Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,273
Suala la bandari mpaka sasa halina jibu linaloeleweka kutoka serikani kutokana na wasemaji wa Serikali wenyewe kupishana na kupingana. Mara waseme mkataba haujasainiwa, mara bunge limepitisha makubaliano, mara wananchi waendelee kutoa maoni wakati muda wake ulishapita ndipo wakapeleka bungeni. Yaani kila mmoja anajisemea kivyake.
Katika yoote yanayosemwa mtu pekee aliyepaswa kumaliza utata huu kwa kutoa kauli ya mwisho alikuwa ni Rais wa nchi. Bahati mbaya sana Rais ametangaza wazi kuwa atakaa kimya. Yaani iwe uwongo au ukweli yeye hajibu chochote. Ni kama ameliweka hilo suala kwenye Auto Pilot. Swali ni kuwa kwanini Rais anyamaze kimya kwenye suala nyeti kama hili wakati naye akiwa katikati ya tuhuma? Anaogopa nini? Je hajiamini? Je anahusika kwenye mgogoro huu?
Nashauri Rais aache kujificha kwenye masuala rahisi kama ya mpira atoke hadharani tusikie kauli yake kuhusu suala la bandari atoe jibu kama mkataba umesainiwa ama Bado?