residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,020
- 9,609
Ukiwa mlevi,mara nyingi rafikizo wengi watakuwa walevi. Ukiwa mpenda kwenda bar,utakaokutana nao huko bar ndio utakaokuwa nao karibu.Watu dizaini ya Chalamila sijui mwendazake alikuwa anawatoa wapi aisee...!
Ukiwa mcha Mungu,rafikizo wengi watakuwa wacha Mungu. Ukiwa mpenda kwenda kanisani/msikitini,utakaokutana nao huko kanisani/msikitini ndio utakuwa nao karibu.
Ukiwa mgonjwa wa akili,utakuwa muhudhuriaji wa mara kwa mara pale "Taasisi ya Magonjwa" ya Akili karibu na gereza kuu la Isanga. Ukiwa muhudhuriaji wa mara kwa mara wa Mirembe,rafikizo wengi wa karibu watakuwa wana Mirembe wenzako.