Mhhh.. taratibu bandugu hamkawii kuitwa wachochezi mnao tishia amani ya nchi!
Hapa si Amani ya nchi ni amani ya MAFISADI nchi itapata amani ya kweli mpaka pale watu watakakuwa wanalala milango wazi, hawaweki walinzi, hawaweki magrili milangoni, Laptop zikiachwa kwenye gari vioo havivunjwi na kuibiwa, Watu wanatembea usiku bila woga, Watu wanakula wanachokitaka, wanadrive magari wanayoyapenda. Hii ndio Amani ya kweli ambayo haipaswi kutishiwa kama itapatikana.
Je Amani hii itapatikana vipi?, Ni pale tutakapowatoa mafisadi na kuhakikisha nchi yetu inatumia rasilimali zetu kwa manufaa ya wananchi wote badala ya kikundi cha watu wachache, Ili kukuza uchumi wetu, watu wapatiwe ajira zinazolipa vizuri, Hakutakuwa na mtu mwenye mawazo ya kuvizia cha mtu kwani tayari ana ajira yake halali. Tukifika hapa yeyote atakeye sema tutumie jeshi kuwaondoa viongozi itabidi adhibitiwe kwa laana zote za wananchi