Rais Samia ametoa tiketi 7,000 za mechi ya Stars vs Uganda

Izy_Name

JF-Expert Member
Apr 9, 2020
647
1,295
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amesema tiketi hizo ni kwa ajili ya motisha ili kuhakikisha timu yetu ya taifa inafanya vizuri katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa na Uganda siku ya jumanne tarehe machi 28.



"Tunashukuru sana jitihada za Rais wetu katika maendeleo ya michezo hapa nchini, tunaamini kwa umoja huu uliopo tutafikia malengo yetu tuliyojiwekea ya kuona tunapiga hatua."

Aidha Yakubu aliongeza kwa kusema kuwa mbali na tiketi hizo za mheshimiwa Rais kunaa wadau wengine mbalimbali wamejitolea kwa lengo la kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi uwanjani ili kutoa sapoti kwa timu yao ya Taifa (Taifa Stars).

"Tunamshukuru pia Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kwa kutoa tiketi 2000 na sisi kama Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo tunatoa 11, 000 na wale wote ambao wamejitoa ingawa hawakutaka kutajwa majina yao wazi," amesema.

Kwa upande wa Rais wa TFF, Wallace Karia aliongeza kwa kuipongeza Serikali chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa inazozifanya kwa ajili ya maendeleo na jitihada mbalimbali inazozifanya katika kukuzasoka letu hapa nchini.

"Tunatambua changamoto kidogo zilizopo hasa katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan lakini naamini Watanzania watajitokeza kwa wingi ili kuipa timu yetu hamasa." amesema Karia.

Vilevile Karia aliwapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kucheza soka safi na kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi dhidi ya Uganda iliyochezwa Machi 24 nchini Misri wiki moja iliyo pita katika jiji la ismailia.
 
Tatizo la timu yetu ya Taifa siyo ya kuiwekea dhamana hata kidogo. Yaani ukitaka kufa kwa ugonjwa wa moyo, iwekee dhamana hii timu! Pale unapofikiria watashinda, unashangaa wanafungwa!

Halafu kwenye mechi unayofikiria watafungwa/ au kutoa sare; wanashinda!!
 
Tatizo la timu yetu ya Taifa siyo ya kuiwekea dhamana hata kidogo. Yaani ukitaka kufa kwa ugonjwa wa moyo, iwekee dhamana hii timu! Pale unapofikiria watashinda, unashangaa wanafungwa!

Halafu kwenye mechi unayofikiria watafungwa/ au kutoa sare; wanashinda!!
Yaan kiufupi haitabiriki
 
nilichogundua kuhusu timu ya taifa sio kama vipaji hakuna au wachezaji hatuna hapana sababu ya timu yetu ya taifa kuwa kama hivi ilivyo ni serikali yetu kutokujali maslahi ya wachezaji wanaoitwa kutumikia timu ya taifa posho ndogo ila pia hakuna maslahi na posho za kumfanya mtu ajitume.

mambo ya kuwa mzalendo kwa taifa hakuna siku hizi ni maslahi kwanza.

serikali iangalie hili mchezaji akichaguliwa team ya taifa haisi ni bahati na aone fahari kutumia nchi yake.
 
Back
Top Bottom