Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
RAIS SAMIA: MRADI WA MKUJU KUIWEKA TANZANIA KWENYE RAMANI YA URANI DUNIANI
✅️ Azindua Kiwanda cha Majaribio cha Uchenjuaji Urani Namtumbo- Ruvuma
✅️ Asema Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 10 zinazozalisha Urani kwa wingi duniani.
✅️ Mradi kuzalisha tani laki 3 za Urani kwa mwaka
✅️ Serikali inamiliki hisa asilimia 20 ya mradi
📍 Namtumbo – Ruvuma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa Mradi wa Uchimbaji na Uchakataji Madini ya Urani uliopo katika Eneo la Mto Mkuju, Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma, ni hatua ya kimkakati itakayoiweka Tanzania katika ramani ya dunia kwa kuifanya kuwa miongoni mwa mataifa kumi yanayoongoza kwa uzalishaji wa madini hayo muhimu duniani.
Amesema hayo Julai 30, 2025, wakati akizungumza na wananchi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha Majaribio cha kuchenjua madini ya urani kilichopo Mto Mkuju, hatua inayoashiria mwanzo wa safari ya Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji na uchakataji wa urani barani Afrika.
Rais Samia amesema kuwa, hatua hiyo ni ssehemu ya mkakati wa Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia matumizi bora ya rasilimali asilia, ikiwemo madini ya urani ambayo yana thamani kubwa kimataifa.
“Ni siku ya historia kwa nchi yetu, kwani Tanzania inaanza rasmi safari ya kuwa mzalishaji mkubwa wa madini ya urani duniani kwa mara ya kwanza katika kiwango hiki. Urani ni moja ya madini mkakati tuliyobarikiwa kuwa nayo, na upatikanaji wake utachangia katika kuzalisha nishati salama na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika sekta ya madini duniani.” Amesema Rais Dkt. Samia.
Rais Dkt. Samia amesema kuwa, kwa hatua hiyo, Tanzania inajiweka kuwa kitovu cha utafiti na uchakataji wa urani duniani na Afrika, hatua itakayofungua fursa mpya za kiteknolojia, kitaaluma na kiuwekezaji nchini na kuifanya Tanzania kuingia katika ramani ya dunia kuwa miongoni mwa nchi 10 zinazozalisha urani duniani, na hivyo kuvutia uwekezaji wa kimataifa katika sekta ya madini mkakati.
Ameongeza kuwa, Sekta ya Madini ni miongoni mwa vipaumbele vya Dira ya Taifa ya 2050, kwq kwamba kupitia sekta hiyo, Tanzania inalenga kukuza uchumi wa viwanda unaotumia teknolojia.
Attachments
-
Screenshot 2025-07-31 at 10-07-33 Instagram.png658.3 KB · Views: 16 -
Screenshot 2025-07-31 at 10-07-45 Instagram.png666.8 KB · Views: 16 -
Screenshot 2025-07-31 at 10-08-01 Instagram.png651.2 KB · Views: 14 -
Screenshot 2025-07-31 at 10-08-16 Instagram.png652.1 KB · Views: 16 -
Screenshot 2025-07-31 at 10-08-58 Instagram.png424.5 KB · Views: 13 -
Screenshot 2025-07-31 at 10-08-51 Instagram.png498.2 KB · Views: 11 -
Screenshot 2025-07-31 at 10-09-07 Instagram.png700.1 KB · Views: 11