Rais TLS: Uongozi wa Rais Samia umejaa Utu na Utawala Bora

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Screenshot 2023-08-15 161354.png

"Mhe. Rais SuluhuSamia tunakushukuru sana kwa uongozi wako bora uliojaa utu utawala bora, malengo mema na bora kabisa ya kujenga maridhiano na kuleta maridhiano ya mifumo, sera na sheria na kutekeleza mipango yakujenga Taifa letu kuwa bora na imara kiuchumi na kijamii.

"Tanganyika Law Society tunatambua juhudi zako kubwa za kuwakaribisha wadau wa maendeleo nchini kuvutia mitaji na wawekezaji pamoja na kuongeza fursa za ajira, kuimarisha huduma za jamii hususan elimu, afya, maji na kwa kweli ni vigumu kwa muda huu mfupi kutaja mambo haya makubwa Mhe. Rais umeyafanya kwetu kwa kipindi hiki kifupi.

Tunaamini kwamba kwa mwendo huu uchumi wetu wa Taifa na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja bila shaka utaendelea kuwa bora zaidi Tunakushukuru sana Mhe. Rais."

Wakili Harlod Sungusia, Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika akizungumza jana Ikulu ya Chamwino baada ya uongozi wa chama hicho kukutana na Rais Samia.

Jambo TV

Pia soma - Rais Samia amkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Hati ya Kiwanja
 
Haw TLS waliundaga kamati ya kufanya review ya mkataba wa bandari. Tutarajie majibu ya kamati yatakayomfurahisha bi hangaya
 
Asisahau hata Dr. Slaa alilamba uteuzi ila leo yuko behind bars. Hivyo, na yeye aendelee kusaka uteuzi akiamini atakuwa amepata shavu.
 
Tumekwisha rushwa hutia upofu. Hongereni kwa kuhongwa kiwanja, kisha kuunga mkono kuuzwa kwa bandari. Ila mungu ni mkali mnooo. Pia anawackiliza wa tanganyika.
Asante
 
"Mhe. Rais SuluhuSamia tunakushukuru sana kwa uongozi wako bora uliojaa utu utawala bora, malengo mema na bora kabisa ya kujenga maridhiano na kuleta maridhiano ya mifumo, sera na sheria na kutekeleza mipango yakujenga Taifa letu kuwa bora na imara kiuchumi na kijamii.

"Tanganyika Law Society tunatambua juhudi zako kubwa za kuwakaribisha wadau wa maendeleo nchini kuvutia mitaji na wawekezaji pamoja na kuongeza fursa za ajira, kuimarisha huduma za jamii hususan elimu, afya, maji na kwa kweli ni vigumu kwa muda huu mfupi kutaja mambo haya makubwa Mhe. Rais umeyafanya kwetu kwa kipindi hiki kifupi.

Tunaamini kwamba kwa mwendo huu uchumi wetu wa Taifa na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja bila shaka utaendelea kuwa bora zaidi Tunakushukuru sana Mhe. Rais."

Wakili Harlod Sungusia, Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika akizungumza jana Ikulu ya Chamwino baada ya uongozi wa chama hicho kukutana na Rais Samia.

Jambo TV

Pia soma - Rais Samia amkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Hati ya Kiwanja
Matope tu

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
Hivi hawa kwa nini huwa wanaitwa Wakili Msomi. Mbona kauli na matendo haviendani na jina hilo?
Kwani we unataka kusikia unachokitaka tu? Sikia na usivyovitaka ili uishi vizuri mtu wangu. The world's systems are already set you cant change anything.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom