Rais Sata wa Zambia ateua Baraza la Mawaziri.

Aliyechagua kichwa cha habari ana mawazo mgando. Scott ni Mzambia kama alivyoelezewa. Wanaoangalia rangi ya mtu inabidi tuwakumbushe labda walizaliwa juzi. Tanzania na viongozi wetu mpaka kushika nyadhifa za uwaziri. Amil Jamali. Alnoor Kasam. Julie Manning. Dereck Bryson. Dr Stirling achilia mbali Wabunge kibao kama marehemu Msukuma Biku Mohamedi Biku. Kama tutaangalia rangi na kadhalika, iko siku tutasema Tanzania imepata Raisi ******, Msubi, Mvidunda, Mmachame, Mmbulu na kadhalika. Acheni unywanywa.
 
Anayesema Afrika ni bara la watu weusi ninamwomba anielimishe labda mimi sijui historia. Misri, Tunisia, Libya, Sudan, Moroco, Algeria ziko bara gani na walioko huko, raia wa sasa walifikaje huko na walitokea wapi?
 
Anayesema Afrika ni bara la watu weusi ninamwomba anielimishe labda mimi sijui historia. Misri, Tunisia, Libya, Sudan, Moroco, Algeria ziko bara gani na walioko huko, raia wa sasa walifikaje huko na walitokea wapi?

wananchi wa hizo nchi ulizotaja wenyewe hawajichulii kama ni wa Africa
 
I salute Zambians kwa kumchagua SATA na hatiame nae kuchagua mawaziri mchanganyiko!
Tz kuna cha kujifunza apo tena sio mbali ni majirani zetu tuu apa apa Africa
 
Kama kweli kitendo cha mzungu kupewa umakamu wa raisi katika nchi ya kiafrika ni tatizo basi ungemlaumu Sata kwa kuwa na akili ya kikoloni.Lakini badala yake kutokana na mgando wa chuki za kidini katika akili yako unalaumu kuchaguliwa dkt Shein na Mohammed Gharib Bilal kuwa makamo wa raisi Tanzania.Umesahau kuwa wakatoliki kama Sata waliwahi kushika nafasi hii na haikuwa lolote la maana mbali na njaa kali.
Hapo mmekutana wote wadini. Wewe pamoja na yule unayemkosoa mko kapu moja.
 
kwa mara ya kwanza Africa tangu tupate uhuru mzungu ameteuliwa kuwa makam wa rais
hiyo ni dalili tosha kuwa Rais Sata yuko serious kuibadilisha zambia na mifumo yote mibovu
vile vile ameteua wanachama wa vyama vingine kuunda serikali jambo ambalo hapa kwetu ni ndoto ya mchana
kitendo cha mzungu kuwa makamu wa rais kinaonyesha jinsi wenzetu walivyokomaa na walivyo na elimu kubwa ukilinganisha
na sisi watanzania tunavyohangaika na makamu wa marais wetu wanaopenda sana vibaghashia vya bakwata kushika hiyo nafasi

Zambia has white vice president, as Sata creates another ministry | Zambian Watchdog

Umeanza vizuri ile mbaya hiyo thread yako ingawa ukaja kuharibu hapo kwenye red; cjui unawakilisha ujumbe gani hapo mwana kwetu!!!
 
So, what about Bashe, Rage,Rostam....
Julie manning, Amir Jamal, Alnoor Kassum....
Stop racism,tribalism,provincialism
 
Huyu ni mzambia na wala sio mzungu, amezaliwa zambia, kakulia zambia, kasoma zambia kaanzia kazi zambia. Rangi yake nyeupe isimfanye aonekane ni mzungu huyu ni mzambia halisi kama inavyoonekana kwenye historia yake.

Ni mzungu ambae ni raia wa Zambia.

Kukulia sehemu, kuzaliwa sehemu flani haibadilishi mbegu/race ya mtu.
 
jamaa ni innovative na siasa kwake si kazi ya kutegemea.kama tunavyoona amejishughulisha na kilimo muda mwingi
 
Umeanza vizuri ile mbaya hiyo thread yako ingawa ukaja kuharibu hapo kwenye red; cjui unawakilisha ujumbe gani hapo mwana kwetu!!!

thibitisha kama siko sawa kwenye kumaliza
mimi tangu nimekua naona makamu wa marais wote wanavaa vibaghashia,yaani ni waislam
 
Well done Zambs! hii issue ni necessary but mmhh! NOT sufficient na tumeona hao wanyama wakuja wanaua kabisa!! Ref RA and the gang of death!
 
Well done Zambs! hii issue ni necessary but mmhh! NOT sufficient na tumeona hao wanyama wakuja wanaua kabisa!! Ref RA and the gang of death!

ni hatua nzuri kwa sababu hawakuangalia rangi,nafikiri angekuwa muhindi au mwarabu asingepewa
 
Nnilikuwa na matumaini na huyu ndugu Sata lakini taratibu naanza kuondoa shilingi yangu. Binafsi I don't buy the idea ya kujipendekeza kwa ze mzunguz, trust me, few of them they might look nice but overall they won't consider us as equal..na hii si kwa wazungu tu, bali mwarabu, mhindi, mchina n.k, mnawababaikia tu lakini wenzenu wanacheki tu kwene saiti-mira huku wakisema kimoyomoyo..'bich ass niga'
 
wabongo tumekuwa wabaguzi sana,kila kitu ni mpaka tuseme,kuna jamaa wa amechguliwa kuwa mkurugenzi utalii kama sikusei tumemsema kutokana na rangi yake
yaani watu kama kina mwisho mwampamba wenye rangi nyeupe wasije shika madaraka nchi hii,tunasema sana pasipo kuangalia uhalisia

SAFIIIII sana ZAMBIA acha kuiga wabongo mungu azidi kutupa upumbavu huu wa kubaguana kwa Rangi
mkuu safi sana,tusiwe tunaangalia rangi tuangalie anafanya kazi vp.bongo tunalo hii shida sio nasema tuwape wazungu nafasi,ninacho sema wote ni sawa na na apewe mtu kwa uaminifu,uhodari,mvumilivu,mwenye subira na mjanja.
 
Je mtu mweusi anaweza kuwa makamu wa rais au rais usa au wazir mkuu uk,kwa vile tu amezaliwa huko?don't tell me about obama(half cast)mi naungana na bob mugabe kwamba africa ni bara la mtu mweusi hao jamaa wana kwao.kwetu ni kwao kwa nini?(kandoro saadan)
Umewasahau akina Andrew Young, Condolezza Rice na General Powell.
Kwa watu wanaojali maendeleo, wanachagua watu kwa ajili ya utendaji wao na wala si rangi, dini, kabila wala asili zao, vitu ambavyo TZ vinatutafuna na vitaendelea.
 
sata michael.jpg

Rais wa Zambia Michael Sata


RAIS wa Zambia Michael Sata, ametangaza Baraza lake la Mawaziri linalowajumuisha wabunge sita wa chama cha MMD kilichokuwa kikiongozwa na mpinzani wake, Rupiah Banda, huku akimpa umakamu wa rais Guy Scott mwenye asili ya Uingereza wa chama chake cha Patriotic Front (PF). Jana Sata alitangaza baraza hilo jipya la mawaziri lenye wizara 19 tu kutoka 22 zililokuwapo hiyo na kusema: “Hawa ndio watakaonisaidia kuongoza”. Rais Sata alimteua pia msaidizi wake maalum wa mahusiano na vyombo vya habari, George Chella.

Septemba 23 mwaka huu, Zambia iliandika historia mpya katika mfumo wa utawala wake, kufuatia kiongozi huyo wa upinzani kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini humo. Sata (74), ambaye pia anajulikana kwa jina maarufu la “King Cobra” alitangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo dhidi ya rais aliyekuwa madarakani, Rupiah Banda wa MMD. Mgombea huyo wa upinzani ambaye aligombea nafasi hiyo mara tatu na kushindwa, safari hii alipata kura 1,150,045, sawa na asilimia 43, wakati Banda aliambulia kura 961,796, sawa na asilimia 36.1. Idadi ya watu waliojiandikisha ni 5.2 milioni.


Sata anakuwa rais wa tano kuiongoza nchi hiyo ambayo ilijinyakulia uhuru wake mwaka 1964 kutoka Uingereza kwa kuking’oa madarakani chama cha MMD kilichokaa madarakani kwa miaka 20.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom