Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
"Mhe. Rais SuluhuSamia tunakushukuru sana kwa uongozi wako bora uliojaa utu utawala bora, malengo mema na bora kabisa ya kujenga maridhiano na kuleta maridhiano ya mifumo, sera na sheria na kutekeleza mipango yakujenga Taifa letu kuwa bora na imara kiuchumi na kijamii.
"Tanganyika Law Society tunatambua juhudi zako kubwa za kuwakaribisha wadau wa maendeleo nchini kuvutia mitaji na wawekezaji pamoja na kuongeza fursa za ajira, kuimarisha huduma za jamii hususan elimu, afya, maji na kwa kweli ni vigumu kwa muda huu mfupi kutaja mambo haya makubwa Mhe. Rais umeyafanya kwetu kwa kipindi hiki kifupi.
Tunaamini kwamba kwa mwendo huu uchumi wetu wa Taifa na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja bila shaka utaendelea kuwa bora zaidi Tunakushukuru sana Mhe. Rais."
Wakili Harlod Sungusia, Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika akizungumza jana Ikulu ya Chamwino baada ya uongozi wa chama hicho kukutana na Rais Samia.
Jambo TV
Pia soma - Rais Samia amkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Hati ya Kiwanja