Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Nguruka

Senior Member
Dec 6, 2006
135
225
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

=====

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.

Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadaye.

IMG-20210611-WA0003.jpg
 

Jeh

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,944
2,000
Ally Hapi ndo kwanza alikuwa anajitambulisha kwenye wilaya za mkoa wa Tabora. Jumatatu na Jumanne alikuwa anajitambulisha wilaya ya Kaliua, Jumatano na Alhamisi alikuwa wilaya ya Urambo, Ijumaa amehamishwa mkoa.

Sijui kama alishamaliza kujitambulisha Tabora. Kazi Iendelee.
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
142,062
2,000
Chalamila alikuwa anahangaika mno. Juzi hapa nimemuona akiwataka wananchi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kwenye ziara ya Rais atakayoifanya mkoani humo na akawataka waje na mabango ya kutosha - hata kama ni ya matusi sawa tu.

Wakati huo huo mama ameshatoa onyo kuwa hataki kuona mabango wananchi wakiilalamikia serikali; na kwamba mabango hayo yatawa-cost wakuu wa mikoa.

Huu ni wakati wa ku-lay low na kusoma upepo unavyokwenda. Haoni wenzake akina Hapi wako kimya wanahamishwa tu huku na huko utafikiri mpira wa kona?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom