Rais wetu aige mfano wa mwenzake wa Kenya

Haiwezekani Rais wetu aamini kuwa kila anayemkosoa amchukulie kuwa mtu huyo ana lengo la kumjaribu........

Na kulielekeza Jeshi la Polisi kumkamata mtu yeyote anayetoa maneno ya kumkosoa.......

Hebu aige mfano wa mwenzake Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye ameruhusu wafuasi wa Raila Odinga wanaopinga matokeo yaliyomtangaza yeye kuwa Rais waweze kuandamana na kuliagiza Jeshi lake la Polisi kuyalinda maandamano hayo ili yawe ya amani.
Ndugu yangu kosa pia ni la CCM !! Huwezi mchukua mtu ambayo huko nyuma hakuwahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ktk chama na kumpandisha ghafla, na kumpa vyeo vyote bila kuwa na udhibiti. Huyu bwana angebaki kuwa Rais huku chama kikimuweka sawa kwa muda. Baadaye ndiyo angepewa uenyekiti. Lakini ccm kwa kutaka waendelee kubaki salama wanakimbilia kumpa uenyekiti ili kiendelee kuwa chama dola.

Uhuru ameanza mbali alijaribu na kuanzia upinzani na alianguka mwanzoni. Kesi za the Hague imemfanya kufanya alliance ya nguvu na Ruto (kalenjin) kuukwaa u Rais. Hivyo anajua thamani ya kuwaheshimu wananchi!! Huyu yule mmachinga alidictate mkutano mzima na kumweka hapo hawezi kujua thamani ya kura moja ya mwananchi

Cairo's
 
Ikitokea ktk kipindi cha ngosha cha miaka 10 tukaipita au angalao tukalingana na Kenya kiuchumi basi mapungufu yake sitayamaindi sana.
 
Mbona unakuwa mgumu kuelewa vitu vyepesi, nimekuambia kwa wakenya ukabila ndio kigezo namba moja ktk uchaguzi - hivyo unapokuja uchaguzi ni lazima watamtosa Raila ingawa hilo haliondoi ukweli kwamba wakenya wengi wanampenda ngosha!
Na hii nakupa sio kwamba ni simulizi, nimeishuhudia mwenyewe, Raila yeye anahukumiwa kwa kigezo cha ukabila ila wakenya wengi wanampenda sana ngosha.
Kumbuka Kenya kuna ufisadi sana, sasa kinachowavutia wengi kwa ngosha ni utumbuaji majipu....wanatamani na kiongozi wao afanye kama ngosha!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sisi ufisadi hakuna? Kama hakuna mbona Kenya wametuzid kwa kila kitu? Nini kinakufanya uamini wa Kenya wote wanampenda magufuli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie Uchama imewafunga akili. Hamjui nini kinachoendelea Kenya.
Sababu Lowasa kamsifia Uhuru. Na nyie mnafata mkumbo kumsifia.
Watanzania hatujui tunataka nini.

sent by Samson Cyper
 
Watu mnamsifia sana Kenyatta lakini mkumbuke na haya, mwenyekiti as tume ya uchaguzi Kenya aliuawa na serikali baada ya yeye kusema hakuna anayeweza kuingia kwenye system isipokuwa yeye Tu kwa kutumia finger print zake,
Uhuru tayari kashawapiga mkwara majaji kuhusu kesi yoyote itakayoletwa na upinzani dhidi yake.
Uhuru kajilimbikizia Mali na mashamba kama sumaye.
Na kama yeye anademokrasia ya UKWELI si aruhusu wapinzani waangalie matokeo kwenye hiyo system ya IEBC ili wajiridhishe.
walipewa wasaa kuhakiki fomu zote za matokeo toka vituoni F34/35 kingine kipi walitaka kama sio hizo zilizotiliwa sahihi na mawakala wao?
Lakini kumbuka ni wao waliofungua shauri mahakamani kuiomba mahakama itoe amri kwa tume ya uchaguzi kukubaliana tu na matokeo ya kielektroniki na si vinginevyo,mahakama ikatupilia mbali ombi hilo kwa kuzingatia kuwa endapo patatokea ubishi hapatakuwa na mahali pa kupata rejea ya kuamua ubishi badala yake ikaamuru tume kuthibitisha matokeo ya kielektroniki kwa kutumia F34/35 kabla ya kumtangaza mshindi.
Mkubali tu ndugu zangu tena kwa unyenyekevu kuwa MMEPIGWA...... over
 
