Huyo anaitwa Edgar Rinkevics, ametumikia muda mrefu (tangu 2011) kama waziri wa mambo ya nje wa Latvia huko Ulaya Mashariki.
Umoja wa Ulaya umewahi kuwa na viongozi mashoga wa serikali lakini sio kiongozi mkuu wa serikali hadi Edgar anachaguliwa.
Tangu mwaka 2014 bwana Rinkevics mwenye umri wa miaka 49 amekuwa mtetezi mkubwa wa mashoga na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Ndoa za jinsia moja Latvia ni haramu pamoja na kwamba Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo imeruhusu ndoa hizo tangu mwaka jana.
Mwezi Mei mwaka huu bunge la Latvia lilimchagua Rinkevics kuwa rais. Katika hotuba yake ya ufunguzi, bwana Rinkevics ameahidi kujenga Latvia ya kisasa yenye nguvu, na yenye kufuata sheria na haki kwa ajili ya faida ya watu wote.