Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,958
- 718
Rais wa Maurtania Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi amepinduliwa. Kwa mujibu wa habari za kuaminika ni kwamba kikosi maalumu wa kumlinda Rais (Presidental Security Batallion) kilifika nyumbani kwa Rais huyo na kumuweka chini ya ulinzi kisha kuondoka naye. Habari hizo zilithibitishwa na binti wa Rais huyo aitwaye Amal Mint Cheikh Abdallahi.
Mapinduzi haya ya kijeshi yametokea baada ya Rais kumfukuza Mkuu wa Majeshi General Mohamed Ould Cheikh Mohamed Ahmed Ghazouani na Mkuu wa kikosi maalumu cha kumlinda Rais, Mohamed Ould Abdelaziz.
Habari hizo vilevile zimedai kuwa wengine ambao wako chini ya ulinzi ni Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo. Mapinduzi hayo yametokea bila umwagaji damu.
Rais JK ana shughuli nzito akiwa kama Mwenyekiti wa AU. Sasa sijui kama litatumwa jeshi huko kama Comoro au watatumia Demokrasia.