Ze Bulldozer

JF-Expert Member
Jun 12, 2020
730
500
Mimi ni mkristu safi naomba ifahamike hivyo, Nimeokoka na nampenda sana Mungu Baba, Yesu kristu na Roho Mtakatifu,

Mungu wangu ananguvu kuliko nguvu zenyewe, hakuna linaloshindikana katika yeye,

Mungu wangu anataka imani tu na kila kitu kwako kitakuwa ni Ushindi na Pepo ni uhakika,

Uwepo wake huambatana na ishara mbalimbali kama hii ya mvua ghafla,

Mtakumbuka,hivi majuzi wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Hospitali ya Rufaa Bugando,

Wakati Mhe Rais akiendelea na hotuba yake alipofikia hatua ya kusema "Tuombe dua kuiombea mvua inyeshe " dakika zilezile mvua ikaanza kunyesha (angalia video).

Mkumbuke kunawatu wameusaka Urais kwa zaidi ya miongo mitatu sasa akiwemo Mhe Edward Ngoyayi Lowassa, Dkt. Slaa, Mhe Bernard Membe,Mhe Freeman Mbowe na wengine wengi.

Pamoja na msako wao huo wa Urais wa JMT lakini hawajawahi kupata Urais hata wa TFF.

Chaajabu, Rais Samia Suluhu Hassan hajawahi kuomba Urais popote lakini Mungu wa Mbinguni akamchagua yeye kirahisi tu,

Swali: Rais Samia Suluhu ni nani hata Mbingu na nchi zinamsikia na kuachilia mvua papo hapo?


|[Mungu wa Elia& Elisha

tunaomba mvua yenye neema tunakutukuza wewe peke yako katika Utatu mtakatifu]|
#SISI NI NANI HATA TUSIKUUNGE MKONO.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Acheni kufuru. Nina imani Samia hataingia kwenye mtego huu wa kishetani.

Mbingu na nchi zinamtii Mungu pekee yake maana ndiye aliyeziumba.

Kwani hiyo siku mvua iliponyesha Mwanza, ilikuwa siku ya kwanza kunyesha? Mvua Mwanza, kwa msimu huu wa mvua zimenyesha mara nyingi, na nyingine moaka ziliezua mabati ya nyumba za watu kuke Ilemela kueleka Airport.

Kabla ya siku hiyo, nilikuwa Shinyanga, mvua kubwa ilikuwa imenyesha. Siku ya nyuma yake nilikuwa Tabora, mvua kubwa ilikuwa imenyesha.

Kagera mvua zimekuwa zinanyesha maeneo mengi tangu mwishoni mwa mwezi wa September.

Uwongo na unafiki haumwongezei mwanadamu chochote zaidi ya aibu na fedheha.
 

Nyamagondo

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
538
1,000
Yesu Kristo si Mungu ,hata kwa imani ya wakristu wanaoijua dini yao kiundani kabisa wanalijua hilo.
halafu wacha kukufulu ni wapi Mbingu na ardhi zilionyesha kumtii Raisi Samia Suluhu Hasani. wewe utakuwa mshilikina tu ,ndio wenye imani hizo za kichawi.
John 1:1-3
[1]In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

[2]The same was in the beginning with God.
Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

[3]All things were made by him; and without him was not any thing made that was made.
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
John 1:1-3
[1]In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu...
Andiko jingine lanena:
John 1:18 “No one has ever seen God, but the one and only Son, who is himself God and is in closest relationship with the Father, has made him known.“

Yohane 14:6-9 BHN

Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na ukweli na uhai. Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu. Ikiwa mnanijua mimi, mnamjua na Baba yangu pia. Na tangu sasa, mnamjua, tena mmekwisha mwona.”

Filipo akamwambia, “Bwana, tuoneshe Baba, nasi tutatosheka.” Yesu akamwambia, “Nimekaa nanyi muda wote huu, nawe Filipo hujanijua? Aliyekwisha niona mimi amemwona Baba. Unawezaje basi, kusema: ‘Tuoneshe Baba?’
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,850
2,000
Sasa iweje sifa umpe mwanasiasa badala ya kuwapa hao viongozi wa dini walioomba?

Anyway, hiyo mvua kama ilikuwa inakuja hata bila maombi ingenyesha tu, coz sio kila panaponyesha mvua lazima maombi yawe yamefanyika, na pia, sio kila panapofanyika maombi lazima mvua inyeshe.

Kama mnaona ni rahisi hivyo, basi nashauri Rais azunguke mikoa yote Tanzania kuongoza maombi ya mvua tuondokane na hiki kiangazi, aanze na huko Arusha alipo sasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom