beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Hospitali zote zinakabiliwa na uhaba wa Watumishi, akifafanua "Hii ni kutokana na kiwango cha ukuaji wa Uchumi"
Amesema hayo leo akiwa Moshi Mkoani Kilimanjaro katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Hospitali ya KCMC
Ameongeza, "Tunapopiga mahesabu ya Uchumi kuna kitu kinaitwa Wage Bill. Kila tunapopata upenyo, Uchumi ukikua kidogo tunafanya Ajira haraka haraka hasa hizi zinazogusa maisha ya wananchi"
Vilevile, Rais Samia amesema Serikali imeendelea kuiwezesha Hospitali ya KCMC kuboresha miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kuwezesha kuwekwa mtambo wa kuzalisha hewa tiba
Ameeleza, "Mtambo huu una uwezo wa kuzalisha mitungi 400 kwa saa 24. Uwepo wa Mtambo huo wenye thamani ya Milioni 800 umesaidia kupunguza uhaba wa hewa tiba hiyo katika Mikoa ya Kaskazini hususan kipindi cha mapambano dhidi ya COVID19"