Rungwe88
JF-Expert Member
- Jul 12, 2013
- 605
- 1,523
Unazidi kuji expose jinsi ulivyo feki.Msalimie msh*** hapo N****
Huo unafiki wako watanzania wameshaujua
Unazidi kuji expose jinsi ulivyo feki.Msalimie msh*** hapo N****
Nawe hujazuiwa bwana Mdogo undeni timu yenu na yule jamaa yako uzuri ni Jukwaa huru dogoMzee ameamua kuvaa viatu vya Seikh Yahaya Hussein.
UMEANDIKA MAMBO YOTE YA KUTABIRIKA YA 2028-30.
Mimi sio muumini wa unabii na hizi Tabili za Tambitambi.
Kwaninibritanicca wewe na Pascal Mayalla ni ndugu?
Nimejiunga JF miaka mingi kabla yako, jitafakari kama unastahili kuniita dogo.Dogo Huna lolote ukiona unakuja kwenye uzi wangu means am threat to you! Ni chuki, na uzuri ni me kuignore sana kwenye nyuzi nyingi sana! We ndo unakuja kwenye nyuzi zangu na utakuja sana! Mpaka utaanzisha nyingine kusema ujinga but we mshamba tu
Dogo niko JF since 2007 au kwakiwa umeona account hii bado ikiwa Jambo forumNimejiunga JF miaka mingi kabla yako, jitafakari kama unastahili kuniita dogo.
Unadhihirisha jinsi ulivyo na uelewa mdogo wa mambo ya kawaida sana
Ulivyosema ni mwenzioKwanini
"Your level of understanding is disappointingly shallow, and your inability to see beyond your narrow perspective is quite obvious."Dogo niko JF since 2007 au kwakiwa umeona account hii bado ikiwa Jambo forum
Hao wote ni wana CCM mtandao kwa namna moja au nyingine.britanicca wewe na Pascal Mayalla ni ndugu?
Kwa namna unavyoonyesha, mbona hata mtoto wangu wa STD II kakuzidi akili, hivyo kubali tu kwamba wewe nikadogo.Nimejiunga JF miaka mingi kabla yako, jitafakari kama unastahili kuniita dogo.
Unadhihirisha jinsi ulivyo na uelewa mdogo wa mambo ya kawaida sana
Kwa kifupi niishie japa Kwa comment hii ni ya Mwisho kwako"Your level of understanding is disappointingly shallow, and your inability to see beyond your narrow perspective is quite obvious."
Ninyi vijana mmeshalewa pesa za ufisadi na mmeshakua vipofu sasa.Kwa namna unavyoonyesha, mbona hata mtoto wangu wa STD II kakuzidi akili, hivyo kubali tu kwamba wewe nikadogo.
Stupidity at the highest levelKwa kifupi niishie japa Kwa comment hii ni ya Mwisho kwako
Nisikilize vizuri, na nikwambie mara moja tu.
Usijilinganishe na mimi. Sio kwa dharau, ni kwa ukweli.
Unachokiona kwenye mitandao sio nusu ya nilivyo kihalisia. Mimi sio wa kuigiza, mimi ni wa vitendo.
1. Exposure
Wewe unajua mtaa wako tu. Mimi dunia imenijua kabla hata hujaijua. Nimekutana na watu wakubwa, nimekaa meza kubwa ambazo wewe huwezi hata kuziota.
2. Uzalendo
Nimeifanyia nchi kazi nyingi sana. Sio kwa maneno, ni kwa vitendo. Nimejitolea kwa Taifa hili wakati wewe ulikuwa bado unatafuta kiki. Uzalendo wangu umeandikwa kwenye historia, sio kwenye status.
3. Kipato
Kiasi cha pesa ninachoingiza, wewe hungeweza kukihesabu. Mimi siishi kwa mshahara wa mwezi. Mimi natengeneza pesa dunia nzima inapolala. Usiingie kwenye vita vya pesa na mimi, utashindwa vibaya.
4. Asset
Wewe unamiliki simu na nguo. Mimi namiliki Asset. Vitu vinavyoonekana, vinavyoweza kuhesabika, vinavyozalisha pesa hata nikiwa nimelala. Tofauti yetu ni kubwa sana.
5. Mikutano ya Kimataifa
Mimi nimeshakaa kwenye mikutano ya kimataifa na majarida makubwa barani Ulaya na Asia. Nimehojiwa, nimealikwa, nimeheshimiwa. Wewe bado unatafuta mwaliko wa kuingia kwenye ukumbi wa mtaani.
