Rais Samia naomba umfariji Tundu Lissu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,697
2,000
Rais wetu mama, Tanzania ni ya watanzania wote, na kila RAIA ni muhimu sana kwa nchi yake. Watanzania hawana kwao kwingine ila Tanzania.

Kilichompata Tundu Lissu ni vigumu kuamini kwamba yuko hai hadi Leo.

Tundu Lisu amepata maumivu makubwa sana ya kimwili, kisaikolojia, kijamii na kiuchumi. Anahitaji MTU muhimu wa kumwambia pole. Kama mfariji mkuu tafadhali mfariji huyu RAIA wako mwenye weledi mkubwa wa sheria.

Tumuite nyumbani aungane na watanzania wengine kwenye ujenzi wa nchi yao, kufanya hivyo dunia itatutukuza kama taifa.

Tumlipe anachostahili kama kipo, tumhakikishie usalama wake kama anayo hofu, tumrudishe nyumbani kama hawezi.

Vyama vingi ni mfumo ambao uko kwenye katiba yetu, usiwe uhasama bali tuendeshe kwa staha kwakuwa ulibuniwa na wazungu bila ya sisi kujitayarisha ili tuvurugane wenyewe kwa wenyewe.

Nadhani Tanzania yetu ni kubwa kuliko vyama vya siasa. Vyama vinakufa lakini taifa halifi.
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,697
2,000
Faraja kutoka kwa mkewe inatosha
Mama analea kuliko baba, ninao ushahidi kuwa akinamama waliumia sana kuliko akina baba kwa kitendo cha lissu kumiminiwa risasi na wasiojulikana. Rais wetu ni mama kama mama wengine anaelewa maumivu ya mtoto kufanyiwa vile. Ndiyo maana alienda kumjulia hali kwenye ule wakati mgumu kwa lisu
 

crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,357
2,000
Changamoto inakuja zikija memory za mikwara ya MIGA na zile harakati za kugombea kifusi cha makinikia..
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
6,697
2,000
Na shoga yake rob amster juu!
Jaribu kuvivaa viatu vya TL halafu akuachie viwe vyako uone. Hivi siasa tu zinasababisha mtu auawe, ageuzwe mlemavu na awe mkimbizi. Kwani tunafanya hivyo kwa maslahi ya nani. Taifa litabaki sisi sote tutapita, na wala kesho zetu sio nyingi kivilee.

Binafsi napenda nikifa nikumbukwe kwa mema, kama nitashindwa kuwatendea mema basi nitawapandia mti wa kivuli na matunda kwaajili yao wakae kivulini wakati wa jua Kali.
 

Nigrastratatract

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
705
1,000
Jaribu kuvivaa viatu vya TL halafu akuachie viwe vyako uone. Hivi siasa tu zinasababisha mtu auawe, ageuzwe mlemavu na awe mkimbizi. Kwani tunafanya hivyo kwa maslahi ya nani. Taifa litabaki sisi sote tutapita, na wala kesho zetu sio nyingi kivilee.

Binafsi napenda nikifa nikumbukwe kwa mema, kama nitashindwa kuwatendea mema basi nitawapandia mti wa kivuli na matunda kwaajili yao wakae kivulini wakati wa jua Kali.
Tundu lisu hana akili utavaaje viatu vya mwehu amewatumaa kubwabwaja eeh mwambieni majuto ni mjukuu na bado ataendelea kuteseka sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom