“Harufu ya ufisadi SGR kipande cha 6 Tabora-Kigoma”

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
Dec 20, 2022 serikali ilisaini mkataba wa ujenzi wa SGR Tabora-Kigoma kilometa 506km. $2.7bn (Sh6.34 trilioni) na ujenzi huu unatarajiwa kuchukua miezi 48. Kwa kusaini kipande hiki, Serikali itakuwa imewekeza $10.04bn (Sh23.3 trilioni) kwa awamu ya Dar-Mwanza na Tabora-Kigoma.

Waziri wa fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, hotuba ya bajeti ya serikali, uk.44, alisema serikali imeanza mchakato wa kutafuta mkandarasi wa kujenga kipande cha SGR (Tabora-Kigoma) 514km kwa $2.1 bilioni (Sh4.89 trillioni).

Tulifahamu kabla ya kusaini mkataba huo hadharani, walikuwa tayari wamewapa kandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) kwa utaratibu wa manunuzi wa zabuni zisizoshindanishwa (single source) tangu mwezi June 2022

Hapa ipo tofauti. Hotuba ya Mwigulu ya bajeti alisema ni 514km, lakini Shirika la Reli Tanzania (TRC) wamesaini mkataba wa kujenga 506km. Kuna pungufu ya 8km. Mwigulu alisema ujenzi utagharimu Sh4.89 trilioni lakini mkataba umesainiwa Sh6.34 trilioni. Ongezeko la Sh1.45 trilioni.

Mkurugenzi Mkuu (TRC), Masanja Kadogosa amesema Mikataba haitakuwa na mabadiliko ya bei, ikijumuisha vitu vya ujenzi, hivyo ongezeko la $1.304bn (30.3%, kwa maana ya thamani ya fedha) HALIPO. Ongezeko la Sh1.45 trilioni kwenye bajeti kuu ya serikali na mkataba imetoka wapi?

Katika mfumo wa TANePS (Tanzanian National e-Procurement System), Mkandarasi CCECC alipewa zabuni ya ujenzi wa SGR Tabora-Kigoma kwa Sh6.69T. Tofauti ya bajeti ya Mwigulu na TANePS ni Sh1.85T. Tofauti ya bajeti ya Mwigulu na mkataba (TRC na CCECC) ni Sh1.45T. Lipo TATIZO.

Mwigulu Nchemba wakati akisoma bajeti kuu ya serikali 2022/2023 alisema “serikali imeanza mchakato” wakati ukweli ni kwamba Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alikuwa tayari amepewa zabuni tangu 04.04.2022 kwa utaratibu wa ‘single source’.

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) alipewa hii zabuni kwa utaratibu wa bila ushindani (single source) ambayo ilidumu TANePS kwa dakika 30, yenye BID ID 421346 ambayo ipo secured. Opening na Closing date yake ni 10:00 hadi 10:30, 04/04/2022

Hii ndiyo zabuni ambayo mkandarasi (CCECC) alishinda kama ilivyoonekana katika mfumo wa TANePS. Mwigulu, hotuba ya Bajeti kuu ya serikali ilisema ni $2.1 bilioni (Sh4.90 trillioni) kwa 516km. Mkataba wa ujenzi uliosainiwa kati ya TRC na CCECC ni $2.7bn (Sh6.34 trilioni) kwa 506km

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) aliyepewa zabuni hiyo bila kushindana (single source) ana zaidi ya 38% ya kiasi ambacho Mwigulu (waziri wa fedha) amekitaja katika hotuba yake ya bajeti. Gharama za ujenzi ni US$4.8M (Sh11.19bn) kwa kila 1km.

Hii tofauti ambayo ni ziada ya Sh1.45 trilioni, ni mara 30 ya pesa waliotumia USA kushambulia miji ya Homs na Damascus nchini Syria 14.4.2018. USA walitumia Nyambizi inayotumia umeme wa nyuklia, ndege ya kijeshi B-1 bomber na meli vita bajeti ikiwa US$26M (Sh60.7 bilioni)

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka–Mwanza (249km). Miezi 16 alijenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli aliweka katika miezi 17. Mwigulu akaenda bungeni kusema haukuwepo ufadhili wa kifedha. MZAHA.

RICHMOND; kampuni ilipewa zabuni ya kuzalisha umeme ikiwa haina fedha, wataalam wala ofisi. Ndiyo iliondoka na Edward Lowassa. Sasa China Civil Engineering construction corporation (CCECC) nao wamepewa zabuni katika mazingira kama hayo. Mwigulu anakiri kweli hawakuwa na fedha

Utaratibu wa zabuni za ‘single source’ ni LAZIMA mkandarasi akidhi vigezo na uwezo. Huyu mkandarasi wa Mwigulu hana sifa hizo. Miezi 17 alishindwa kupeleka hata ambulance, hakuna usalama kwa wafanyakazi, amefanya kazi kwa 4.4%. Mkandarasi huyu hajakidhi vigezo vya single source.

China Civil Engineering construction corporation (CCECC) kapewa ujenzi wa lot Na.6 kutoka Tabora-Kigoma (506km). Hivyo kwa 506km mkandarasi atatumia $2.7 bilioni (Sh6.34 trillioni). Kapewa zabuni bila ushindani. Zingatia; TANePS inaonyesha ni Sh6.69 trilioni

Phase 1 Dar es Salaam – Morogoro (300km) kandarasi ni Yapi Merkezi na Mota Engil Africa. Phase 2 Morogoro - Makutupora (422km) kandarasi ni Yapi Merkezi. Phase 3 Makutupora–Tabora (294km) kandarasi ni Yapi Merkezi. Kumbuka, phase 3 imegharimu US$1.9 billion (Sh4.43 trillioni)

Mwigulu na TRC, Mkandarasi wenu, China Civil Engineering construction corporation (CCECC), amekidhi wapi vigezo vya kupewa kandarasi yenye thamani ya $2.7 bilioni (Sh6.34 trillioni) wakati kwa miezi 17 alifanikiwa kujenga lot Na.5 kwa 4.4% pekee?

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) kipande cha Tabora-Kigoma (514km) anachukua Sh6.34 trilioni. Nusu ya fedha zote ambazo zimetengwa kwa ujenzi wa DSM-Mwanza ambao ujenzi wake jumla ni Sh14.9 trillion (US$6.4 billion). Hapa kuna mashaka makubwa.

Athari za kutumia mzabuni mmoja kwa utaratibu wa manunuzi wa zabuni zisizoshindanishwa (single source) ni kiini cha rushwa, uzembe, upendeleo, pamoja na uwezo mdogo wa mzabuni. Tunaona yanayotokea kati ya Mwigulu, TRC na China Civil Engineering construction corporation (CCECC).

Mfumo wa ushindani wa wazabuni wengi, ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi, huchukua takriban miezi mitatu au zaidi hadi kutangazwa mshindi. kutoa zabuni bila ushindani kunaleta upendeleo kwa baadhi ya wazabuni kwa gharama za watu wengine. Rushwa inaweza kutamalaki.

Kimsingi lipo ongezeko kubwa (TZS 1.85 trilioni) la fedha katika biashara hii kati ya TRC na CCECC (nje ya bajeti) fedha za walipa kodi (watanzania) hivyo ni LAZIMA tuelezwe, tupate ufafanuzi. Biashara hii imegubikwa na mashaka makubwa.

Sources via

#MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila
 
Back
Top Bottom