Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Tumemsikia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipolihutubia Taifa lake baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya, kuwa anawaruhusu wafuasi wa mshindani wake mkuu kisiasa Raila Odinga kuwa wanaruhusiwa kuandamana na kuelezea hisia zao kwa kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba na akaliagiza Jeshi la Polisi la nchi hiyo liyalinde maandamano hayo na wala wasiwazuie wananchi hao kuandamana.

Nimejaribu kulinganisha kauli ya Rais wa Kenya na kauli za Rais wetu anazopendelea kuzitoa mara kwa mara nimeona zinatofautiana sana kama umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!

Tumeshuhudia hapa nchini kwetu Rais wetu akipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akijiruhusu yeye mwenyewe na chama chake kuendelea na shughuli za kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Tumewahi kumsikia Rais wetu wakati ule ambapo vyama vya upinzani waliopokuwa wakipanga maandamano waliyoyapa jina la UKUTA, Rais wetu alipiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi!

Tumeshuhudia nchini kwetu viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani wakikamatwa na Jeshi la Polisi hata pale wanapofanya vikao vya ndani kwa kile ambacho kimekuwa kikiitwa tuhuma za uchochezi kwa kile ambacho Jeshi hilo limekuwa likidai ni maelekezo toka juu.........

Kama nchi yetu inaongozwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inaelezea kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vina Uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa, sasa ni kwa nini Rais wetu anaamua kuivunja Katiba ya nchi yetu na kuamua kuendesha nchi yetu iwe kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja?
 
Rais wetu anapaswa aruhusu freedom of expression kama inavyoelezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1)

Katiba hiyo Rais wetu aliapa kuitii na kuilinda kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa letu
 
Ninamkumbuka mzee kingunge alisema huyu alistahili kuwa mnyampala wa barabara na si vinginevyo sasa yametimia.
It is very true.

Haiwezekani kwa nafasi kubwa kama ya Urais halafu uamue kuongoza nchi kwa jinsi unavyojisikia mwenyewe badala ya kuongoza nchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
 
Kenyata ni kiongozi na huyo mwingine ni mtawala, na yeye anapenda kutawala kuliko kuongoza!

Sent using Jamii Forums mobile app
On top of that, Uhuru anajiamini kwa vile kashinda kihalali Magufuli hajiamini na haamini kama kweli alishinda uchaguzi, anategemea jeshi la polisi kutawala, ndiyo maana kila siku haishi kusema mimi ndiye rais.
 
Kama unampenda sana kenyata hamia kenya, by the way ukiondoa ukabila - wakenya wanamkubali ngosha vibaya kabisa asikuambie mtu!
Ngosha anafungamana na Raila nikweli kabisa, ila wakenya wengi kamwe hawawezi kumuunga mkono raila kwa sabb ya ukabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu! Kujiamini ni silaha nzito sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
On top of that, Uhuru anajiamini kwa vile kashinda kihalali Magufuli hajiamini na haamini kama kweli alishinda uchaguzi, anategemea jeshi la polisi kutawala, ndiyo maana kila siku haishi kusema mimi ndiye rais.
Refer kauli aliyoitoa EL hivi karibuni ambayo ilimtia matatani hadi akakamatwa na kufikishwa Polisi kuhojiwa, pale aliposema kuwa kura "hazikuhesabiwa" vizuri kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.......
 
Kama unampenda sana kenyata hamia kenya, by the way ukiondoa ukabila - wakenya wanamkubali ngosha vibaya kabisa asikuambie mtu!
Ngosha anafungamana na Raila nikweli kabisa, ila wakenya wengi kamwe hawawezi kumuunga mkono raila kwa sabb ya ukabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kweli wakenya wangekuwa wanamkubali JPM kama unavyotaka kutuaminisha basi wangemchagua "mshirika" wake Raila.......

Sasa ni kwanini wakenya wamempiga chini Raila na kumchagua Uhuru Kenyatta?

Jibu liko wazi kuwa wakenya hawakutaka style ya utawala wa TZ ihamie kwao Kenya, style hiyo si nyingine bali ya ONE MAN SHOW........
 
Mkuu Mystery Salute.. umesema kweli tupu.

Shida huyu anatumia tabia zake za ASILI kuongoza Nchi..

Badala ya kutumia tabia za KI-UONGOZI na kufata KATIBA ya Nchi ambayo ndio msahafu Mkuu wa kuongoza Nchi..

Hapa ndio tulipo na shida kubwa kwelikweli kama Nchi kwa bwana huyu.
Na watanzania tukiamua kuukalia kimya utawala wa huyu Rais wetu wa kugeuza matamko yake kuwa sheria, hakika Taifa hili litaelekea kuangamia .........

Tujikumbishe pia kauli ya hekima sana aliyowahi kuitoa Baba wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake wakati wa uhai wake aliposema.....

"Ni lazima wananchi mchague Rais ambaye mnaamini ataongoza kwa kufuata Katiba ya nchi yetu ambayo anaapa kuiltii na kuilinda na Mwalimu anaendelea kueleza katika hotuba hiyo kuwa iwapo watanzania mtachagua Rais ambaye hataki kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu, Rais wa aina hiyo HATUFAI" mwisho wa kunukuu.
 
Lingine linalomsumbua sana huyu na kubehave hivi ni kwamba anajua kabisa HAKUSHINDA kihalali and that's why mambo mengi anayaendesha kibabe na sometimes kutumia vyombo vya dola kusimamia lolote atakalo amua hata kama ni kinyume cha Katiba..

Uhuru Kenyatta hawezi kuwa na tabia hizi kwasababu kwanza amekulia katika Uongozi na ni jambo la kawaida kwake kushinda na kushindwa.
 
Huyu wetu anakosa ueledi wa kuwaona WaTz kama nao ni muhimu ktk uongozi wake, Bali huamini kichwa chake na hulka yake!! Alishasema Katiba si kipaumbele chake. Akiamini yeye kama yeye anaweza kunyoosha nchi!!

Washauri wake wafanye kazi ya ziada kumfanya kuwa democrat

Cairo's
 
Hatusemi Kenya ndiyo Tanzania......

Bali tunachosema Rais wetu anapaswa aige mfano wa mwenzake Uhuru Kenyatta, kwa kutawala kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo aliapa kuitii na kuilinda kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa letu
Nakuelewa.Kwani Magufuli amevunja Katiba?Hawa wenzetu wa Kenya kumbuka walifanya mabadiliko kwenye Katiba.Halafu wakati mwingine tusisahau hawa marais ni binadamu.Bahati nzuri nina DSTV imejaa channels za Kenya na mm nimfuatiliaji wa Channels hizi.Ukimuangalia Kenyata anaufanya Urais so simple.Ukiingia ukumbini ukakuta anahutubia kama haumfahamu unaweza usitambue kama ni Rais wa Nchi anautubia.The guy is simply so simple.Mungu ibariki Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: lup
Back
Top Bottom