Rais Samia na dhana ya "Baniani mbaya kiatu chake dawa"

Rais Samia na dhana ya "Baniani mbaya kiatu chake dawa"

Mada kama hii huwezi kupata wachangiaji humu jf.
Hapa weka mada ya kumponda Samia uone utavyoungwa mkono bila kujali uongo utakaosema
Nawaita haters wa Samia na mpaka Sasa wameshaprove kuwa hawana mpango wowote hivyo ni wa kuwapotezea tu.
 
Tanzania tumeanza utamaduni mbaya sana siku hizi. Yeyote anayelisema zuri lolote la serikali anaitwa chawa, kibaraka na maneno mengine mengi ya hovyo hovyo.

Siku hizi ukweli hautokani tena na hali halisi, bali ni chochote kile kinachoonekana kimesemwa na mwenzetu. Jambo hili ni hatari sana, kwani sasa nyeusi tutaita nyeupe maadam tu mwenzetu kasema.

Chukulia kwa mfano uamuzi wa serikali ya awamu ya sita kuondoa "retation fee" kwenye madeni ya mikopo ya elimu ya juu. Ingawa jambo hili limetua mzigo kwa wanufaika wa mikopo hiyo wa kuwa na deni linalokua kila mwaka, lakini bado tunaaminishwa serikali haijali vijana.

Vijana walioingia kwenye soko la ajira katika kipindi cha mwaka 2015-2021, na watuambie katika kipindi hicho waliona matangazo mangapi ya ajira za serikali?

Ni kipindi hicho hicho watumishi hususani wa serikali kuu walikaa bila kupanda cheo wala kimo na wakaufyata. Lakini leo hali ni tofauti.

Sipo hapa kusema selikali ya awamu ya sita ni serikali ya malaika, hapana! Inayomapungu yake, lakini hayo mapungufu yasiwe sababu ya kuiona kuwa haijafanya zuri lolote, kwani kusema hivyo ni kujidanganya wenyewe.

Kama nchi tutanufaika sana kujenga utamaduni wa kupenda mijadala ya maswala na hoja kuliko ushabiki wa kivyama
Mkuu umeongea vizuri sana. Nyie wakweli Wala msitetereke na hawa haters, endeleeni kutueleza ukweli. Nakuhakikishia kuwa ukweli wanauona na Wana ukiri mioyoni mwao sema ndo hivyo tena vinywa vyao havisemi sababu ya chuki.
 
Hii itakuwa AI ya kichina, tumia. AI yaujerumani au USA Ili picha ikae vizuri zaidi.
FB_IMG_1748360197313.jpg
 
Tanzania tumeanza utamaduni mbaya sana siku hizi. Yeyote anayelisema zuri lolote la serikali anaitwa chawa, kibaraka na maneno mengine mengi ya hovyo hovyo.

Siku hizi ukweli hautokani tena na hali halisi, bali ni chochote kile kinachoonekana kimesemwa na mwenzetu. Jambo hili ni hatari sana, kwani sasa nyeusi tutaita nyeupe maadam tu mwenzetu kasema.

Chukulia kwa mfano uamuzi wa serikali ya awamu ya sita kuondoa "retation fee" kwenye madeni ya mikopo ya elimu ya juu. Ingawa jambo hili limetua mzigo kwa wanufaika wa mikopo hiyo wa kuwa na deni linalokua kila mwaka, lakini bado tunaaminishwa serikali haijali vijana.

Vijana walioingia kwenye soko la ajira katika kipindi cha mwaka 2015-2021, na watuambie katika kipindi hicho waliona matangazo mangapi ya ajira za serikali?

Ni kipindi hicho hicho watumishi hususani wa serikali kuu walikaa bila kupanda cheo wala kimo na wakaufyata. Lakini leo hali ni tofauti.

Sipo hapa kusema selikali ya awamu ya sita ni serikali ya malaika, hapana! Inayomapungu yake, lakini hayo mapungufu yasiwe sababu ya kuiona kuwa haijafanya zuri lolote, kwani kusema hivyo ni kujidanganya wenyewe.

Kama nchi tutanufaika sana kujenga utamaduni wa kupenda mijadala ya maswala na hoja kuliko ushabiki wa kivyama
Kwanini mnapenda kusifiwa kwa mambo ambayo ni wajibu wa serikali🤔

Ibara ya nane ya Katiba hii ambayo Samia aliita ni kijitabu tu iko wazi kabisa "Serikali itawajibika kwa wananchi"

Hata wakoloni walikuwa wanatoa ajira na kujenga hospitali, barabara, reli n k lakini walikataliwa
 
MWENYE MAMLAKA YA ULIMWENGU HUU AKUREHEMU.

Mauaji ya kikatili namna hii unaita zilipendwa???

Huu MSIBA hautaisha. Tutapiga kelele tukiwa hai, na hata tukifa bado tutaendelea kupiga kelele popote tutakapokuwa.

WAO walikuwa kama SISI, na SISI tutakuwa kama WAO.
Hakuna msiba usioisha.
Alikufa Nyerere, Magufuli na maisha yanaendelea.
 
Mimi binafsi nitakupinga Hadi naingia kaburini, shetani alikuwa malaika aliyeasi, asikudanganye na vitu vidogo anavyofanya ambavyo alikuwa akivifanya akiwa malaika. Ukipewa kazi ya kulinda uhai wa mtu mwengine alafu ukashindwa au ukashiriki kuukatisha uhai wa raia...alafu ukiulizwa unatoa sababu zisizo na msingi...wewe unayesifia tutakuita mshirika au chawa wake katika maovu anayoendelea kuyatekeleza. Kitu Cha kwanza ni uzima, hayo mengine hata kama unayafanya kwa upendeleo Haina shida sana
 
Back
Top Bottom