Kama unampenda sana kenyata hamia kenya, by the way ukiondoa ukabila - wakenya wanamkubali ngosha vibaya kabisa asikuambie mtu!
Ngosha anafungamana na Raila nikweli kabisa, ila wakenya wengi kamwe hawawezi kumuunga mkono raila kwa sabb ya ukabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama matamanio yako ndio hayo, nchi ndio hatuhami tutabanana hapahapa hadi kieleweke.
 
Rais wetu anapaswa aruhusu freedom of expression kama inavyoelezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1)

Katiba hiyo Rais wetu aliapa kuitii na kuilinda kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa letu
Sio kila kitu tuige Kenya.Mbona husemi tuige kuua watu wanaoleta vikwazo kwa serikali?
Kama unaona tabu hamia kenya tu mtuu ukapate fursa ya kuandamana
 
Tumemsikia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipolihutubia Taifa lake baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya, kuwa anawaruhusu wafuasi wa mshindani wake mkuu kisiasa Raila Odinga kuwa wanaruhusiwa kuandamana na kuelezea hisia zao kwa kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba na akaliagiza Jeshi la Polisi la nchi hiyo liyalinde maandamano hayo na wala wasiwazuie wananchi hao kuandamana.

Nimejaribu kulinganisha kauli ya Rais wa Kenya na kauli ya Rais wetu nimeona zinatofautiana sana kama umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!

Tumeshuhudia hapa nchini kwetu Rais wetu akipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akijiruhusu yeye mwenyewe na chama chake kuendelea na shughuli za kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Tumewahi kumsikia Rais wetu wakati ule ambapo vyama vya upinzani waliopokuwa wakipanga maandamano waliyoyapa jina la UKUTA, Rais wetu alipiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi!

Tumeshuhudia nchini kwetu viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani wakikamatwa na Jeshi la Polisi hata pale wanapofanya vikao vya ndani kwa kile ambacho kimekuwa kikiitwa tuhuma za uchochezi kwa kile ambacho Jeshi hilo limekuwa likidai ni maelekezo toka juu.........

Kama nchi yetu inaongozwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inaelezea kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vina Uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa, sasa ni kwa nini Rais wetu anaamua kuivunja Katiba ya nchi yetu na kuamua kuendesha nchi yetu iwe kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja?
sasa wewe siunajua mukulu ni akili moja ma Odinga na Yule mmasai ni akili moja na Lowassa
 
Ndugu yangu kosa pia ni la CCM !! Huwezi mchukua mtu ambayo huko nyuma hakuwahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote ktk chama na kumpandisha ghafla, na kumpa vyeo vyote bila kuwa na udhibiti. Huyu bwana angebaki kuwa Rais huku chama kikimuweka sawa kwa muda. Baadaye ndiyo angepewa uenyekiti. Lakini ccm kwa kutaka waendelee kubaki salama wanakimbilia kumpa uenyekiti ili kiendelee kuwa chama dola.

Uhuru ameanza mbali alijaribu na kuanzia upinzani na alianguka mwanzoni. Kesi za the Hague imemfanya kufanya alliance ya nguvu na Ruto (kalenjin) kuukwaa u Rais. Hivyo anajua thamani ya kuwaheshimu wananchi!! Huyu yule mmachinga alidictate mkutano mzima na kumweka hapo hawezi kujua thamani ya kura moja ya mwananchi

Cairo's
Very true.

Mtu ambaye hajawahi kuwa hata Mwenyekiti wa serikali ya mtaa, ghafla bin vuu anakuwa Head of State!
 
