Rais Samia: Nanenane Mbeya Iongezewe Wiki Moja

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe aruhusu kuongezwa kwa Wiki moja zaidi ya Maonesho ya Nanenane Mbeya ili Watu waendelee na shughuli zao katika viwanja vya maonesho kama Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Dkt. Tulia Ackson alivyoomba.

“Naunganisha ombi la Mh.Spika kwamba kwasababu hapo mbele tunakwenda kubomoa eneo hili na kujenga uwanja mzuri utakaokuwa na hadhi ya Kimataifa na nilipofika hapa niliingalia mchoro na ramani utakavyokuwa ni uwanja wa Kimataifa haswa”

“Sasa kwasababu kazi hii haitochelewa kuanza naungana na Mh.Spika kutoa Wiki moja zaidi kwa waoneshaji hapa hasa waliotoka Mikoa ya nyanda za juu kusini ili waweze kuonesha na vilevile polepole wachukue vile watakavyowaona vinawafaa kabla shughuli za kubomoa hazijaanza”

“Nimtake Waziri wa Kilimo aruhusu Wiki zaidi Watu waendelee na shughuli zao hapa na kubwa zaidi ni kwamba kuingia hapa ni bure kwahiyo Watu watakuja tu watakuwepo”
WhatsApp Image 2023-08-08 at 16.48.17.jpeg
 
Back
Top Bottom