Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Kitombile

JF-Expert Member
Mar 21, 2021
438
500
Post #63 ukiingia you tube pia utakuta hotuba nzima aliongea vizuri tu nahisi jamaa analazimishaga utani halafu hauwezi siyo mara ya kwanza kuongeaongea vitu vya kipuuzi.

Ila hiyo siyo hapo naona alikuwa anafafanua kauli yake ngoja nitafute ile clip iko somewhere nitaituma hapa soon
Ila Chalamila ameniuma sana, alikuwa ameanza kuchangamsha jiji.
 

coolboyjsen

JF-Expert Member
Apr 10, 2021
205
250
dah chalamila naona mdomo umemponza amesifiwa juzi kuwa ni mlipukaji ameenda kuropoka anataka wananchi wamtukane raisi.
juzi alikuwa anawaambia ma Dc hawaelewi hatima yao nakujiona yy amemaliza.
achukue pension yake akajiajiri kama vijana wengine.
uongozi ni zamana tu
kazi iendele
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
55,604
2,000
Hmm…huyu mama naye kama Magufuli tu sasa.

Anateua leo, jioni anatengua.

Kesho anateua, keshokutwa anatengua!

Hivi hao wateuliwa huwa hawafanyiwi vetting??

NB: Hizi press releases huwa zinatolewa saa ngapi usiku?
Kuteua ni moja ya majukumu ya rais
Rais asipo teua mtaanza pia kulalamika

Ova
 

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,216
2,000
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

=====

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.

Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae
View attachment 1814796
Batilda Salha Buriani kutoka uraiani Hadi kuwa RAS mama alichemsha. Hivyo amebuni kumpa ukuu wa mkoa cheo Cha kusiasa
 

othuman dan fodio

JF-Expert Member
Jan 2, 2018
2,413
2,000
Viongozi wengi walioteuliwa kutokea upinzani wanafanya vizuri hii inaonesha upinzani unapika viongozi vizuri mf. Juliasi mtatiro, machari hawa vijana mpaka sasa hamjasikia skendo zao japo kuna kipindi mtatiro alitaka kuiga mkumbo wa mwenda zake kwa kuchapa viboko wanafunzi watoro huku akiwa live mainstream nadhani alijirekebisha.

Wengine ni mgwira ambaye amestahafu bila doa na sasa kafulila amepewa mkoa tangu apewe mkoa hatujaskia madoido yoyote, lkn nina mashaka na huyu mlevi mwita waitara naona hana muda mrefu sana kwenye baraza


Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,439
2,000
Chalamila hakujua kuchuja maneno. Hana wa kumlaumu isipokuwa mwenyewe.
Sidhani kama alikuwa mtendaji super kiasi hicho
 

residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,832
2,000
Watu dizaini ya Chalamila sijui mwendazake alikuwa anawatoa wapi aisee...!
Ukiwa mlevi,mara nyingi rafikizo wengi watakuwa walevi. Ukiwa mpenda kwenda bar,utakaokutana nao huko bar ndio utakaokuwa nao karibu.
Ukiwa mcha Mungu,rafikizo wengi watakuwa wacha Mungu. Ukiwa mpenda kwenda kanisani/msikitini,utakaokutana nao huko kanisani/msikitini ndio utakuwa nao karibu.
Ukiwa mgonjwa wa akili,utakuwa muhudhuriaji wa mara kwa mara pale "Taasisi ya Magonjwa" ya Akili karibu na gereza kuu la Isanga. Ukiwa muhudhuriaji wa mara kwa mara wa Mirembe,rafikizo wengi wa karibu watakuwa wana Mirembe wenzako.
 

hito

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
472
1,000
Mbuzi wa kafara. Wadanganyika kesho wanaamka na Agenda ya Charamila wanasahau Mambo ya bajeti na Kodi za 'Ovyo ovyo'
Asilimia 120 wamejaa ccm huku mtapiga kelele were mruke vinyume lakini bajeti imesha pita hiyo hapo hakuna namna tena
 

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
38,904
2,000
Duh Chalamila kaliwa kichwa, pombe itanywekwa kweli? Haha
alizidi uropokaji ulikuwa unadhihaki mamlaka! kuna siku alisema watu watafikiri Samia kamuua Mwendazake! Nikajua huyu hachukui muda alipokuja kusema wananchi waje na mabango ya matusi nikasema aisee! Zimefyatuka! maana maelekezo ya Mwenye nchi sasa yanadhihakiwa mubashara!
 

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
4,431
2,000
Samia ni Magufuli.

Samia aliteuliwa na Magufuli kama alivyoteuliwa Sabaya, Hapi, Majaliwa,Mpango etc

Acha wanafunzi wa Magufuli waumane
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom