Rais Samia: Tanesco iliharibiwa hapa katikati eti mwananchi aunganishiwe umeme kwa sh 27,000/=

Mada imechelewa kuruhusiwa na mods kuingia jukwaani mkuu. Hotuba imeisha
Dah... mods hawana maana kabisa. Nachelea kusema neno nisijekujikuta natamka yale maneno kuntu.... NIMEKOSA MIMI....
 
Machinga wanapigwa, bei ya vitu juu, umeme nao kuunganishiwa iwe juu.

Sawa hiyo ndiyo ccm mpya

Umehama CCM mkuu?

😁😁😁 cha moto sasa wanakiona watu wote...na hapo sindano haijaingia yote bado
 
Amesema kwa wale wenye hali ya chini huko vijijini watawafanyia hisani ila kwa wengine walipe kulingana na uhalisia.
 
Umehama CCM mkuu?

😁😁😁 cha moto sasa wanakiona watu wote...na hapo sindano haijaingia yote bado
Hawa walijiona miungu watu sababu ya Bwana yule. Sasa acha tuisome namba wote.

Waliamini mungu wao, kiongozi wa malaika mbinguni ndio kila kitu kwao. Sasa yuko chini ya dongo.

Mungu mdogo aliyebakia ambaye alimwona Yesu na "mkewe" naye kapigwa teke na mwanamke.

Hivi sasa ni kulia na kusaga meno

Mi nasema mama apewe mitano tena tuheshimiane mjini
 
Naangalia marudio ya hotuba ya rais hv sasa kupitia ITV rais Samia anatema cheche.

Amegusia suala la kuunganisha umeme kwa sh 27,000/= na akasema kuwa haina uhalisia kabisa na haiwezekani.

Amemtaka waziri wa nishati kuweka gharama zitakazowezesha Tanesco kujiendesha kwa faida. Tena akamtaka waziri asiogope kueleza suala hili kwa wananchi.

"Hapa katikati Tanesco iliharibiwa kwa kusema eti gharama za kuunganisha umeme ziwe sh 27,000/=".

Sasa nawauliza, mnamfahamu aliyetoa wazo hili la kiuharibifu kwa Tanesco?
Sera ya serikali iliyopita ilikuwa ni umeme ufike mpaka vijijini.. hakuna mwanachi ambae ameshindwa kulipa Ada ya 20,000 Kwa mwafunzi akaweza kulipa 420,000 kama gharama za awali kuunganishiwa umeme.

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom