Rais Samia, Mteue ACP Theopista Mallya awe Mkuu wa Trafiki Nchini, asante kwa kumteua Kaganda

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Salaam Wakuu,

Rais Samia ameonesha Ushujaa ukomavu mkubwa na Ushujaa wa nguvu, kumteua Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi.

Kutokana na ajali kuongezeka barabarani, ni muda mwafaka rais kumchukua Mkuu wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Theopista Mallya, awe Mkuu wa Usalama Barabarani.

Mara rais Samia ulipoingia Madarakani, Kwa takwimu, watu 1,191 walifariki dunia na 2,139 kujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani 1,594 zilizotokea nchini kati ya mwezi Julai mwaka 2021 na mwezi Machi mwaka 2022 likiwa ni ongezeko la silimia 29.8.

Na Jeshi la Polisi wote kufa wanaona kawaida wala hawawajibishani. Nia wanataka watu waseme Rais Samia haufanyi kazi. Hii ni hujuma.

5.jpg

ACP Theopista Mallya atawawanyosha Matrafiki Wapokea Rushwa na Madereva Wazembe.

Ni Wakati wa watendaji wapenda haki Serikali watiwe moyo sababu wanapitia Magumu mengi.

Kuteuliwa kwa ACP Theopista Mallya kitafanya Watendaji wengine wajue kumbe ukiwa mchapa kazi mzuri Serikali inaona. Tusiishie kuwapa vyeti siku ya Mei Mosi tu.

Naamini ACP Theopista Mallya hatatuangusha. Nenda kafanye kazi. Tujivunie kuteuliwa kwako.

Je, ni nani Askari Mwadilifu mwingine unadhani anafaa kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani? Mpendekeze rais amuone.

Pia soma; Viva Tanzania, Viva Afande SACP Susan Kaganda, Rais Samia ni Msikivu
images (1).jpeg
Screenshot_20221025-080602.png
 
Ajabu niliyokuwa sifahamu ni kwamba toka tupate uhuru Kaganda ndio mwanamke wa kwanza kuwa CP! Hili ni tatizo kwenye majeshi yetu! Pengine hata Kaganda kelele za nje ndio zimesaidia....
 
Ajabu niliyokuwa sifahamu ni kwamba toka tupate uhuru Kaganda ndio mwanamke wa kwanza kuwa CP! Hili ni tatizo kwenye majeshi yetu! Pengine hata Kaganda kelele za nje ndio zimesaidia....
Nafikiri ni wa pili mkuu fuatilia vizuri
 
Clip za kiki zinasaidia watu kupata vyeo.

Mwambie Theopista aandae clip moja matata sana wiki hii hii atapewa cheo.

NCHI HII VETTING ZERO/SIFURI.

kiki, jinsia na dini yako ndio vitakavyokubeba.
 
Anaye teua mkuu wa trafiki sio rais bali ni IGP.
Hivi Ng'hazi kateuliwa wiki moja tu unataka atimuliwe uko siriaz kweli?
Mallya ana kipi cha ziada?
Mkuu, hapo ndo unakosea. Rais wa Nchi ana Mamlaka makubwa sana ukizingatia ndiye Mwajiri Mkuu wa Serikali. Ndo maana hata kesi ya Mbowe watu walikuwa wanasema Samia muachilie Mbowe. Kwani samia alikuwa ni hakimu? Rais hawezi kukubali watu wake waendelee kufa eti kisa hateui yeye. Anatoa maelekezo kwa IGP. Kikubwa ni Ustawi wa Jamii
 
Kusema ukweli huyu Dada Msllya wakati akiwa Rto Kinondoni na baadae kuwa Staff one jeshi la polisi aliweka nidhamu kwa Rtos wote Tanzania. Walikuwa na nidhamu na kutekeleza majukumu yao.

Kitu kidogo hawa wa chini waliomba kwa siri sana. Cha ajabu badala ya kumfanya mkuu wa usalama barabarani ili awe na madaraka kamili wakamfanya Rpc.

