Rais Samia Mgeni Rasmi Nanenane Mbeya, Wadau Kutoka Nje ya Nchi Kushiriki Kwa Mara ya Kwanza

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Rais Samia Suluhu Hassana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maonesho ya kilimo maarufu kama Nanenane Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema viongozi wengine kitaifa watakaotembelea maonesho hayo yanayoanza kesho ni Makamu wa Rais, Dk Phillip Mango katika katika siku ya ufunguzi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika siku ya tatu ya maonesho hayo.

Mweli alisema kwa mara ya kwanza maonesho hayo yatahusisha wadau wa kilimo kutoka nje ya nchi wakiwemo wafanyabiashara na wakulima.

"Tunapata nafasi ya kuiifunza nia bora za kilimo, pia kukutanisha wakulima na masoko kwa maana ya wanunuzi na wanunuaji wa mazao ya kilimo," alisema.

Maonesho ya mwaka huu yatakuwa na kaulimbiu ya 'Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula'.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Kilimo, Tagie Daisy alisema sambamba na maonesho ya Mbeya yatafanyika mengine ya kikanda ya kilimo katika maeneo manane ikiwamo mikoa ya Dodoma, Morogoro, Lindi na Arusha.
 
Hawa wanaojiita watanganyika wana majungu hatari sana,
Walizoea Vya kunyonga..!
RAIS WETU SONGA MBELE,WANAJUA WAMESHASHINDWA WANAJARIBU KUKUCHOSHA AKILI NDIO NJIA INAYOTUMIKA SASA,NCHI KILA MRADI UMENYOOKA,BARABARA ZINAJENGWA,MASHULE YA MAGOROFA,MAJI KILIMO KIMEPAMBA MOTO.
 
Chonde chonde watu wa Mbeya heshima Kwa mama yasitoke Yale ya Jakaya
Nilitaka kusema hili. Ujuaji na usela mavi hauna faida. Kujifanya mnajua sana na mna uchungu sana wakati mikoa mingine inapiga hatua kwa maendeleo ni upumbavu.

Mbeya mtaishia kuwa kama Kagera. Acheni ujinga na ujuaji. Ukiheshimiwa na wewe jiheshimu. Ya akina Mwambukusi waachieni akina Mdude. Tena ole wenu muipoteze fursa ya kuwa na Tulia hapo Mbeya, ole wenu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom