Rais Samia atoa Milioni 2 kwa anayekumbatia Watoto hospitali ya Amana

Mpaka huyo Dada anaamua kujitolea kuwasaidia watoto njiti kwenye hospitali kubwa kama Amana, ndiyo kusema Serikali haina pesa ya kununulia mashine maalum za kuwasaidia hao watoto!
 
Mbona YY hajitoi na kuhudumia wenye uhitaji mpk anauza BANDARI?
Mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka Bandari yetu.
Asante
Unataka kwa nani sasa!
Kama ni yako si ukaichukue! Unalilia nn hapa ikiwa kitu ni chako mwenyewe, au tukusaidieje wewe na familia yako
 
Hapo kwenye auditing sijajua. Hivi ofisi ya raisi au ikulu huwa zinafanyiwa auditing?
Ikulu haiwi audited. Wala Rais halipi kodi. Hakuna loophole kubwa ya kuchota hela kihalali kama ofisi ya Rais ikiwemo Usalama.

Bajeti ya matumizi ya Ikulu na taasisi zake haihojiwi popote.

Siwalaumu hawa kleptocrats and meatheads wa tawala za enzi hizi. Uchafu huu ni wa founding father himself. Julius Nyerere knew better. Alikuwa member wa Fabian Society akiwa Edinburg University. Fabian Society wanajadili siasa za dunia usiku kucha. He was infinitely exposed and sophisticated in good governance systems of the world.

Lakini akatuletea catastrophic imperial presidency, Ikulu haikaguliwi, Rais halipi kodi. Why the eff ? Third rate Founding Father of a third world nation.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Mariam Mwakabungu (25) anayejitolea kukumbatia watoto njiti waliotelekezwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana jijini Dar es Salaam.

Ujumbe huu umetumwa siku moja tangu mitandao ya Mwananchi Julai 18, 2023 iliporipoti habari kuhusu Mariam na namna alivyosaidia watoto watatu waliotelekezwa na mama zao.

Samia ametuma ujumbe huo leo Jumatano, Julai 19, 2023 uliwasilishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Brayson Kiwelu ambaye amemkabidhi Mariam kiasi cha Sh2 milioni.

Dk Kiwelu amesema ujumbe huo umetumwa na Rais Samia ambaye amekuwa mstari wa mbele katika huduma za mama na mtoto.

"Rais ametoa Sh2 milioni fedha taslim kumpatia mama huyu kwa kujitoa kwake na amewapongeza viongozi wa Wizara ya Afya na Amana kwa ubunifu huu na uthubutu mama huyu kuwa sehemu yetu.

"Rais ameshukuru sana msaada ambao mama huyu ameutoa na amewataka Watanzania kuendelea kujitoa kwa ajili ya kuhudumia wale wenye uhitaji," amesema Dk Kiwelu.

Soma pia - Mwanamke Anayejitolea Kukumbatia Watoto Njiti Waliotelekezwa Hospitali ya Amana

Machawa kina Kitenge wanapewa mil.6 Kwa trip huyu anayefanya kazi ya maana anapewa milion 2?
 
Ushilole sjui magoli wanapewa mihela mingi

Ova
Ni ajabu kweli. Maana kiuhalisia alitakiwa kununua hizo mashine za kutosha na kuhakikisha umeme au standby generator ipo muda wote.

Sasa huyu anafanya kazi ya kitume hii, eti million 2..!!
 
Kwanza nampongeza kwa ujasiri wake wa kufanya hayo anayoyafanya!

Nimefikiria sana,nimejiuliza swali moja, ni Nani aliempeleka Amana,na kumruhusu kuingia wodini?

Je, ktk eneo ulilopo unaweza ruhusiwa from no where uingie wodini Tena za watoto ,hawakujui,hawakutambui,Wala huna Elimu na ujuzi huo?

Huyu Marium-watoto njiti Ni "JASUSI NGULI" ,Kuna zaidi ya hayo!
(Kapelekwa kufanya kitu ambacho wengine si rahisi kukiona) Ila impact yake hatuna siku 8 tutaanza kuiona.

Nawasilisha!
 
Wanapambana kuzima issue ya bandari

Kwamba watanzania ni watu wa huruma sana.

Tunataka bandari zetu.
 
Mataahira wanazidi kuongezeka nchi hii.
Kwaheri bandari.
Tanganyika unazidi kupotezwa
 
Huyu Marium-watoto njiti
Anaitwa Mariam Mwakabungu ni mke na mama wa watoto wawili, sasa sijaelewa lengo lako la kupingana nae maana ameeleza kila kitu kwamba alienda pale akaelezwa situation za watoto wale na akaomba awe anasaidia kuwakuza akakubariwa na uongozi wa hospital nahisi hivyo, nini shida mkuu wangekua hawamtambui si wangesema hawamtambui?
✍️
 
Anaitwa Mariam Mwakabungu ni mke na mama wa watoto wawili, sasa sijaelewa lengo lako la kupingana nae maana ameeleza kila kitu kwamba alienda pale akaelezwa situation za watoto wale na akaomba awe anasaidia kuwakuza akakubariwa na uongozi wa hospital nahisi hivyo, nini shida mkuu wangekua hawamtambui si wangesema hawamtambui?
✍️
Mleta uzi ameandika kama vile wote tunajua hilo sakata..pua pua
 
Anaitwa Mariam Mwakabungu ni mke na mama wa watoto wawili, sasa sijaelewa lengo lako la kupingana nae maana ameeleza kila kitu kwamba alienda pale akaelezwa situation za watoto wale na akaomba awe anasaidia kuwakuza akakubariwa na uongozi wa hospital nahisi hivyo, nini shida mkuu wangekua hawamtambui si wangesema hawamtambui?
✍️
Mkuu ,Ebu fikiria from no where ktk mazingira uliyopo ,uende hospital uwaambie unataka kuhudumia wagonjwa ,then wakuruhusu!

It's impossible
 
Back
Top Bottom