Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Cicadulina

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
962
2,347
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Ndgu. Eric Hamisi. Nafasi yake inachukuliwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndgu. Plasduce Mkeli Mbossa.

1656934333348.png

Mbossa.jpg

PICHA: Plasduce Mbossa​
 
Binafsisha hizi BANDARI, naona zinatupa shida kubwa kuziendesha au recruits freshers kutoka University, peleka wachache pale Durban, Capetown, Rotterdam, Botswana (dry port)wakajifunze kwa 24mth kuhusu uendeshaji wa hizi bandari, na ajira mpya zifanyike yaani we need to start upya
 
Ikibinafsishwa ndio inakufa kabisa. Rejea kilichowahi kutokea kwenye Reli, Shirika la ndege na viwanda
 
Sasa kumtumbua na kumuweka aliyekuwa kaimu wake ndio suluhisho la tatizo?

Bandari inatakiwa ifumuliwe kuanzia chini kabisa mpaka kileleni. Hii mambo ya kuondoa mtu mmoja mmoja huku kuacha mashina na mizizi ni ujinga tu.

Ni ngumu kuamini kama kuna madudu basi yalifanywa na Mkurugenzi peke yake. Kwa vyovyote ni kwa msaada mkubwa wa waliokuwa chini yake. Sasa leo hii ukisema unamuondosha mkurugenzi na kuacha walio chini yake ambao kiuhalisia ndio watekelezaji wakuu wa hayo madudu hapo unakuwa umefanya nini?

Hiki kinachofanyika ni sawa na kuzima moto kwa kutumia mabua, kwa juu unaona kama moto umezimika ila chini unafukuta vile vile.
 
Back
Top Bottom