Huenda aliwazibia wengi kula zao. Na kila wakati mwenye kusimamia misingi ya haki huonekana mbaya.

Ni wakati sasa, kama kweli kuna kusafisha maovu polisi, huyu Dada apewe kitengo cha usalama barabarani.
 
Kusema ukweli huyu Dada Msllya wakati akiwa Rto Kinondoni na baadae kuwa Staff one jeshi la polisi aliweka nidhamu kwa Rtos wote Tanzania...
Kipindi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania akiwa afande SACP Fortunatus Musilimu, msaidizi wake alikuwa Staff Officer ACP Teopista Mallya. Na kazi ilikuwa inaenda vizuri.

Simu yake ilikuwa wazi kuripoti tukio lolote barabarani. Awe dereva au Askari lazima haki itapatikana. Hasa mabasi haya.

Alikuwa anataka Taarifa yako iseme:

A. Ni nani amehusika au ni gari gani imehusika;
B. Ipo wapi kwa muda huo;
C. Inatokea wapi inaenda wapi.
D. Taja namba za gari husika,
E. Na kila inapowezekana tuma na ushahidi mfano picha, video, au sauti ya tukio husika.
Ajali zilipungua sana. Trafiki wala rushwa barabara walipungua sana. Hata akikuomba rushwa namba yake kwenye shati anaificha. Ila Polisi ukiwa mtenda haki, unapita milango ya Miba.

Mfano kaganda alitolewa kuwa RPC kinondoni akaenda kufichwa Makao Makuu eti adili na Wastaafu. Ila Mungu hamtupi mja wake. Askari Msivunjike moyo. Jipeni moyo na msiache uadilifu sababu ya watu wachache wanao wanyanyasa
 
Naunga mkono hoja, wanawake ni waadilifu na Kwa nafasi ya Mkuu wa Traffic atakuwa na sense ya huruma kwa sababu ni Mwanamama, Wanaume ni washenzi tuu na wasio jali utu.
 
Hawa trafiki kazi yao imebaki kuokota za kubrashia viatu, maeneo ya barabara ya mlimani city wanavizia asubuhi asubuhi magari kwenye taa za kwenye zebra.....afisa unaamka alfajiri kwenda kuvizia magari yanayowahi makazini (rush hours) kwa kukamata magari kwenye zebra kwa kisingizio cha taa nyekundu wakati hakuna watu wanaovuka, nafikiri tukubaliane kwamba kubambika makosa na kudai rushwa ndo utaratibu wa kawaida wa utendaji kazi wa hili jeshi la polisi.....naunga mkono huyo ateuliwe kama ana commitment ya kuondoa hii aibu ya rushwa kwa matrafiki wanaojazana huko mabarabarani.​
 
Naunga mkono hoja, wanawake ni waadilifu na Kwa nafasi ya Mkuu wa Traffic atakuwa na sense ya huruma kwa sababu ni Mwanamama, Wanaume ni washenzi tuu na wasio jali utu.
Mimi huwa namkubali sana kamanda Magiligimba akiwa RPC Shinyanga alifanya kazi nzuri sana, sijui kwanini Siro alimtoa na kumpeleka makao makuu?
ukute labda aligusa pasipogusika but she was very competent in all aspects.
 
Ajabu niliyokuwa sifahamu ni kwamba toka tupate uhuru Kaganda ndio mwanamke wa kwanza kuwa CP! Hili ni tatizo kwenye majeshi yetu! Pengine hata Kaganda kelele za nje ndio zimesaidia....
Hapana,anakuwa Mwanamke wa Pili!!
 
Afande Malya ni Kiboko,Ila nasikitika kuwa hawezi kuteuliwa kwenye hiyo nafasi kwa sababu ya CP Awadhi!!,Kumbuka kuwa Afande Awadhi akiwa ZTO-DSM,Afande Malya alikuwa RTO-Kinondoni wote wakiwa rank Moja!!kulikuwa na misuguano Sana Kati hao wawili!!
 
Back
Top Bottom