Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Mh pale bandari sijui nani ata paweza labda wakabidhiwe Jeshi JWTZ

Pale TPA atakayeweza kuleta mabadiliko chanya ni baharia wa kimataifa au kuli wa miaka mingi aliyezamia ktk bandari za nchi nyingi za watu aliyeona mabadiliko mengi halafu akapiga kitabu na ambaye ana maono, anayejua ushindani baina ya bandari na bandari, mifumo ya reli, barabara, kreni n.k inaiwezesha kivipi bandari kuwa tajika kikanda / kimataifa na kimbilio la wateja wengi ndiyo angefaa.

Hili la engineer, corporate lawyer wasioijua bandari wakitokea wizarani au kampuni ya bia au benki n.k ni pagumu sana kwao kujua nini wafanye kuongeza ufanisi, kuziba mianya ya ubadhirifu
 
Huwa nashindwa kuelewa BANDARINI kuna nini?! mbona huwa hakuishi MATATIZO?!
yaani kunaonekana kama kuna miungu watu/ uttachable!!!

Nashauri Jeshi lipewe Jukumu la kuendesha Bandari au waongeza nguvu hapo naamini kutakaa sawa, kama kuna wabishi tupa pembeni.

Huwa najisikia maumivu kila mara Rais analalamikia utendaji wa Bandari sio wa kuridhisha. kama kuna watendaji wanao fanya hujuma ya kukwaza juhudi za Rais wabainishwe na watolewe mara moja.
 
Binafsisha hizi BANDARI, naona zinatupa shida kubwa kuziendesha au recruits freshers kutoka University, peleka wachache pale Durban, Capetown, Rotterdam, Botswana (dry port)wakajifunze kwa 24mth kuhusu uendeshaji wa hizi bandari, na ajira mpya zifanyike yaani we need to start upya
Ulaya bandari nyingi mno zimebinafsishwa hizo za kwetu sijui wanasubiria nini!
 
Huwa nashindwa kuelewa BANDARINI kuna nini?! mbona huwa hakuishi MATATIZO?!
yaani kunaonekana kama kuna miungu watu/ uttachable!!!

Nashauri Jeshi lipewe Jukumu la kuendesha Bandari au waongeza nguvu hapo naamini kutakaa sawa, kama kuna wabishi tupa pembeni.

Huwa najisikia maumivu kila mara Rais analalamikia utendaji wa Bandari sio wa kuridhisha. kama kuna watendaji wanao fanya hujuma ya kukwaza juhudi za Rais wabainishwe na watolewe mara moja.
Hela ni nyingi Sana So HAta kama ni ww Utaacha Kupiga Hizo Hela?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom