Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 1,956
- 4,143
Ni ukweli kabisa, mimi nikiwa tayari kabisa kwenda Israel na kuwa kibarua kwenye mashamba ya Wayahudi hao wa mashariki ya kati,
Kwa mshahara wa 4M!! Usinitanie bhana!
Nawasemea vijana lukuki wa Kitanzania na ambapo wengine wakiwa maofisini na wengine mitaani wakihangaika kutafuta ajira wasipate, huku walioko maofsini wakilipwa mshahara kidogo ukilinganisha na mshahara wa kibarua wa mashamba huko Israeli
Mh Rais, unapoamua maamzi haya, ni kutusaidia sisi vijana ili kujipatia kipato, kujijenga kiuchumi na kuijenga nchi yetu.
Kama tunakopa na ili tufanye maendeleo, maana yake ni kwamba, bado tupo chini ya mataifa hayo tunayoyakopa na hatujajikomboa kutoka katika hali ya utumwa wa kiumasikini
Kwa mantiki hiyo, unapotoa fursa hiyo kwa vijana, ni umetoa nafasi ya wao kujikomboa kutoka kwenye umasikini wao.
Huo sio utumwa, maana hata hapa nchini, kazi za kufanya kazi ya mashamba ya watu ipo na inaendelea.
Kama kufanya kazi kwenye mashamba ya wayahudi hao ni utumwa, vipi wale wanaofanya kazi hizo hizo kwenye mashamba ya waswahili wenzao na kwa malipo kidogo!
Binafisi, nipo tayari hata ikiwa ni leo usiku.