6. Utatuzi wa Migogoro
Nimeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa ndani ya nchi na nje ya nchi. Migogoro ambayo kama ingeachwa, nchi zingeungua. Wewe bado unashindwa kutatua hata ugomvi wa kwenu nyumbani.
7. Nchi Nilizotembea
Nimetembea nchi zaidi ya 100 duniani. Nimeona dunia. Nimeishi na tamaduni tofauti. Wewe unajilinganisha na mtu ambaye passport yake ina kurasa zimejaa mihuri ya dunia nzima?
8. Elimu Yangu
Course niliyoisoma na shule nilizosoma, sijui kama unaweza kufika hata kiwango hicho. Mimi sikusoma ili nipate cheti, nilisoma ili nitawale dunia. Elimu yangu ndiyo silaha yangu.
Kwa hiyo, nakukanya kwa heshima: Acha kujilinganisha na mimi.
Fanya kazi yako. Jenga jina lako. Kua wewe. Usijaribu kuwa mimi, kwa sababu huwezi.
Mimi ni BRITANICCA Mimi ni daraja moja, wewe bado uko chini unapanda ngazi.
Nimekwambia mara moja. Usirudie tena.
Britanicca
Haha hapana tumekuwa wote kwenye Jukwaa hili sema alinipa Kazi ya kumchunga shemeji yangu alipokuwa anasoma udaktari hapa urusiUlivyosema ni mwenzio
Nikawaza labda ni ndugu baba yenu ni mmoja si unajua watoto wanajua siri ya baba yao
Umesema unachojua na yeye anakijua
Hakika japo bado kazi ngumuHii inawezekana endapo CCM halisi itajinasua na kutoka kwenye mikono ya wahuni kwanza na kurudi wenye asili na misingi yake.
Vinginevyo mambo ni ya kihuni mwanzo mwisho, na hayo yatawaumiza hadi wahuni wenyewe.
Alafu AI imekutafsiria vibaya ukashindwa toa Funga semi na fungua semi 😁😁"Your level of understanding is disappointingly shallow, and your inability to see beyond your narrow perspective is quite obvious."
Uelewa wako ndio umeishia hapo?Alafu AI imekutafsiria vibaya ukashindwa toa Funga semi na fungua semi 😁😁
Unawezaje kupoteza muda wako kuandika uchafu wote huu? Ndiyo maana umaskini hauwatokiWooote wanaopiga jalamba na kujiset sasa hivi, hakuna hata mmoja atakayekuwa Rais wa nchi hii.
Ndio, nimesema hivyo. Na nitasimama hapo.
Wale wanaotumia pesa, wanaotumia nguvu, wanaotumia vyombo vya habari kujijenga kuwa ni wao ndio wajao, wote wanajidanganya. 2030 si 2025. 2030 si mwaka wa kawaida wa uchaguzi. 2030 ni mwaka wa kupasuka na kujengwa upya kwa Taifa.
Uchambuzi wangu uta-base sehemu 3: 1. Mwelekeo wa Siasa, 2. Madokezo Kadhaa Ndani ya Nchi, 3. Mkwamo Kisiasa.
Tuanze.
1. MWELEKEO WA KISIASA
Tukubaliane kwanza jambo moja la msingi: Rais ajae wala hajatajwa na yeyote.
Yule atakayekuwa Rais wa 2030, leo hii jina lake halipo midomoni mwa watu. Halipo kwenye magazeti. Halipo kwenye mitandao. Kama lipo, basi lipo kimya kimya, kwenye vikao vya ndani kabisa.
Wote wanaofanya maigizo sasa watapata shida. Shida kubwa. Hasa ajali kisiasa ndani ya Chama na ndani ya Serikali.
Kwanini? Kwa sababu siasa za kutafuta kwa nguvu, siasa za kujipendekeza, siasa za kutoa rushwa ili upendwe, siasa za kutumia vyombo vya dola kuwamaliza wenzako — zimechoka. Zimefika mwisho.
Naona kabisa, siasa za namna hiyo zikikoma mwaka 2028.
2028 utakuwa mwaka wenye mwanga kwenye Taifa la Tanzania. Mwaka ambao historia itaandikwa upya. Kwa sababu reforms nyingi zitafanyika. Reforms za kweli, sio za kwenye karatasi. Reforms zitakazosukuma CCM kuwa makini mara 100 zaidi na Mgombea watakayemteua.
CCM itajua: Kama tukikosea mgombea 2030, tumekwisha. Kama tukileta mtu wa jalamba, mtu wa kujiset, mtu asiyekubalika, tutapoteza nchi asubuhi na mapema.
