Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Tatizo la hapa Tanzania ukiruhusu tu maandamano ndokusema umefungulia na vibaka kufanya mambo yao!
That is not true....

Ila maandamano ya kupendekeza Bwana mkubwa wetu awe Life President wetu ndiyo hayana vibaka!
 
Ni kwamba hashauriki.. ...

Alishasema kuwa yeye ni Rais anayejiamini na hakushauriwa na mtu yeyote kwenda kuchukua fomu ya kugombea Urais bali aalienda mwenyewe kwa hiyo hataki mtu yeyote amuelekeze la kufanya......

Kwa hiyo na KURA alijipigia??
 
Kwa hiyo na KURA alijipigia??
Umemuuliza swali zuri sana.

Tusubiri ifikapo 2020 tuone kama kura yake moja na ya mama Jesca ndizo zitakazomrudisha Ikulu!
 
Kama tunataka demokrasia ya kweli basi hatuna budi kujifunza kutoka America, tuachaneni na hizi taka taka za Kenya ,watu wengi wanaifahamu Kenya itakuwa ni vigumu sana kuwabadili mawazo, Obama for me is the champions of democracy in the world at the moment, ni vizuri tukamwambia Magufuli ajaribu kupitia hotuba zake kuna kitu atajifunza, Obama kitu alichokuwa akiongea na kutenda vinawiana, hata juzi ambapo kulikuwa na maandamano mtu mmoja akapoteza maisha na wengine kujeruhiwa at Charlottesville, Obama kashusha bonge la message ,ule ujumbe ni wakibinadamu, hata ukiisoma unajua kweli Obama ni kiongozi, leo hii mimi ukiniambia eti Magufuli should learn from Uhuru,atajifunza nini? ajifunze matakataka atuletee nchini maana yake ni kuizika demokarasia na kuanza kuchapana sisi kwa sisi. Hebu tubadilikeni.
 
Tumemsikia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipolihutubia Taifa lake baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya, kuwa anawaruhusu wafuasi wa mshindani wake mkuu kisiasa Raila Odinga kuwa wanaruhusiwa kuandamana na kuelezea hisia zao kwa kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba na akaliagiza Jeshi la Polisi la nchi hiyo liyalinde maandamano hayo na wala wasiwazuie wananchi hao kuandamana.

Nimejaribu kulinganisha kauli ya Rais wa Kenya na kauli ya Rais wetu nimeona zinatofautiana sana kama umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!

Tumeshuhudia hapa nchini kwetu Rais wetu akipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akijiruhusu yeye mwenyewe na chama chake kuendelea na shughuli za kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Tumewahi kumsikia Rais wetu wakati ule ambapo vyama vya upinzani waliopokuwa wakipanga maandamano waliyoyapa jina la UKUTA, Rais wetu alipiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi!

Tumeshuhudia nchini kwetu viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani wakikamatwa na Jeshi la Polisi hata pale wanapofanya vikao vya ndani kwa kile ambacho kimekuwa kikiitwa tuhuma za uchochezi kwa kile ambacho Jeshi hilo limekuwa likidai ni maelekezo toka juu.........

Kama nchi yetu inaongozwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inaelezea kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vina Uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa, sasa ni kwa nini Rais wetu anaamua kuivunja Katiba ya nchi yetu na kuamua kuendesha nchi yetu iwe kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja?
Mtu jasiri haogopi mtu wa watu husikiliza hisia za watu yumkini akapata jambo moja jema katikati ya mambo mengi ya hovyo. Mtu mwoga huwa daima hajiamini na wala hawezi ruhusu mwinyine kusema lolote labda awe anamsifia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama tunataka demokrasia ya kweli basi hatuna budi kujifunza kutoka America, tuachaneni na hizi taka taka za Kenya ,watu wengi wanaifahamu Kenya itakuwa ni vigumu sana kuwabadili mawazo, Obama for me is the champions of democracy in the world at the moment, ni vizuri tukamwambia Magufuli ajaribu kupitia hotuba zake kuna kitu atajifunza, Obama kitu alichokuwa akiongea na kutenda vinawiana, hata juzi ambapo kulikuwa na maandamano mtu mmoja akapoteza maisha na wengine kujeruhiwa at Charlottesville, Obama kashusha bonge la message ,ule ujumbe ni wakibinadamu, hata ukiisoma unajua kweli Obama ni kiongozi, leo hii mimi ukiniambia eti Magufuli should learn from Uhuru,atajifunza nini? ajifunze matakataka atuletee nchini maana yake ni kuizika demokarasia na kuanza kuchapana sisi kwa sisi. Hebu tubadilikeni.
Nakubaliana nawe Mkuu ya kwamba ni vigumu kwa nchi za kiafrika kufikia kiwango cha demokrasia iliyofikiwa na mataifa makubwa ya magharibi for example USA.

