Lukuvi ndiye aliitendea haki wizara ya ardhi

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Lukuvi amefanya mengi sana pale wizara ya ardhi na alikuwa na maono, mipango na mikakati sahihi.

Lukuvi ndiye aliyehamisha kazi ya kutoa hati milki za ardhi kutoka wizarani na kwenda kwenye ofisi za Kanda. Haikupita muda akashusha mpk ofisi za mikoa.

Kaingia Angelina Mabula akataka kuendeleza maono ya Lukuvi lkn viatu havikumtosha.

Sasa kaingia Jerry Slaa. Hyu tangu aingie anatoa ahadi na matamko tu na wakati mwingine kusimamisha maafisa ardhi lkn kero ziko pale pale.

Matamko ya Slaa yameanika udhaifu wake kiuongozi. Aliahidi na kutamka kuwa ndani ya siku 100 atakuwa kamaliza migogoro yote ya ardhi nchi hii. Wenye akili waliishia kumcheka tu, kwasabb wanajua wingi na mizizi ya migogoro ya ardhi na ugumu wa kuimaliza. Siku 100 zimeisha hata 1 ya 8 ya migogoro hajaitatua.

Sasa ametoa tamko jipya ambalo bila shaka wazoefu wa wizara hii akina Lukuvi huko waliko watakuwa wanakunywa juisi huku waking'ong'a tu. Eti kapiga marufuku wananchi kununua ardhi isiyopimwa. Na kwamba kuanzia Sasa ardhi itauzwa na maafisa ardhi tu.

Maskini Jerry Slaa!!! Natamani mtu amnong'oneze kwamba hiki alichokisema ni kituko cha karne.

*Hivi anafahamu kwamba nusu ya migogoro ya ardhi nchi hii imesababishwa na hao hao maafisa ardhi?

*Hivi anafahamu utofauti wa bei uliopo kati ya viwanja vilivyopimwa na visivyopimwa Vs uwezo wa wananchi kiuchumi?

Mwambieni Jerry Slaa kwamba ama atengue tamko lake ama asubiri kutenguliwa yeye.
 
Migogoro ya Ardhi chimbuko lake sheria yetu mama. Kwakuwa inatamka Rais ndio mwenye ardhi, nadiriki kusema hati haina uzito wowote. Kwa kulifahamu hilo, sio Mawaziri, wakuu wa Mikoa , wananchi , yeyote yule akiumendendea mendea eneo lolote anakianzisha mgogoro. Njia nyingi tu ya kuanzisha migogoro. Na kisiasa ni rahisi Kwa walio wengi au wenye nyadhifa kusikilizwa na hati kufutwa. Kwa msingi huu migogoro ya ardhi atakayeumaliza Tanzania hayupo ni ugonjwa wenye mizizi mizito kuingoa ni kungoa serikali madarakani. Jerry slaa aendelee kushabikia mwanawe apate ujumbee wa chipukizi tu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kiufupi, Sekta ya ardhi ni ngumu sana. Halafu ina hela sana. Inahitaji mtu mwenye uwezo wa ziada
 
Back
Top Bottom