Rais Samia atumie kete yake ya mwisho kumaliza utata wa bandari

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,154
4,520
Mpaka sasa tumeachwa gizani hatujui mustakabali wa nchi yetu swala la mkataba wa bandari upande wa utetezi ukimsikiliza Mheshimiwa waziri mkuu ,waziri wa ujenzi na uchukuzi,na msemaji wa serikali hawa wote nimewasikiliza kauli zao kila mtu kila mtu anasema lake lakini bado hawakati kiu ya Watanzania wengi na ndio mana mkataba huu umeendelea kubaki na maswali mengi bila kupata muafaka.

Kauli ya Waziri Mkuu

"Bandari imepewa DP-World kwa kuwa utendaji wa TICTS ni mdogo

Kauli ya waziri wa ujenzi na uchukuzi

"Mkataba huu utakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa mikataba ya nchi mwenyeji na mikataba ya miradi

Kauli ya msemaji wa serikali

"hakuna mpango wa kuuza bandari lengo ni kuongeza ufanisi

Kauli ya mwisho tuliyokuwa tunaisubiri ni kutoka kwa mwanasheria mkuu serikali kutokana na ukimya wake tulitegemea aje na hitimisho sataka hili la bandari lakini naye bado katuacha na maswali mengi tulitegemea moja kwa moja aje na majibu vifungu vya mkataba ambavyo vina utata katika mkataba huo.

Anasema hakuna mkataba tulioingia na dubai yale ni makubaliano.

Swali ambalo wengi wanabaki wanahoji sasa bungeni walikuwa wanajadili nini kama hakuna mkataba

Mpaka hapa tulipofika tumtupie mpira Mheshimiwa rais atutoe hofu watanzania najua siku anaapishwa aliapa kwa vitabu vitakatifu ni muda sasa ajitokeze asizibe pamba masikioni atuambie ukweli nini kinaendelea kwenye mkataba huu.

Mpaka lini hii nguvu ya kuendelea kushambulia wanaopinga mkataba itakoma wanaopinga mkataba wanaambiwa wapotoshaji.
 
Mwanasheria mkuu ameongea sana lakini hakusema makubaliano ya mkataba unaanza lini na unaisha lini?.
 
hatujaingia mkataba ila HAYA ni makubaliano.mkataba Ni NINI na makubaliano Ni NINI MKATABA NI MAKUBALIANO KATI YA PANDE KADHAA ZINAZOHUSIKA,JINSI YA KUENDESHA/KUTIMIZA/KUSHUGHULIKIA JAMBO/ MAMBO WALIYOPANGA. WAWEZA KUWA makubaliano ya KUPANGISHA, KUKODISHA, KUUZIANA MALI, KUAJIRIWA,KUOANA,NK. Hauwezi kusema kuwa SIJAOGA ILA NIMEJIMWAGIA MAJI NA KUJISUGUA NA SABUNI.
 
Suala la bandari linanilazimu kuzirudia hoja zangu kwenye kila bandiko linalohusu mkataba wa IGA unaoipa DPW (kampuni) mamlaka ya kinchi kuendesha na kuboresha bandari badala ya kuingia ubia na TPA au kujisajiri katika Kituo chetu cha Uwekezaji (Tanzania Investment Centre - TIC). Nauliza lakini hakuna anayejitokeza kujibu, kulikoni.

Ni kwa sababu hiyo narejea hoja zangu kuhusu sakata hilo nikiamini kuna atakayejitokeza kujibu

 
CCM ni majizi sana. Baada ya kuona yameiba sana hii nchi yameamua kuiuza kabisa. Huyu sa100 hakutakiwa afike huko kwenye kuuza nchi
 
Back
Top Bottom