Hata hivyo kama ilivyo kwenye FIFA rankings, Tanzania tunatrail behind Kenya kwa namna walivyoipanua demokrasia yao.

Kumbuka hapa nchini Mkuu wa nchi akitamka hadharani kuwa amepiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020, huku akijua kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inaeleza wazi kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vinatakiwa kufanya shughuli zao vikiwa huru.....

Ndiyo maana tukifanya comparison ya Uhuru Kenyatta kusema anawaruhusu wapinzani wanaotaka kuandamana kupinga matokeo yaliyompa Urais yeye na akawaelekeza Polisi kuwa wajibu wao siyo kuzuia maandamano hayo Bali kuyalinda ili yafanyike kwa amani......

Sasa compare na hapa kwetu walipokuwa wanapanga kuandamana katika yale maandamano waliyoyapa jina la UKUTA.....

Unakumbuka nini kilitokea?

Ni Mkulu kupiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi na kwa Mara ta kwanza nchini kwetu tokea baada ya vita ya Kagera miaka ile ya 70, tuliwashudia maaskari wetu wakifanya mazoeslzi yao ya kivita huku uraiani huku kila mtu akishuhidia .....

Kitendo cha vikosi vya Ulinzi na Usalama kufanya mazoezi yao ya kivita uraiani yalikuwa yana lengo la kuwatisha wananchi wasifanye maandamano yake ambayo ni haki yao ya kikatiba kuyafanya.....
 
Sasa wewe Utafanisha vipi Uhuru na Pombe?

Huyu hawezi akawa kama Uhuru, keshakuwa Pombe tayari
 
Mtu jasiri haogopi mtu wa watu husikiliza hisia za watu yumkini akapata jambo moja jema katikati ya mambo mengi ya hovyo. Mtu mwoga huwa daima hajiamini na wala hawezi ruhusu mwinyine kusema lolote labda awe anamsifia

Sent using Jamii Forums mobile app
Very true....
 
Sasa wewe Utafanisha vipi Uhuru na Pombe?

Huyu hawezi akawa kama Uhuru, keshakuwa Pombe tayari
Mkuu usije ukatakiwa kwenda kupimwa mkojo kwa tuhuma ya uchochezi?
 
Mzee hivi kweli umpe Godbles Lema Masaa 4 azungumze na watanzania..unajua matokeo yake..wewe utakuwa wa kwanza kwenda kuliamsha dude la maandamano...na ndo utajua watanzania wengi ni wapinzani wa CCM ila sijuagi CCM wanashindaje..
 
Je wanashinda kimiujiza?

Au ndiyo wanapata ushindi wa goli la mkono kama ambavyo Nape aliwahi kuujulisha Umma wa watanzania?
 
Nilipenda Uhuru zaidi alisema niliwahi kugombea urais nilishindwa lakini nilienda nikasubiri but now nimeshinda...............

Tena mnafanya kosa sana kumfananisha UHURU na Magufuli maana ni shida hana ethics wala hajui uongozi ni nini yeye ni mnyapara kabisa hatakaa awe kiongozi
 
Rais wetu anapaswa aruhusu freedom of expression kama inavyoelezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1)

Katiba hiyo Rais wetu aliapa kuitii na kuilinda kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa letu

Ulishawahi kusikia Kemya wamefanya siasa baada ya uchaguzi? Kama jibu ni ndio, basi una haki ya kueleza zaidi ili kumtofautisha JPM na UK
 
Back
Top Bottom