Rais Sata wa Zambia ateua Baraza la Mawaziri.

Jamani huyo mzungu ni mwanaharakati wa kweli na ningeshangaa sana kama angemuacha kwenye safu yake ya uongozi, wametoka naye mbali sana-kwenye shida na karaha zote.Acha amsaidie kazi King Cobra!

uanaharaka wake ni kudai mambo gani pale ZAMBIA
 
Hiyo ni kwa manufaa ya taifa, kwa walio wengi.
Ushindani wa vyama umeisha na uchaguzi sasa ni kufanya kazi kwa ajili ya wazambia wote, hivyo wanaotafutwa ni watendaji wanaoweza kuisadia serikari kuhudumia wananchi wake. Hapa kwetu vyeo ni kama peremende vinagawiwa kishikaji kwa marafiki, watoto wao hata magirlf wao.
Huyu aweza akavaa viatu vya Mandela.
 
Natamani ningezaliwa Zambia, Kila la kheri Dr.Sata.
Umetuonesha njia.
 
Hapa kigezo ni kudeliver na sio ukilemba.
wewe bado ni kalaza nasisitiza
Kati ya mimi na wewe kwa huo mtizamo nani anaonekana kilaza?
Unamaanisha kuwa Zambia nzima hamna mtu anayeweza kudeliver zaidi ya huyu mzungu?
Nyie ndio watu msiojiamini, mnawahusudu wazungu, mnaona wao ni kila ktu
 
hapo nakubaliana na wewe, ingawa inatakiwa tumujue huyu mzungu UZAMBIA WAKE uko vipi
tayari mtoa mada katubainisha.....
"Guy Scott mwenye asili ya Uingereza wa chama chake cha Patriotic Front (PF)."
 
Kweli sata kichwa jamaa ana bifu wamempinga na kawapa uwaziri so! Kacheki uwezo wa mtu si chama chake bravo sata kikazi zaidi.. But jamaa ukipiga nyumba ndogo 2 kazi unayo ukitoka jera pipi inauzwa laki moja!! Sasa itakuwa kumpa uwaziri mpinzani.somo kubwa sana kwa magamba.
 
Mzungu ni mtu yoyote ambaye asili yake ni "caucasian", haijalishi Mzungu kazaliwa wapi, ataendelea kuwa mzungu tu!,
hata hivyo haijalishi mzungu hawezi kuwa Mtanzania, mzambia, mmarekani! n.k.

kiufupi kwa lugha isiyo rasmi mzungu ni "white man".
 
Kati ya mimi na wewe kwa huo mtizamo nani anaonekana kilaza?
Unamaanisha kuwa Zambia nzima hamna mtu anayeweza kudeliver zaidi ya huyu mzungu?wewe
Nyie ndio watu msiojiamini, mnawahusudu wazungu, mnaona wao ni kila ktu
Wewe ni mpuzi sana mbinafsi mbna south wanamawaziri wazungu na wanamaendeleo obama si black mbna rais kama hamna hoja si mtulie
 
Vyovyote iwavyo na itakavokuwa,huyu Sata anaonekana ni kweli presidential material.Nadhani pia wazambia na demokrasia yao ni ya kweli na hawana unafiki.They are hudred miles awayfrom othr African countries even beyond.
 
Wewe ni mpuzi sana mbinafsi mbna south wanamawaziri wazungu na wanamaendeleo obama si black mbna rais kama hamna hoja si mtulie

South Africa si Zambia. Wazambia waliwafukuza wazungu baada ya uhuru lakini wazungu wa South Africa hawakufukuzwa kwa kuwa kwao ni South Africa.
 
wazungu ni wetu walituletea shanga za kuvaa kule kwetu ni kamba za kufungia ng'ombe na..........na sasa wametuletea demokrasia ya kuwavuruga waafrica ili waweze kututawala vizuri ,,,,demokrasia bila elimu wapi wapi,,ili watu wawe na demokrasia lazima waeelimika vizuri ili kutambua mbivu na mbichi..sasa wazungu watapiga makofi kwa wingi kwa sata.......
 
Big Up for President Sata and VP Dr. Guy. Serious leaders think out of box and beyond. Hata Tz tulikuwa na kina Amir Jamal, Derick Bryceson. Huyu kaanzia harakati za kuleta democrasy kwenye nyumba kumi zao na ni Mzambia anastahili.

Uko sahihi kabisa, Mfano Alnoor Kassum pamoja na kuwa alikuwa mtanzania mwenye asili ya kihindi alifanya vitu vingi, vikubwa na vizuri kwenye nishati na madini kuliko waziri wa wizara wa sasa mmatumbi mwenzetu ambaye ni msanii wa kutupwa. Jamal amiri mtanzania mwenye asili ya kihindi alifanya kazi kubwa sana kwenye viwanda na Biashara na baadaye fedha kuliko hawa wa sasa wabantu ambao wamefocus kuuza viwanda mpaka inafikia wakati nchi yenye rasilimali kama yetu inajivunia kiwanda cha bia, konyagi na sigara tu.

Dereck Bryson,mtanzania mwenye asili ya ulaya alikuwa waziri wa afya wa kweli na wa vitendo sio hawa wa sasa wa kwa hisani ya watu wa marekani na kutokomeza malaria kwa kupiga muziki leaders club.

Uzambia, utanzania sio rangi ya mtu bali ni uzalendo na kujitoa kwa kila jinsi kwa faida ya nchi yako
 
Umewasahau akina Andrew Young, Condolezza Rice na General Powell.
Kwa watu wanaojali maendeleo, wanachagua watu kwa ajili ya utendaji wao na wala si rangi, dini, kabila wala asili zao, vitu ambavyo TZ vinatutafuna na vitaendelea.

Wakitaka kuchagua mawaziri ramani ya tanzania lazima iwepo the reason is kila mkoa utoe angalau waziri au naibu, kigezo kimekua maeneo ya kiutawala mikoa na wilaya kuliko uwezo wa mtu. Ndio maana miaka 50 baada ya uhuru nchi afadhali ya jana
 
Back
Top Bottom