWE NA TABIA ZINAZOFANANA, waswahili wanasema "birds of a feather flock together" Wangemchagua Odinga angeweza kuwa Dictator kama Dikteta uchwara. Kenya ndio nchi pekee iliyobaki katika ukanda huu nyenye Demokrasia ya kweli, na viongozi wanaoheshimu katiba.
 
I remember one book titled ' A LONG WALK TO UHURU'' yaani kutembea mwendo mrefu kufikia Uhuru. Ndivyo ilivyo Tanzania kwa sasa kabla ya kufikia Uhuru wa kweli. Tulicho nacho ni Uhuru Bandia chini ya CCM ambayo ilishasema Wapinzani hawatakaa waingie Ikulu Bara au Visiwani. Tumeyaona yaliyotokea Uchagauzi Mkuu huko Zanzibar, kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) kwa makusudi iliamua kufuta matokeo baada ya kuona ushindi unaenda kwa CUF!!
CCM wako radhi kufuta hata matokeo ya Nchi nzima kwa maana ya Tanzania Bara kama wataona ushindi unaelekea kuchukuliwa na Upinzani kwa vile hizi Tume za Uchaguzi za NEC na ZEC ni zao na kuna watu wao mle ambao hawawezi kukubali CCM ishindwe na kuna sheria walisha jitengezea za kuhakikisha CCM inashinda kwa gharama zozote!!!

Kwa kweli Tanzania bado tuna safari ndefu............!!
Absolutely true.

Ulichokisema ni kweli tupu, kuwa hata uchaguzi wa kila baada ya miaka 5 unafanyika kama mjini macho tuu.....

Inafahamika wazi kuwa watawala huwa wanakuwa "weshajifungia" kwenye vikao vya siri na Tume zetu za uchaguzi na kuwaekekeza matokeo wanavyotaka wao watawala yawe....

Tumeshuhudia namna Jecha kule Zenji alivyofuta matokeo ambayo yalikuwa yanampa ushindi Maalim Seif.

It is true that we have a long walk to "real" Uhuru.....
 
WAKENYA WALISHUTUKA, HUWEZI KUWA NA URAFIKI NA MTU MSIWE NA TABIA ZINAZOFANANA, waswahili wanasema "birds of a feather flock together" Wangemchagua Odinga angeweza kuwa Dictator kama Dikteta uchwara. Kenya ndio nchi pekee iliyobaki katika ukanda huu nyenye Demokrasia ya kweli, na viongozi wanaoheshimu katiba.
Very true.

Raila na Mheshimiwa wetu they are best friends...
 
Pkease don't put words in Mr. Kenyatta's mouth. Kasema abaruhusu maandamano ya amani. Haya ni maandamano ya Pasaka; Maulidi ya Mtume; Wazee wa World War 2; na graduation ya dogodogo Centre. Hebu nikuulize: unategemea maandano ya amani Halima Mdie mbele Mchungaji Msigwa katikati na Sharif Hamad nyuma? Kimwete aliwaita Mbowe na Tundulissu wanywe chai Ikulu mwrnzao Mnyika akasena Rais ni dhaifu. Lakini nani hajui Kenya ibaendeshwa na Ukabila?
Nilichom-quote Uhuru Kenyatta alichosema ni kuwa as far as hao wafuasi wa Raila Odinga wana haki ya kuandamana kwa amani kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya Kenya kwa hiyo akasema yeye kama Rais hawazuii kufanya maandamano yao....

Na akatoa wito kwa Polisi wa Kenya wayalinde maandamano hayo sehemu yatakapopita ili yasilete uvunjifu wa amani.

Sasa wewe unapojudge kuwa iwapo akina Halima Mdee, Godbless Lema na Maalim Seif maandamano yeo hayatakuwa ya amani. Ina maana wewe unafanya kazi ya utabiri kama zilivyokuwa zikifanywa na akina Sheikh Yahya?
 
Mbona unakuwa mgumu kuelewa vitu vyepesi, nimekuambia kwa wakenya ukabila ndio kigezo namba moja ktk uchaguzi - hivyo unapokuja uchaguzi ni lazima watamtosa Raila ingawa hilo haliondoi ukweli kwamba wakenya wengi wanampenda ngosha!
Na hii nakupa sio kwamba ni simulizi, nimeishuhudia mwenyewe, Raila yeye anahukumiwa kwa kigezo cha ukabila ila wakenya wengi wanampenda sana ngosha.
Kumbuka Kenya kuna ufisadi sana, sasa kinachowavutia wengi kwa ngosha ni utumbuaji majipu....wanatamani na kiongozi wao afanye kama ngosha!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uongo mkuu....tangu Ngosha aingie tumekuwa "kituko" mbele ya wakenya.... wanamuona yupo standards za chini sana kuwa Rais
 
Lakini kinachodaiwa si kipokwenye katiba kama ilivyo kwenye katiba ya kenya?

Sent using Jamii Forums mobile app
Absolutely right.

Kwenye Katiba ya Kenya maandamano ya wananchi yanaruhusiwa........

Kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, vivyo hivyo maandamano yanaruhusiwa......

Iweje basi Kenya maandamano hayo yawe halali kufanyika na huku kwetu TZ yawe haramu?
 
Back
Top Bottom