Kwa kifupi niishie japa Kwa comment hii ni ya Mwisho kwako
Nisikilize vizuri, na nikwambie mara moja tu.
Usijilinganishe na mimi. Sio kwa dharau, ni kwa ukweli.
Unachokiona kwenye mitandao sio nusu ya nilivyo kihalisia. Mimi sio wa kuigiza, mimi ni wa vitendo.
1. Exposure
Wewe unajua mtaa wako tu. Mimi dunia imenijua kabla hata hujaijua. Nimekutana na watu wakubwa, nimekaa meza kubwa ambazo wewe huwezi hata kuziota.
2. Uzalendo
Nimeifanyia nchi kazi nyingi sana. Sio kwa maneno, ni kwa vitendo. Nimejitolea kwa Taifa hili wakati wewe ulikuwa bado unatafuta kiki. Uzalendo wangu umeandikwa kwenye historia, sio kwenye status.
3. Kipato
Kiasi cha pesa ninachoingiza, wewe hungeweza kukihesabu. Mimi siishi kwa mshahara wa mwezi. Mimi natengeneza pesa dunia nzima inapolala. Usiingie kwenye vita vya pesa na mimi, utashindwa vibaya.
4. Asset
Wewe unamiliki simu na nguo. Mimi namiliki Asset. Vitu vinavyoonekana, vinavyoweza kuhesabika, vinavyozalisha pesa hata nikiwa nimelala. Tofauti yetu ni kubwa sana.
5. Mikutano ya Kimataifa
Mimi nimeshakaa kwenye mikutano ya kimataifa na majarida makubwa barani Ulaya na Asia. Nimehojiwa, nimealikwa, nimeheshimiwa. Wewe bado unatafuta mwaliko wa kuingia kwenye ukumbi wa mtaani.
6. Utatuzi wa Migogoro
Nimeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa ndani ya nchi na nje ya nchi. Migogoro ambayo kama ingeachwa, nchi zingeungua. Wewe bado unashindwa kutatua hata ugomvi wa kwenu nyumbani.
7. Nchi Nilizotembea
Nimetembea nchi zaidi ya 100 duniani. Nimeona dunia. Nimeishi na tamaduni tofauti. Wewe unajilinganisha na mtu ambaye passport yake ina kurasa zimejaa mihuri ya dunia nzima?
8. Elimu Yangu
Course niliyoisoma na shule nilizosoma, sijui kama unaweza kufika hata kiwango hicho. Mimi sikusoma ili nipate cheti, nilisoma ili nitawale dunia. Elimu yangu ndiyo silaha yangu.
Kwa hiyo, nakukanya kwa heshima: Acha kujilinganisha na mimi.
Fanya kazi yako. Jenga jina lako. Kua wewe. Usijaribu kuwa mimi, kwa sababu huwezi.
Mimi ni BRITANICCA Mimi ni daraja moja, wewe bado uko chini unapanda ngazi.
Nimekwambia mara moja. Usirudie tena.
Britanicca