Na hapa ndipo Turufu ilipo:
Kama reforms zikifanyika vema, na Upinzani wakajipanga vema, wanashinda asubuhi na mapema!
Sio usiku. Sio jioni. Asubuhi na mapema. Kwa sababu wananchi wamechoka. Wananchi wanataka mabadiliko ya kweli. Hawataki tena maneno matamu. Wanataka mtu wa vitendo.
Kwa hiyo 2028 ndio mwaka wa kuamua. 2028 ndio mwaka wa kuweka msingi. Yeyote atakayecheza vibaya 2028, 2030 hatakuwepo hata kwenye karatasi ya kupigia kura.
2. MADOKEZO KADHAA YA NDANI
Hapa ndipo penye siri kubwa.
Rais wa 2030 nishaambiwa ni nani.
Hata mwenzangu we Pascal Mayalla unamjua
Ndio, nimeshaambiwa. Na watu wa ndani kabisa. Lakini kutomuharibia, ngoja nisimtaje jina lake hapa. Kwa sababu kwa sifa alizo nazo, anamzidi tuliyenaye sasa mara 100.
Mara 100 kwa utulivu. Mara 100 kwa akili. Mara 100 kwa kukubalika. Mara 100 kwa kutokuwa na doa la rushwa.
Ni mtu ambaye hata adui zake wanamuheshimu. Ni mtu ambaye hahitaji kupiga kelele ili aonekane. Kazi yake inamzungumzia.
Lakini, asipokuwa yeye, basi huyu wa kizuizini ananyanyua ndoo mapema.
Ninazungumzia MKIZUIZI
MKIZUIZI ni jina ambalo haliwezi kufutika kwenye siasa za Tanzania. Unaweza kumfunga. Unaweza kumzuia. Unaweza kumweka kizuizini. Lakini huwezi kumfuta mioyoni mwa Watanzania.
MKIZUIZI akinyanyua ndoo mapema, mambo yatabadilika ghafla. Kwa sababu MKIZUIZI ana kitu ambacho wengine hawana: Sympathy ya Taifa.
Baada ya yote aliyopitia, baada ya kufukuzwa, baada ya kuwekwa kizuizini — Watanzania wanamwona kama shujaa. Wanamuona kama mtu aliyejitoa kwa ajili yao.
Na kama LISSU atagombea, basi Serikali ya Muungano wa Kitaifa haiwezi kuepukika.
Kifupi: Upinzani na CCM wanaweza kuungana kutengeneza serikali, hata kama KATIBA haisemi hivyo. Hata kama sheria haisemi hivyo.
Kwanini? Kwa sababu kutakuwa na Tragedy itakayotokea. Tragedy ambayo itawalazimu watu waketi mezani, na bandeji kichwani, kuandika makubaliano mapya ya Taifa. Sio kwa kupenda, bali kwa kulazimishwa na hali.
Watu wataulizana: Tunataka nchi iungue au tunataka tuketi tujadiliane?
Na hapo ndipo MKIZUIZI atakuwa muhimu. Kwa sababu ndani ya CCM wenyewe, yeye ni miongoni mwa Top 5 wanaokubalika bila rushwa wala sarakasi. Na anamkubali Lissu mbaya sanaaa
Ndiyo, umesikia vizuri. Hata ndani ya CCM, wapo wanaomkubali LISSU. Wapo wanaosema: Huyu mtu ni msafi. Huyu mtu ni mkweli. Huyu mtu hana unafiki.
Mbaya zaidi kwa wapinzani wake, sasa kaongezewa ka-sympathy ka kufukuzwa na kuwekwa kizuizini. Kila siku anapokuwa ndani, umaarufu wake unaongezeka nje. Kila siku anaponyamazishwa, sauti yake inasikika zaidi.
Kwanini MKIZUIZI atalazimika kugombea? Kwa sababu Taifa litamhitaji. Kwa sababu hakuna mwingine atakayeweza kuunganisha pande mbili zilizogawanyika. CCM itamhitaji ili iponyoke.
Na hapa ndipo jina la EMMANUEL NCHIMBI linaingia.
NCHIMBI ni mtu wa kimya kimya lakini ni mchezaji mkubwa sana ndani ya CCM. NCHIMBI anajua Chama ndani nje. NCHIMBI anajua Serikali ndani nje. NCHIMBI si mtu wa jalamba. NCHIMBI si mtu wa kujiset. NCHIMBI ni mtu wa mfumo.
