Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,850
- 12,086
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Majaji na Kamishna Jenerali wa Magereza leo tarehe 29 Agosti, 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Viongozi watakaoapishwa ni:
A. MAGEREZA
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP Mzee Ramadhani Nyamka, kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza
B. MAJAJI
1. Mhe.Kevin David Mhina, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
2. Mhe.Gabriel Pascal Malata, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
3. Mhe. Happiness Philemon Ndesamburo, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
4. Mhe. Ruth Betwel Massam, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
5. Mhe.Adrian Philbert Kilimi,Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
6. Mhe.Godfrey Mtemi Isaya Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
7. Mhe.Obadia Festo Bwegoge, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
8. Mhe.Victoria Mlonganile Nongwa, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
9. Mhe.Gladys Nancy Barth, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
10. Mhe. Fatma Rashid Khalfan,Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
11. Mhe. Asina Abdillah Omari, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
12. Mhe.Hamidu Rajabu Mwanga, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
13. Mhe. Merlyn Leonce Komba, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
14. Mhe.Monica Peter Otaru, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
15. Mhe.Kamana Stanley Kamana, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
16. Mhe. Lusungu Hemed Hongoli,Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
17. Suleiman Haji Hassan, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
18. Mhe.Mwajuma Kadilu Juma, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
19. Mhe. Dkt.Cleophace Kassenene, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
20. Mhe. Aisha Zuni Bade, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
21. Mhe. Musa Kassim Pomo, Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
MAKAMU WA RAIS - PHILIP MPANGO
Amempongeza kamishna mkuu wa magereza pamoja na majaji walio apishwa. Amewaasa kuishi viapo vyao katika kusikiliza kesi na kutoa hukumu za haki.
Aidha, amewaasa kutokupendelea maskini wala kuwastahi wenye nguvu. Wasitazame nafsi za watu katika kuhuku, wawasikilize wadogo na wakubwa kwa kipimo sawa.
Waende wakawatendee watanzania haki kwa kuwa sheria huonekana njema ikitumika kwa halali kama ilivyo kusudiwa.
SAMIA SULUHU HASSAN - RAIS
Amesisitiza teuzi za majaji anazofanya zinazingatia usawa wa kijinsia, akiwa na lengo la kufikia asilimia 50/50. Pia katika mambo mengi yaliyosaidia kuongeza ufanisi wa utendaji wa mahakama ni kuongezeka kwa majaji wanawake ambao kiwango chao cha uadilifu kipo juu kuzidi wanaume.
Ataendelea kufanya teuzi kulingana na miongozo ya kikatiba pamoja na uwezo wa kiuchumi wa nchi.
Pamoja na kuwa Mungu ndiye mwenye haki, ni muhimu kwa majaji hawa kusimama katika haki kwani wamepewa dhamana kubwa inayohusisha haki za watu.
Muhimili wa mahakama unapaswa kusimama vizuri ndiyo maana amekuwa anaruhusu majaji wasafiri kwenda sehemu mbalimbali ili wajifunze pamoja na kubadilishana uzoefu kutoka nchi mbalimbali. Hii itaongeza ufanisi wa mhimili huu pamoja na kupunguza malalamiko ya wananchi.
Kuhusu magereza, maisha na wafungwa pamoja na haki zao zilindwe. Taasisi hii ifanyiwe marekebisho na kuongozwa kwa weledi.
Wafungwa ni binadamu kama walivyo wengine, lazima wapate haki zao zote pamoja na kuwasaidia kurekebisha tabia zao. Aidha, taasisi hii ina changamoto ya utawala bora. Ni muhimu yawepo mafunzo kwa watendaji wanaosimamia taasisi hii.
Kutokufuata sheria kwenye matumizi ya fedha ya magereza ni changamoto kubwa. Kazi kubwa iende kufanywa kwenye kitengo hiki.