Rais Samia: Tulifika uchumi wa kati tukarudishwa, tupambane turudi tulikokuwa

ukitembelea maeneo ya vijijini halafu ukasikia tanzania kuingia uchumi wa kati utashangaa sana. uchumi wa kati na umaskini huu tulio nao!!!!! unemployment hii?
 
Rais alishakufa!
Na walisema kuingia uchumi wa kati ni juhudi za Kikwete na sio Magufuli... sasa tuone!
Hakya nani tukirudi tena uchumi wa kati NAJITOA JAMIIFORUM
 
Kwenda uchumi wa kati siyo kitu Cha bahati mbaya Bali ni mipango ya mwamba kutoka chato na kwasasa hayupo,kwaiyo aliuleta uchumi kati na sasa amaondoka nao,acha tuone hatima ya hili.
 
Kwanza hata speed of light haijui wala kuilewa unajiandikia na kujiropokea linamba huyo role model wako.

Speed of light ni 3*10^8 [m/s], got it?
 
ukitembelea maeneo ya vijijini halafu ukasikia tanzania kuingia uchumi wa kati utashangaa sana. uchumi wa kati na umaskini huu tulio nao!!!!! unemployment hii?

Tatizo la umasikini wetu wakati mwingine ni la kujitakia tu. Mfano unakuta mtu huko kijijini anamiliki ng’ombe 1000 lakini ukiangalia maisha anayoishi yeye na mifugo yake havina tofauti. Wakati ng’ombe mmoja akimleta mjini na kumuuza anapata sio chini ya laki 3-8 hivii, akiweza uza hata ng’ombe 500 huyu mtu anakuwa na hela nyingi sana na hii mifugo bado itaendelea kuzaliana kila kukicha.
Wengine wana ardhi ya kutoshaa, lakini bado sisi tunajiita masikini. Huu umasikini wetu huu upo vichwani zaidi.
Mwamba alijitahidi sana kutuondolea hizi fikra.
RIP JPM
 
Wewe umeangalia asichokijua tu lakini hujasema unachokijua hapa.. chuki ni upofu

Ninachokijua ni speed of light niliyomsahihisha, kulikuwa hamna haja ya kuandika kitu ambacho hakijui wala kukielewa, angeweza kuacha hiyo namba ya speed of light na wafuasi wake bado mngemuelewa tu, lkn anafanana na anayempigia debe hata hivyo, maneno meengi no substance!
 
Ukitolewa kwenye nchi zenye uchumi wa kati lazma kuna faida unazipata hasa zal misaada yenye nafuu kuliko uchumi wa kati.
Sijajua kama imefanyika makusudi au vipi maana kuingia uchumi wa kati sanasana wanaangalia kadirio la kipato cha mtu mmoja mmoja katika nchi (per capital income)

Sasa imeshuka ghafla!!
 
Mbona kama tunafanywa wajinga na baadhi mnakubali....
Tulikua uchumi wa Kati wa Chini hakuna kundi lingine hilo ndo la mwisho sasa ukisema tumeondolewa hapo ni ili tuwekwe wapi ama Sisi tumeanzishiwa kundi spesho?
Au pengune tumekua nchi fukara....

Anyway alikua makamu wa Rais....CCM NI ILE ILE
 
Hahahaha, haiwezekani kila mwaka tulioe trillioni 20 mariba matupa kwa waliotukopesha halafu tubaki salama. Pumzika kwa amani JPM, si mmesema mnafungua nchi nyie, imekuwaje?
 
Mbona kama tunafanywa wajinga na baadhi mnakubali....
Tulikua uchumi wa Kati wa Chini hakuna kundi lingine hilo ndo la mwisho sasa ukisema tumeondolewa hapo ni ili tuwekwe wapi ama Sisi tumeanzishiwa kundi spesho?
Maana yake tumerudi kwenye nchi masikini kabisa duniani za kutupwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…