#COVID19 Rais Samia kuzindua na kupata Chanjo ya COVID-19 Julai 28, 2021

Waziri wa Afya Dk. Dorothy Gwajima amesema Rais @SuluhuSamia siku ya Julai 28, 2021 katika Ikulu ya Dar es Salaam atazindua zoezi la kuchanja chanjo ya Corona aina ya Janssen, ambapo Rais Samia atachanjwa.

Chanzo : @wizara_afyatz

View attachment 1869420
Asante kwa kutaarifu hiyo uzinduzi.
Nani asiyejua wengi walishachanjwa ile ya ubora!? Hapo ukiona anadungwa ni geresha tu! Sivyo tuwaombe waandishi wa habari hizi muonyeshe wazi zoezi la dawa hiyo kwenye Sindano na kuchomwa kwake si vinginevyo. Kama tulivyoona kwa wengine waliowapa hiyo chanjo.
Pia mtuleteeni Gwajima na Ndungai!.
 
Achanje yeye kutuwakilisha,

Ila.chonde chonde jamani, kuna baadhi ya watu watakuwa wanachomwa live kwenye tv kumbe ni maji ya dripu, sasa jichanganye na wewe uige 😂😂 baada ya miaka kadhaa ndio utajua hukujua
 
Watanzania wengi wamekuwa informed kuhusu chanjo na wahuni wa mitandaoni akiwemo gwajiboy.
Bahati mbaya na kiongozi wao wa zamani alilishwa elimu hiyo na hao wahuni na akaishikili na kisha kuwahubiria wananchi ambao hawana acccess ya kupata habari kutoka chanzo cha hakika.
Ilivyo sasa ni kuwa wale wanaomwabudu yule bwana wao wanajitahidi kuhakikisha kuwa mawazo yake yanaendelea kuaminika. Wanafanya juu chini kuendeleza zile story za wahuni ambazo bwana wao alizifuata kwa lile wanaloliita ni legacy. Ni rahisi kuwadanganya watanzania kwa mtindo huu kwani hata wasomi wakubwa wamekusudia kumuenzi bwana wao kwa hali na mali.

Ukweli kuhusu chanjo; Zina kinga ya aslimia kuanzia 70 na kuendelea.
Kwanini uendelee kuvaa barakoa?: Ni kwasababu ya hizo asilimia zilizobaki ili kufikia 100.
Side effects: Kila chanjo zina side efffects kulingana na mtu mmoja mmoja, baadhi ya watu hawapati hizo side effects.
UONGO WA GWAJIMA UPUUZWE.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hivi mna nini watanzania? Wewe kuna mtu amekushikia panga uchanje kwa nguvu? Kwanini isiachwe kwa anayetaka sawa na asiyetaka sawa?
Mkuu, hivi hutambui kuwa kwa sasa kuna uhiari katka kupata hizo chanjo? Lakini amini nakwambia siku zinakuja haitakuwa tena hiari bali ni lazima kwa watu wote kupata chanjo.

Kama unatambua kuna uhiru wa kutoa mawazo, basi nakuomba usiwapuuzie wale wenye mashaka na nini kilichopo nyuma ya agenda na uharaka wa kutaka makundi muhimu ya watu hapa nchini kuchanjwa chanjo hizo. Tambua kuwa hata kama saa ni mbovu lakini kuna wakati mishale yake huwa sahihi kuendana muda.

Kwa hiyo basi katika kipindi hiki cha uwepo wa uhiari wa kupata hizi chanjo za Johnson ambazo matumizi yake yametiliwa mashaka na baadhi ya majimbo huko Marekani, basi tujipe muda wa kujadiliana uhalali wa uharaka wa matumizi yake hapa nchini. Pengine pamoja na nia njema ya "consignment" ya kwanza ya msaada iliyowasili hapa nchini hivi majuzi kutoka USA na kupokelewa na waziri mwenye dhamana, isiwe sababu ya kuwapuuzia wale wenye mashaka nayo.
 
Back
Top Bottom