Rais Sata wa Zambia ateua Baraza la Mawaziri.

watu wamezaliwa na busara na hekima zao... Tz kupata watu kama hao bado sana!
 
Ni mfano wa kuigwa.
images

Mr. Guy Scott ameula..
 
Atawasaidia nini WaZambia kwa UMRI ule? Mpeni Mzee Malecela Urais mwaka 2015.

Hao wadogo kwake wametusaidia nini mpaka sasa zaidi ya kutuletea majanga kila siku? Sidhani kama issue ya umri ina weight kubwa kwenye urais as long as still yuko mentally ok. Niseme kama alivyosema Mrema, urais si kunyanyua vyuma, uzuri wa sura (tuliliwa hapa maskini TZ) au kupigana ngumi bali ni mapenzi na nia ya dhati ya kutaka kuitumikia nchi ni si marafiki, vimada, familia, wanamtandao na wengine kama hao. Kama nakumbuka vizuri Mandela alikuwa mkubwa kwa Sata au same age alipochaguliwa kuwa rais na alideliver poa tu.
 
Mbunge wa mmd jimbo la Chongwe katika Lusaka province huko Zambia amejiuzulu. Akitoa sababu za kujiuzulu, alisema wananchi wa Chongwe hawamtaki. Alipoulizwa alishindaje ikiwa wapiga kura wake hawamtaki, alijibu kwamba hata yeye mwenyewe hajui.
Ukweli wa mambo ni kwamba Rais aliyeng'olewa madarakani Banda alikuwa amemhakikishia mgombea wa chama cha Sata ambae ni mwanamke Silvia Masebo kuwa hatapewa jimbo kwa namna yoyote ile. Hii ni kwa sababu mwanamke huyu alikuwa amekihama chama cha MMD na kujiunga na upinzani, huku akiwa ni waziri katika serikali ya Banda. Zambia ni nchi ya kikristo na raia wake ni watu wanaopenda haki, hivyo imepelekea yule aliyetangazwa mshindi bila kushinda katika sanduku la kura kuukataa huo ubunge, na badala yake amedai anataka kuishi na familia yake kwa furaha na amani.
.
 
hapo kwenye red ni 'shubiri' kuliongelea hapa TZ lakini ina kaulweli fulani. Mambo ya "Ideology" yana mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii yoyote unless kuamua kuishi kama (mfano) China ni bora
Mbunge wa mmd jimbo la Chongwe katika Lusaka province huko Zambia amejiuzulu. Akitoa sababu za kujiuzulu, alisema wananchi wa Chongwe hawamtaki. Alipoulizwa alishindaje ikiwa wapiga kura wake hawamtaki, alijibu kwamba hata yeye mwenyewe hajui.
Ukweli wa mambo ni kwamba Rais aliyeng'olewa madarakani Banda alikuwa amemhakikishia mgombea wa chama cha Sata ambae ni mwanamke Silvia Masebo kuwa hatapewa jimbo kwa namna yoyote ile. Hii ni kwa sababu mwanamke huyu alikuwa amekihama chama cha MMD na kujiunga na upinzani, huku akiwa ni waziri katika serikali ya Banda. Zambia ni nchi ya kikristo na raia wake ni watu wanaopenda haki, hivyo imepelekea yule aliyetangazwa mshindi bila kushinda katika sanduku la kura kuukataa huo ubunge, na badala yake amedai anataka kuishi na familia yake kwa furaha na amani.
.
 
Mi nafikiri huyo mheshimiwa yuko sahihi kwani nafsi yake ina msuta...unajua viongozi wa kiafriaka wanajiona kuwa wao ndiyo wanahaki ya kutawala hapa AFRICA
 
Wakitaka kuchagua mawaziri ramani ya tanzania lazima iwepo the reason is kila mkoa utoe angalau waziri au naibu, kigezo kimekua maeneo ya kiutawala mikoa na wilaya kuliko uwezo wa mtu. Ndio maana miaka 50 baada ya uhuru nchi afadhali ya jana
Uko sahihi Mkuu!. Mara zote huwa ninajiuliza kwa nini TZ (mfano tu miongoni mwa nchi za Afrika) na umasikini wake inakuwa na mawazir 60 wakati nchi zilizoendelea daima hawazidi 20. Sababu ni hizo: ukanda, ukabila, undugu, urafiki, ulipaji fadhila n.k.

Mada tafauti lakini ina uhusiano: juzi juzi tu tulikuwa na mjadala kufuatia tukio la JK kuunda mikoa na wilaya mpya, nikalinganisha na Italy (one among the 8 most rich) ilipunguza mikoa, wilaya, na mabaraza ya miji. Wakati matajiri wanapunguza matumizi na kukaza mikanda, sisi tunaongeza matumizi na tusivyoona haya, bajeti zetu mpaka tupitishe kopo kwao.

TANZANIA INAELEKEA WAPI!!!!!!
 
TANZANIA INAELEKEA WAPI!!!!!!

Unachosema ni kweli kabisa, nchi iliyo kwenye autopilot, macrew wanakunywa whisky na mvinyo, abaria wako busy wanaangalia the comedy lazima nchi ita crashland: hamna jinsi.
Halafu nacheka hao watanzania wanaoongoza nchi wako busy kusherehekea miaka 50 ya uhuru huu ni mwezi wa tatu toka sherehe zimeanza.
Najiuliza is it worth doing so??????
Napata jibu kuwa hakuna uzalendo ni unafiki tu
 
Hapo mmekutana wote wadini. Wewe pamoja na yule unayemkosoa mko kapu moja.

kweli kabisa,sijui kwanini baadhi ya watu humu JF wanapenda udini udini sielewi wanafaidika na nini.mambo ya ajabu sana haya.anyway Sata ameonesha mwelekeo mzuri!
 
Ni mfano wa kuigwa.
images

Mr. Guy Scott ameula..

Miaka hamsini baada ya kuwafukuza kwa mbwembwe leo hii tunawarudisha kwa mbwembwe tena!! Ama kweli hii ndio Africa. Tumepitia Ukoloni Mkongwe, Ubeberu, Uhuru wa Bendera, Ukoloni Mamboleo na sasa tunarudi kwenye ukoloni mkongwe wa kutawaliwa na wazungu. Ina maana Waafrica tumeshindwa kabisa kujitawala kabisa kabisa!!
 
Color is not an issue so long is living on leadership ethics!

Kuna siku tutasema uhuru hauna maana kwa kuwa tuliwafukuza wazungu who were living on ledership ethics and put in place our own sisters and brothers who have proved to be unethical!!
 
Miaka hamsini baada ya kuwafukuza kwa mbwembwe leo hii tunawarudisha kwa mbwembwe tena!! Ama kweli hii ndio Africa. Tumepitia Ukoloni Mkongwe, Ubeberu, Uhuru wa Bendera, Ukoloni Mamboleo na sasa tunarudi kwenye ukoloni mkongwe wa kutawaliwa na wazungu. Ina maana Waafrica tumeshindwa kabisa kujitawala kabisa kabisa!!

.
Hata kule Marekani sisi waafrika kupitia Obama tunawatawala wazungu. Tena ukizingatia kuwa hili ni taifa kubwa duniani, inamaanisha mwafrika anatawala dunia.
.
 
Jamani mi naona mjadala unakoelekea siko tumeanza kujadili rangi , dini sijui tunakoelekea ni wapi!
Cha msingi wazambia wamemashapata kiongozi wao kila la kheri, awe fisadi awe nani ni maamuzi yao watajua wenyewe. Swala ni sisi tumejifunza nini?
Raisi wetu umeona mfano huo hujachelewa kufanya maamuzi, unaweza kusema basi tutakuunga mkono vunja baraza la mawaziri unda jipya watupilie mbali miwaziri mizigo, weka yeyote hata mpiga debe lakini awe mchapa kazi mwenye uchngu na nchi bado nina imani na ww.

Mungu mjalie Raisi wetu mpe ujasiri wa kufanya maamuzi ili aliokoe taifa letu linaloangamia
 
MODs kumbe hata nyinyi tu hapo mnamuogopa Sata na mabadiliko ya amani Zambia kiasi cha kuficha uzi wake kiasi hiki????????????????????????
 
Back
Top Bottom