Kama CCM itataka ku-survive 2030, itamlazimu imsikilize NCHIMBI. Kwa sababu NCHIMBI ndiye anayeweza kusema ukweli mchungu ndani ya Chama: Tukileta mtu mbovu, tumepoteza nchi.
NCHIMBI na LISSU, kwa namna moja au nyingine, ni majina mawili ambayo yatakuwa katikati ya meza ya 2030. Mmoja ndani ya mfumo, mwingine nje ya mfumo. Lakini wote wawili wanakubalika.
Kama NCHIMBI ataamua kusimama na ukweli, na LISSU ataamua kunyanyua ndoo basi mchezo unabadilika kabisa.
3. MKWAMO KISIASA
Sasa tuje kwenye sehemu ambayo watu wengi hawataki kuiongelea, lakini harufu yake inasikika.
Kuna harufu ya Jeshi kuja kushika nchi kutokana na mkwamo kisiasa.
Sio uvumi wa mtaani. Ni harufu ya kweli. Ndani si kuzuri. Hali ndani ni tete. Watu wamegawanyika. Viongozi wamegawanyika. Chama kimegawanyika. Nchi imegawanyika.
Kama mkwamo huu utaendelea, kama reforms zikicheleweshwa, kama 2028 ukipita bila suluhisho, basi mkwamo utafika kileleni baada ya 2030.
Na hapo ndipo Jeshi linaweza kujaribu kuingia.
Lakini nikuambie ukweli mchungu:
Wakijichanganya Jeshi si zuri kushika nchi.
Kwanini? Kwa sababu wao uwa wakishashika hawatoki. Wanakuwa na kamchezo ka kupinduana!
Leo huyu anampindua huyu, kesho huyu anampindua huyu. Nchi inakuwa uwanja wa kupinduana. Maendeleo yanasimama. Demokrasia inakufa. Na mwisho, wananchi ndio wanaumia.
Jeshi lina kazi yake: Kulinda mipaka, kulinda Taifa dhidi ya adui wa nje. Sio kushika madaraka. Kama Jeshi likishika madaraka, halitoki kirahisi. Na historia ya Afrika inatuambia hivyo wazi wazi.
Kwa hiyo, suluhisho sio Jeshi. Suluhisho ni MEZANI.Suluhisho ni mazungumzo. Suluhisho ni Serikali ya Muungano wa Kitaifa ambayo itazaliwa baada ya tragedy, kabla Jeshi halijajaribu kuingia.
Tunapaswa kuzuia Jeshi kuingia kwa kufanya reforms mapema. Kwa kuleta mgombea sahihi. Kwa kumruhusu LISSU na wengine kushiriki kwa haki. Kwa kumsikiliza NCHIMBI na wengine wanaosema ukweli ndani ya CCM.
Kama tukifanya hivyo, Jeshi litabaki barracks. Kama tukikataa, Jeshi litatoka barracks.
NA NDEJA?
Hapa lazima niongee na moyo mzito.
NDEJA anaweza kama Mungu atafanya jambo kabla ya 2030.
Jambo ambalo hatutaki. Jambo ambalo ninaliona, lakini ninaomba lisitokee.
Kama jambo hilo likitokea, basi hesabu zote za 2030 zitabadilika ghafla. Mchezo wote utabadilika. Majina yote ya sasa yatapotea. Na Taifa litaingia kwenye kipindi kigumu sana cha maombolezo na sintofahamu.
Sitamani. Siombe. Lakini naliona. Na ndio maana ninasema: Tusifanye mzaha na 2030. Tujipange mapema. Tumwombe Mungu atulinde.
HITIMISHO
Kwa hiyo, nirudie tena:
Wote wanaopiga jalamba na kujiset sasa, hakuna atakayekuwa Rais.
Rais wa 2030 ni mtu mwingine kabisa. Mtu ambaye hajatajwa. Au kama sio yeye, ni LISSU.
Na kama ni LISSU, basi Serikali ya Muungano wa Kitaifa haiwezi kuepukika.
Na kama tukikataa kuungana, basi mkwamo utaleta harufu ya Jeshi.
Chaguo ni letu. 2028 ndio mwaka wa kuamua. 2030 ndio mwaka wa kulipa.
Watu wanauchukulia 2030 powa powa. Lakini 2030 ndio mwaka utakaoamua kama Tanzania inabaki kuwa Tanzania, au inakuwa kitu kingine kabisa.
Mwisho: KATIBA MPYA NA REFORMS NI MUHIMU
Britanicca