Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Kwanza kabisa nakupongeza kwa ukipofikia. 1. Kwenye chanjo
2. Kwenye Makato ya Kodi
Tanzania ilipokuwa imefikia ilikuwa ni pabaya sana. Watu waliaminishwa ujinga na wakaendelea kuishi kwenye ujinga. Tumepoteza watu wengi sana kutokana na kuaminishwa kuwa Tiba asili inatibu Corona badala ya njia za kisayansi. Mimi Pia nilipoteza rafiki yangu.
1. Kwenye Chanjo
Hapa usibadili msimamo. Aliyepita alidharau huu ugonjwa na kwa Kweli hata yeye mwenyewe ulimwondoa. Umeondoa wasaidizi wake na wananchi wengi Pia. Ni bora umeruhusu chanjo. Watu wachomwe wanaotaka na wasiotaka waachwe corona ideal nao. Mfano wa nchi zilizochukulia serious huu ugonjwa upo na sasa wameweza kuudhibiti na sasa wamerejea kwenye maisha yao na kuepusha vifo na kupoteza nguvu kazi
2. Kwenye Tozo
Hapa wala usirudi nyuma. Aliyepita hakupandisha wafanyakazi madaraja, hakuongeza mishahara. Wewe umepandisha wafanyakazi madaraja jambo lililosababisha mishahara yao kuongezeka. Aliyepita alikusanya kodi kwa nguvu na kukopa sana Hadi akawazidi maraisi wote kwa kukopa. Wewe hutaki kodi ya dhuruma na Pia unataka kupunguza kukopa sana.
Wewe unataka kufanya miradi kwa pesa za ndani kweli na sio kuwahadaa wananchi unafanya miradi kwa pesa za ndani kumbe unakopa sana na kuhatarisha uchumi kwa kuongeza deni la taifa.
Tunahitaji miradi ya kimkakati. Maji yawepo kwa wananchi wote, barabara za lami vijijini na mijini na Pia miradi mikubwa iliyoanza kukamilika.
Kwa malengo haya Mama Samia usirudi Nyuma. Zaidi naomba tu haya pia yafanyike
1. Wabunge nao waanze kutozwa kodi
2. Wale wote wasiotozwa kodi( Hasa kwenye utumishi) nao waanze kutozwa kodi.
Mama Samia, China unayoiona Leo ni kutokana na maamuzi magumu kwenye maendeleo yaliyofanywa na Mao Zedong na Deng Xiaoping.
Ulaya unayoiona Leo kuna kodi kwenye kila kitu na wananchi wanalipa Kweli.
Rais Samia namaliza kwa kukwambia, usife moyo wala usirudi nyuma. Hayo ndo maamuzi magumu.