Uoga wako ndio umaskini wako.Kwani unafikiri Kenya imefikia hapo kwa uoga au unadhani walizaliwa wakiwa na katiba nzuri?au Maendeleo ya Dunia yamefikishwa hapa na watu waoga.Ukiwa mwoga hutaweza kujifunza hata kuendesha Baiskeli sembuse kurusha ndege.Majasiri ndio wamefanya mpaka watu wakafika Mwezini.
Mimi nakuhakikishia kwamba watu wameridhika na jinsi wanavyotawaliwa.
Nakubaliana nawe mkuu kuwa woga wetu ndiyo umetifikisha hapa.

Hata hivyo naamini itafika wakati watanzania nao wataamua kuachana na "utamaduni" wao wa yoga na watadai haki zao by hooks and crooks.....

Refer kauli ya Godbless Lema...Hakuna dhambi kubwa duniani kama woga.....
 
Tumemsikia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipolihutubia Taifa lake baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya, kuwa anawaruhusu wafuasi wa mshindani wake mkuu kisiasa Raila Odinga kuwa wanaruhusiwa kuandamana na kuelezea hisia zao kwa kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba na akaliagiza Jeshi la Polisi la nchi hiyo liyalinde maandamano hayo na wala wasiwazuie wananchi hao kuandamana.

Nimejaribu kulinganisha kauli ya Rais wa Kenya na kauli ya Rais wetu nimeona zinatofautiana sana kama umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!

Tumeshuhudia hapa nchini kwetu Rais wetu akipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akijiruhusu yeye mwenyewe na chama chake kuendelea na shughuli za kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Tumewahi kumsikia Rais wetu wakati ule ambapo vyama vya upinzani waliopokuwa wakipanga maandamano waliyoyapa jina la UKUTA, Rais wetu alipiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi!

Tumeshuhudia nchini kwetu viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani wakikamatwa na Jeshi la Polisi hata pale wanapofanya vikao vya ndani kwa kile ambacho kimekuwa kikiitwa tuhuma za uchochezi kwa kile ambacho Jeshi hilo limekuwa likidai ni maelekezo toka juu.........

Kama nchi yetu inaongozwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inaelezea kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vina Uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa, sasa ni kwa nini Rais wetu anaamua kuivunja Katiba ya nchi yetu na kuamua kuendesha nchi yetu iwe kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja?
Kenyata ana akili timamu, na ana hekima na busara. si wa kulinganisha na madikteta waliobaki EA na adio maana Kenya iko juu kiuchumi kuliko hawa wengine wapiga porojo
 
Watu mnamsifia sana Kenyatta lakini mkumbuke na haya, mwenyekiti as tume ya uchaguzi Kenya aliuawa na serikali baada ya yeye kusema hakuna anayeweza kuingia kwenye system isipokuwa yeye Tu kwa kutumia finger print zake,
Uhuru tayari kashawapiga mkwara majaji kuhusu kesi yoyote itakayoletwa na upinzani dhidi yake.
Uhuru kajilimbikizia Mali na mashamba kama sumaye.
Na kama yeye anademokrasia ya UKWELI si aruhusu wapinzani waangalie matokeo kwenye hiyo system ya IEBC ili wajiridhishe.
Umesahau ya Gen. Nkaissery mkuu.
 
Huyu wetu anakosa ueledi wa kuwaona WaTz kama nao ni muhimu ktk uongozi wake, Bali huamini kichwa chake na hulka yake!! Alishasema Katiba si kipaumbele chake. Akiamini yeye kama yeye anaweza kunyoosha nchi!!

Washauri wake wafanye kazi ya ziada kumfanya kuwa democrat

Cairo's

Washauri weshachoka
 
Washauri weshachoka
Ni kwamba hashauriki.. ...

Alishasema kuwa yeye ni Rais anayejiamini na hakushauriwa na mtu yeyote kwenda kuchukua fomu ya kugombea Urais bali aalienda mwenyewe kwa hiyo hataki mtu yeyote amuelekeze la kufanya......
 
walipewa wasaa kuhakiki fomu zote za matokeo toka vituoni F34/35 kingine kipi walitaka kama sio hizo zilizotiliwa sahihi na mawakala wao?
Lakini kumbuka ni wao waliofungua shauri mahakamani kuiomba mahakama itoe amri kwa tume ya uchaguzi kukubaliana tu na matokeo ya kielektroniki na si vinginevyo,mahakama ikatupilia mbali ombi hilo kwa kuzingatia kuwa endapo patatokea ubishi hapatakuwa na mahali pa kupata rejea ya kuamua ubishi badala yake ikaamuru tume kuthibitisha matokeo ya kielektroniki kwa kutumia F34/35 kabla ya kumtangaza mshindi.
Mkubali tu ndugu zangu tena kwa unyenyekevu kuwa MMEPIGWA...... over
Msipotoshe watu kuhusu Uhuru, uhuru ni mafia zaidi ya Magufuli, hayo anayoongea kwenye media ni tofauti na matendo yake, polisi Kenya wamepewa amri ya shoot and kill kwa wote wanaoandamana, Kisumu, mathare, kibera, rongai etc, mpaka sasa zaidi ya watu 100 wamefariki lakini serikali inasema ni watu 10 tu, na polisi wamekuwa wakitumiwa pesa kwenye mpesa kama motisha ya kuzuia maandamano, mimi sijui watanzania huwa muko dunia gani, Bora magufuli anaetumia ukali kusitisha maandamano ingawaje sio sahihi kikatiba kuliko mtu anaeruhusu kwenye media anaonekana mzuri huku ameshatoa amri kwa jeshi ueni . Kuhusu uchaguzi wa Kenya na wizi wa kura angalia below crips, na kuna maafisa wa IEBC wa kike jana wamepelekwa kotini kuanza kujibu tuhuma za kutoa siri, pia kuna mwandishi wa habari NTV yumo lupango,hivi nyie hamjui Kenya au uhur Kenyatta au mna act tu?
[/QUOTE]
 
Tumemsikia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipolihutubia Taifa lake baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya, kuwa anawaruhusu wafuasi wa mshindani wake mkuu kisiasa Raila Odinga kuwa wanaruhusiwa kuandamana na kuelezea hisia zao kwa kuwa hiyo ni haki yao ya kikatiba na akaliagiza Jeshi la Polisi la nchi hiyo liyalinde maandamano hayo na wala wasiwazuie wananchi hao kuandamana.

Nimejaribu kulinganisha kauli ya Rais wa Kenya na kauli ya Rais wetu nimeona zinatofautiana sana kama umbali wa kutoka duniani hadi mbinguni!

Tumeshuhudia hapa nchini kwetu Rais wetu akipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020 wakati akijiruhusu yeye mwenyewe na chama chake kuendelea na shughuli za kisiasa nchi nzima bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Tumewahi kumsikia Rais wetu wakati ule ambapo vyama vya upinzani waliopokuwa wakipanga maandamano waliyoyapa jina la UKUTA, Rais wetu alipiga mkwara mzito kuwa yeye hajaribiwi!

Tumeshuhudia nchini kwetu viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani wakikamatwa na Jeshi la Polisi hata pale wanapofanya vikao vya ndani kwa kile ambacho kimekuwa kikiitwa tuhuma za uchochezi kwa kile ambacho Jeshi hilo limekuwa likidai ni maelekezo toka juu.........

Kama nchi yetu inaongozwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo inaelezea kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vina Uhuru wa kufanya shughuli zao za kisiasa, sasa ni kwa nini Rais wetu anaamua kuivunja Katiba ya nchi yetu na kuamua kuendesha nchi yetu iwe kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja?
Tatizo la hapa Tanzania ukiruhusu tu maandamano ndokusema umefungulia na vibaka kufanya mambo yao!
 
Back
Top Bottom